Kulia
ni Kulwa na kushoto ni Dotto Mwaibale wakiwa na sura za Majonzi wakati
wa Ibada fupi ya Kumuombea Mama yao Mpendwa kabla ya kuanza Safari ya
kwenda Mbeya
Wa
kwanza Kulia ni Mdogo wao wa Mwisho wa Akina Mwaibale Ambwene na wa
pili kutoka kulia ni Dada yao Mkubwa wa akina Mwaibale Mary Anyitike
ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa
Mwili wa Marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mfumu
mama yao Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale ukiwa unaandaliwa tayari kwa kuombewa, Kuagwa na kusafirishwa
Mchungaji
Ephraim Mwakajwanga Akiwa anaongoza Ibada ya Kumuaga Mama mzazi wa
Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale Bi. Twitikege Mlagha Mfumu leo katika
Hospitali ya Temeke
Baba
Mchungaji akitoa Neno la Kiroho (Mahubiri mafupi) wakati wa kuuaga
Mwili wa Marehemu, Katika Mahubiri hayo alisisitiza kuwa Duniani
tunapita kila kitu kinabaki hivyo ni vizuri kila mmoja ajiandae na kuwa
mama ametangulia na sisi tunafuata hivyo yatupasa kuwa tayari
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Abdalah Mrisho akitoa salam za
Rambi rambi kwa wafiwa ambapo Kulwa Mwaibale anafanyia kazi hapo.
Joachim Mushi akisoma utaratibu na kutoa maelezo mbalimbali wakati wa shughuli za kuuaga mwili wa Marehemu.
Muwakilishi
kutoka Jambo Concept ambao ndio wachapishaji wa Gazeti la Jambo leo
ambapo Dotto Mwaibale anafanyia kazi huko Mkurugenzi Beny Kisaka wakitoa
salam za Rambi rambi ambapo walitoa mkono wa pole wa kiasi cha Shilingi
Laki tano.
Muwakilishi kutoka Skauti ambako Dada yao Mkubwa wa akina Mwaibale anafanyia kazi akitoa salam za Rambi rambi
Msemaji
wa kwa Niaba ya Familia Noah Mwakalasya akitoa neno la Shukurani kwa
niaba ya wanafamilia na kushukuru kwa moyo waliojitolea kuja
kumsindikiza mama yao mpendwa
Dada
Mkubwa wa akina Mwaibale Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu
Msaidizi wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa akisoma wasifu wa Marehemu
mama yao
No comments:
Post a Comment