Friday, September 21, 2012

WIKI YA USALAMA BARABARANI MKOANI TABORA


Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akikata Utepe ikiwa ni Ishara ya ufunguzi wa Wiki ya  Nenda kwa usalama barabarani mkoani Tabora,kutoka kushoto ni Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani  SSP Hamisi Kisandu,Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Rage na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini. 

Baadhi ya askari wa usalama barabarani wakiwa katika maandamano wiki ya Usalama iliyofanyika Stendi mpya ya mjini Tabora.


Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani  mkoa wa Tabora SSP Hamisi Kisandu akisoma risala fupi katika hafla ya ufunguzi wa wiki ya usalama barabarani.

Maandamano ya Bajaji za mizigo yakipita mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.

 Mkurugenzi mkuu wa kampuni la usafirishaji la mabasi ya NBS Bw.Hamdani Nassor akiwatunza waimbaji wa kikundi cha kwaya cha Shule ya msingi ya Town School wakati walipokuwa wakitumbuiza katika hafla hiyo ya wiki ya usalama barabarani iliyofanyika kimkoa Stendi mpya ya mabasi mjini Tabora.

WILAYA YA SIKONGE YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI.

 Na mwaanshi wetu Sikinge
HALMASHAURI ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora licha ya kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi wake inakabiliwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa shughuli zake za kila siku kwa sababu ya upungufu wa watendaji katika idara mbalimbali za halmashauri hiyo.
 
Akizungumza na mwandishi wetu, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Bw. Paul Nkulila alibainisha kuwa athari zinazotokana na upungufu huu wa watumishi ni utoaji wa huduma usioridhisha, pamoja na watumishi kukosa ari ya kufanya kazi kwa kuwa mtumishi mmoja kwa wastani anafanya kazi ya watu wawili hadi watatu jambo ambalo huchangia ucheleweshaji wa shughuli nyingi za kimaendeleo ndani ya halmashauri hii.
 
Bw. Nkulila alisema kuwa idara zilizoathirika kwa upungufu wa watendaji  kwa kiasi kikubwa ni  idara ya  Afya, idara ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Utawala, Kilimo, Mifugo na Ushirika. Idara zingine zenye mapungufu kidogo ni Manunuzi, Ukaguzi wa ndani, Ujenzi, Sheria na Maji.
 
Aidha Bw. Nkulila alitaja sababu kuu za upungufu huu wa watumishi kuwa ni mazingira yasioridhisha kufanyia kazi ambayo huwafanya watumishi wengi kufika na kuhama baada ya muda mfupi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa nyumba za kuishi watumishi wanaofanyia kazi vijijini mfano walimu na watoa huduma za afya.
 
Akitoa takwimu za upungufu wa watumishi katika halmashauri hii Afisa Utumishi wa halmashauri hii Bi. Flora Malima alisema kuwa  idara ya Afya ina upungufu wa watumishi 271 katika vituo mbalimbali vya Afya  kati ya mahitaji ya watumishi 511, idara ya Elimu ya Msingi ina upungufu wa waalimu 270 kati ya 876 wanaohitajika wakati  Elimu ya Sekondari inaupungufu  wa waalimu 129 kati ya 270 wanaohitajika.
 
Aidha Bi. Malima  aliongeza kuwa idara ya Utawala katika kada zake zote kuanzia maofisa wa vijiji, kata hadi wilaya ina upungufu wa watumishi 63 kati ya 150 wanaohitajika, idara ya Maji ina upungufu wa watumishi 6 kati ya 20 wanaohitajika, idara za Ushirika, Kilimo na Mifugo kwa pamoja  zina upungufu wa watumishi 53 kati ya 116 wanaohitajika wakati idara ya Manunuzi ina upungufu wa watumishi 4 kati ya 6 wanaohitajika na idara zilizobaki zina upungufu wa watumishi kati ya 1 na 2.
 
Bi.Malima akifafanua mikakati ya kumaliza tatizo hilo , alisema kuwa mwaka jana waliomba kibali cha kuajiri ila hawakupata, hivyo wamepanga kuomba tena mwaka huu ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya kujaza nafasi za kada mbalimbali.
 
Aidha Bi. Malima alitaja mkakati mwingine kuwa ni kuongeza nyumba za watumishi ambapo kwa kuanzia tayari wamepata fedha kiasi cha sh. million 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 10 za watumishi wa afya kwa mwaka huu wa fedha, lakini pia wanafikiria uwezekano wa kuwa na utaratibu wa kuwalipia pango watumishi wanaopangiwa kituo cha kazi hapa wilayani Sikonge.

