Wageni
mbalimbali wanaoshiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii
ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ulioanza
leo katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) wakifanya
usajili kabla ya kuanza kwa mkutano huo. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
MAKAMU
wa pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, amesema mpango wa
serikali ya Tanzania wa hifadhi ya jamii ndio msingi wa sera ya kuondoa
umaskini miongoni mwa watu wake ili kulifanya taifa kuwa la kipato cha
kati ifikapo 2025.
Kauli
hiyo imetolewa leo wakati akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa
hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya
Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha
kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii.
Katika
Mkutano huo wa siku tatu unafanyika Katika kituo cha kimataifa cha
mikutano cha Arusha (AICC) serikali imefanya maandalizi kwa kushirikiana
na mashirika ya kimataifa kama UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya
utafiti wa sera za kiuchumi yenye makao makuu nchini Afrika Kusini
(EPRI).
Imeelezwa
kuwa mkutamo huo umelenga kuchota maarifa mema kutoka Afrika Kusini ya
namna ya kutengeneza sera za kuhudumia makundi maalumu ya wanawake,
watoto, wazee, wasiojiweza na vijana ili kuboresha maisha yao, ikiwa ni
sehemu ya mpango mkakati wa serikali wa kuinua kiwango cha maisha
miongoni mwa wananchi wake.
Mkurugenzi
msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya
Afrika Aeneas C. Chuma (kulia) akiwasili kushiriki mkutano huo akiwa
ameambatana na Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania,
Bw. Magnus Minja (kulia) pamoja na Luis Frota kutoka ILO Afrika Kusini.
Balozi
Seif Ali Iddi, alisema kwa kuzingatia nia ya serikali ya kuwa taifa
lenye kipato cha kati mwaka 2025 serikali inaona haja ya kuangalia sera
ili iweze kutoa haki kwa makundi yote kuelekea ustawi wa jamii ifikapo
mwaka huo..
“Serikali
imechukua hifadhi ya jamii kama mkakati wa kufikia dira ya ukuaji na
maendeleo nchini. Kongamano hili limekusudia kuhakikisha kwamba muono
unatengeneza hatua stahiki zinazotekelezeka kitaifa kukabiliana na
changamoto za umaskini hivyo kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa
endelevu na wenye maana kwa wananchi” alisema.
Alisema
ili kufikia lengo hilo la uchumi endelevu, serikali inataka kuhakikisha
wananchi wake wakiwemo wale maskini na wasiojiweza wanawezeshwa ili
kutambua haki zao na kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye nguvu na
linalotoa haki sawa kwa wote.
Aidha
kuwa taifa linaloangalia mahitaji ya watoto wake kama lishe, afya na
elimu ili kuwasaidia kukua kwa furaha, kuwa wazalishaji na kukwepa mtego
wa umaskini unazinga kizazi kwa kizazi.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania
Hoyce Temu (kulia) akimwongoza Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la
Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kuelekea
kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri kabla ya kuanza kwa mkutano.
Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw.
Magnus Minja.
Balozi
Iddi alisema kwamba amefurahi kuona kwamba ajenda za mkutano pia
zimegusia kuzungumzia uimarishaji wa utendaji wa pamoja kati ya mipango
ya hifadhi ya jamii kama TASAF, Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na huduma
za jamii zinazotolewa na wizara husika kama wizara ya elimu, afya, maji
nakadhalika.
Hata
hivyo aliwataka washiriki kuangalia ukusanyaji wa takwimu kuhusu
masuala ya hifadhji ya jamii kwani kwa hali ilivyo sasa ukusanyaji huo
si mzuri na unazuia maendeleo na uimarishaji wa huduma za jamii.
Alisema
ipo haja ya kuboresha mazingira ya utawala ili kuwezesha kuimarisha
hifadhi kwa wale waliokwishaipata, kubadili sheria ili kuwaingiza na
wale ambao hawajapata huduma za hifadhi ya jamii.
Aliwataka washiriki kuangalia kwa makini changamoto zinazoikumba Afrika na Tanzania katika masuala ya hifadhi na kutolea majibu.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani
(ILO) na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma.
Alizitaja
baadhi ya changamoto hizo kuwa ni umaskini uliotapakaa ambao
unasababisha watu kushindwa kupeleka michango katika hifadhi, misingi ya
ukataji kodi ambayo huleta mushkeri kwa fedha za hifadhi, kuwepo kwa
kundi kubwa lisilo katika sekta rasmi ya ajira na hivyo kupunguza idadi
ya wachangaji katika prgramu zinazohitaji michango mfululizo na
mabadiliko ya tabia nchi yanayotishia kuyumba kwa kilimo na ufugaji
ambao ndio msingi wa mapato kwa wananchi wengi.
Alisema
pia mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha milipuko ya magonjwa
mbalimbali kama Malaria na magonjwa mengine mapya kama Ebola na Dengue.
