Rais
Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku na
kumpendekeza waziri mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi hio.
Wakati
huohuo mkuu wa polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo
amejiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yake afanye hivyo kwa kushindwa
kukabiliana na utovu wa usalama nchini.
Rais
Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali
'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Rais
alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo
jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera
Kaskazini ya Kenya.
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.
Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.
Hatua
ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa
jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu
wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.
Uteuzi
wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani
atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.
Alipokuwa
anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza mda wa vikao
vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua
nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili
wamuidhinishe.crdt BBC Swahili
No comments:
Post a Comment