Mkuu
wa mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila ameipongeza asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Population
Sevices International(PSI) kwa kazi nzuri ya kutoa elimu ya ukimwi kwa njia ya
sinema na uzazi wa mpango kwa jamii.
Pongezi
hizo alizitoa wakati akikangua mabanda siku ya uzinduzi wa kampeni ya nyota ya
kijani na kutolewa na taarifa ya juu
asasi hiyo kutoe elimu ya ukimwi na uzazi wa mpango sehemu mbalimbali mkoani
hapa.
Mwananzila
alisema kwamba jamii inatakiwa kuwa salama na kuyatuza maisha yao kwa
kuzingatia uzazi salama kwa kutumia njia sahihi ya uzazi wa mpango kwa lengo la
kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na wato wachanga.
Alisema
elimu bado inahijatika sana kwa jamii
hasa maeneo ya mijini na vijiji kwani huko ndiko elimu hajiafika kiasi cha kutoasha hivyo
jududi za dhati zinahitajika ili kuwafikia wananchi walio wengi.
Alisema
kiwango cha uzazi nchini kimepungua ila bado ipo juu kwani mwaka 1991-1992
kilikuwa watoto 6.3 kwa kila mwanamke na katika mwaka 2010 kilishuka hadi
kufikia watoto 5.4, na kwa vijijini 6.1.
Mwananzila
alisema katika maeneo ya vijijini kuna kiwango kikubwa cha kuzaliana na elimu
haijawafikia walengwa hivyo serikali ina mikakati ya kupeleka elimu pamoja na
huduma katika maeneo hayo ili kuwa karibu na kupandisha wastani wa Taifa wa
asilimia 60 ifikapo mwaka 2015.
Awali
meneja mauzo wa psi mkoa wa tabora, Gabriel Setumbi alisema kwamba asasi yake tayari imefikia vijiji
vipatavyo 89 kwa ajili ya kutoa elimu ya ukimwi kwa njia ya sinema .
Aidha
alisema licha ya kutoa elimu ya sinema lakini pia wamekuwa wakisambaza biddha
za afya kwa ajili ya kupambana na mambukizi ya ukimwi uzazi za mpango.
Alisema
kwamba asasi hiyo inashirikia na wizara ya afya kuhakikisha itoa huduma sahihi
ya uzazi wa mpango kwa kinamama na wanaume katika sehemu mbalimbali za mkoa wa
Tabora.
Mwisho
No comments:
Post a Comment