Changamoto nyingine ni kuwepo na gharama kubwa za utawala hasa katika siku za mwanzo za uanzishwaji wa mifuko ya hifadhi.
Mkutano
huo wenye washiriki zaidi ya 150 una watu wa kariba mbalimbali wakiwemo
watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka
mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi,
Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji
Tanzania.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi
duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kabla ya
kuwasili kwa mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi.
Mkutano
huo unatarajiwa kutoa mwelekeo wa namna ambavyo Tanzania inaweza
kuanzisha mfumo wa hifadhi kwa ajili ya watu maskini na wale wenye
mahitaji maalumu ili kuwawezesha kupata huduma za afya, elimu na kipato.
Naye
Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa
kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma, amesema Umoja wa Mataifa umefurahishwa
na kuwapo kwa kongamano hilo kwani suala la hifadhi ni msingi wa
maendeleo katika uchumi wowote endelevu.
Alisema
kuwapo kwa Hifadhi ya jamii inayoeleweka na yenye msingi imara husaidia
wananchi kukabiliana na mabadiliko yoyote yale ya kiuchumi katika taifa
lao.
Alisema
shirika hilo katika miaka yote 95 ya uwapo wake inapigania hifadi ya
jamii kama njia salama ambayo inahakikisha ukuaji wa jamii unaozingatia
uwapo wa jamii inayozingatia ukuaji wa uchumi wenye haki kwa kila mmoja.
Waziri
wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya
AICC jijini Arusha kushiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya
jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha huku
akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius
Likwelile (katikati) pamoja na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama
Gulaid.
Pamoja
na mafanikio ya dunia katika masuala ya afya na elimu, Mwakilishi huyo
ameelezea changamoto kubwa inayokabili Tanzania ambayo ni vijana wengi
kuingia katika soko la ajira ambalo ni finyu.
Mwakilishi
huyo amesema kwamba kuanzia mwaka ujao hadi 2030 nchi za Afrika
Kusini mwa jangwa la sahara wanatakiwa kutengeneza nafasi milioni 5 za
kazi kila mwaka ili kuendana na ukuaji wa soko la wasaka ajira.
Alisema
kutokana na ukweli huo hatua ya sasa ya Tanzania kutaka kuwa na msingi
imara ya hifadhi ya jamii ni muhimu sana ili kukabiliana na mabadiliko
yanayokuja katika afya, elimu na ajira.
Wakati
huo huo Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi
mkazi wa UNDP Alvaro Rodriguez amesema hifadhi ya jamii ni kitu muhimu
kinachofanya watengeneza sera kukaa pamoja kuona namna nzuri ya
kufanikisha masuala hayo.
Waziri
wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akiwa na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) pamoja na Naibu
waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana
wakielekea kumpokea mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi.
Alisema
matukio mbalimbali yanayoharibu ustawi wa jamii kama kuporomoka kwa
uchumi duniani, mabadiliko kwenye tabianchi kumefanya kuwepo na haja ya
kuhakikisha kwamba kuna misingi imara ya kutoa hifadhi kwa wananchi na
kuboresha maisha yao.
Akizungumza katika mkutano huo kabla ya Makamu wa rais kuhutubia, Alvaro alisema kuna changamoto kubwa zinazokabili dunia.
Alipongeza
serikali ya Tanzania kwa kuona haja ya kushirikiana na wadau wengine
kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto za maendeleo katika lengo
la kuhakikisha kunauwezeshaji wenye lengo la kuwezesha ustawi wa jamii.
Alisema
mada zitakazojadiliwa zitawezesha mwishoni mwa mkutano kuwapo na
maazimio yenye kuwezesha kutengenezwa kwa mising bora ya hifadhi ya
jamii ili kuwezesha maono ya maendeleo kufikiwa.
Mratibu
huyo pia alielezea kuridhishwa kwake na mafanikio yanayopatikana nchini
Tanzania kupitia TASAF ya kukabiliana na umaskini uliokithiri na kutoa
nafasi ya maskini kuwa na uwezo wa kusonga mbele katika maendeleo ili
kufikia maono ya taifa ya maendeleo endelevu yanayojali watu wote 2025
wakati taifa litakapokuwa la kipato cha kati.
Mgeni
rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya
jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha,
Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif
Iddi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius
Likwelile mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha
leo.
Makamu
wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi ,
akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa
hifadhi ya jamii.
Mgeni
rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi
Seif Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la watoto duniani
(UNICEF), Jama Gulaid.
Mgeni
rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi
Seif Iddi (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum
pamoja na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakielekea
kwenye ukumbi wa mikutano.
Picha
juu na chini ni mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akifungua mkutano mkubwa wa
kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana
uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii
ulioanza leo jijini Arusha.
Kwa picha zaidi ingia humu
No comments:
Post a Comment