Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo
kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la
kujiuzulu.
Katika
barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba
kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya
Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu
No comments:
Post a Comment