Wednesday, September 19, 2012

MKUU WA MKOA WA TABORA MHE. FATMA MWASA KATIKA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA 26 LA SAYANSI NA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA CHAMA CHA WATAALAM WA MAABARA ZA TIBA TANZANIA (MeLSAT) ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA-TABORA-TANZANIA TAREHE 19 SEPTEMBA, 2012














WATAALUM WA MAABARA NCHI WAKIWA KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA

WAJUMBE WA KONGAMANO LA 26 NA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA CHAMA CHA WANASAYANSI WA MAABARA WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA TABORA FATUMA MWASSA KATIKA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA

WATAALAM WA MAABARA WATAKIWA KUTOCHANGANYA SIASA NA TAALUMA YAO


WATAALAM WA MAABARA WATAKIWA KUTOCHANGANYA SIASA NA TAALUMA YAO
 Na Lucas Raphael,Tabora
WATAALAM wa Maabara za tiba Tanzania (MeLSAT), wametakiwa kutojiingiza katika mambo ya Siasa na badala yake wajikite zaidi katika kazi yao ya kutoa huduma kwa wagonjwa.
Wito huo ulitolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi Fatuma Mwassa wakati akifungua kongamano la 26 la Sayansi na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Maabara za tiba Tanzania uliofanyika katika ukiumbi wa chuo cha utumishi wa umma mjini Tabora.
Bi Mwassa alisema kwamba kwa mtaalam wa maabara kujihusisha na Siasa ni kutoitendea haki jamii, hivyo akawataka kuacha maramoja kujihusisha mambo ya siasa ili kuongeza ufanisi kazini kwa kuwahudumia wagonjwa kikamilifu.
“Mimi huwa inauma sana wanasayansi kujiingiza katika msuala ya siasa, na nilikuwa nasubili mahala pa kusemea, sasa leo nimepata sehemu hii napenda sana nisisitize jambo hili, achani kabisa kutamani siasa, mtaua watu ninyi ni watu muhimu sana kwa taifa” alisisitiza Bi Mwassa.
“Ndugu wanasayansi nawaomba sana mpiganie taaluma yenu msije mkajiingiza kabisa kwenye mambo ya haya ya kisisa” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kongamano hilo liwe chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya mabara za tiba hapa nchini na kwamba wataweza kupata fursa ya kubadilishana uzuefu, kuwajengea uwezo zaidi wa kuwahudumia wagonjwa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili sehemu zao za kazi.
“Taaluma ya mtu wa maabara ni mhimu sana kwa wagonjwa maana hawezi kwenda kwa daktari kutibiwa bila kupitia kwa mtaalam wa kupima magonjwa” alisema Bi Mwassa.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba, kwa kuwa wataalam wa maabara ni msingi wa kupata tiba kwa mgonjwa, hivyo hawana budi kufanya kazi kwa bidii ili jamii iweze kupata huduma hiyo muhimu kikamilifu.
Aliwataka kuimarisha uhusiano na kuongeza ubunifu sanjali na kutafuta fursa pamoja na kuzitumia vivuri katika maeneo yao ya kazi, kwa lengo la kuboresha huduma za uchunguzi katika hospitali wanazofanyia kazi.
Awali Rais wa chama cha wataalam wa maabara za tiba hapa nchini Bw. Sabas Mrina alisema kwamba kongamano hilo limelenga zaidi kuimarisha ushirikiano ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa jamii wanayoihudumia.
Alisema kuwa pia kongamano hilo limelenga kuleta ushirikino baina ya madaktari na wataalam wa maabara za  tiba, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa kutoa huduma hiyo muhimu kwa wagonjwa.
Mwisho


Friday, September 14, 2012

WANANCHI WAOMBA KUPATIWA KIVUKO


Na Lucas Raphael,Tabora

W
ANANCHI wa kijiji cha mbutu na kata ya mbutu katika  wilaya ya  Igunga Mkoani Tabora wameitaka serikali wilayani humo kuharakisha ujenzi wa Daraja la mto mbutu kabla ya msimu wa mvua za masika hazija anza kunyesha ,ikiwa na kuwapatiwa kivuko endapo Daraja hilo litachukua muda mrefu kukamilika.




Wakizungumuza na gazeti hili lilipo tembelea Daraja hilo wa lisema kuwa Daraja hilo limekuwa nitatizo kubwa kwa wananchi wa Igunga hasa katika kipindi cha masika.

Wameiomba serikali kuharakisha ujenzi huo wa daraja kwa muda uliopangwa ikiwa na kuwapatia kivuko cha dharula ili kuwa epushia adha ambazo walikuwa wakizipata.

Evalist Juma ni mmoja ya wananchi wa kata ya Mbutu akizungumuza kwa nyakati tofauti alisema kuwa Daraja hilo ni kiungo muhimu kwa wananchi wa igunga katika shuguli mbalimbali za kijamii na biashara.

Alisema kuwa kwakipindi hiki ujenzi unaendelea serikali iwapatie kivuko cha dharula ambacho kitaweza kuwa saidia kuvuka wakati shuguli za ujenzi huo zinaendelea.

Evalist alisema katika Daraja hilo watu wengi wamepoteza maisha  wakati wa mvua za masika hali ambayo imekuwa tishio kubwa kwa wananchi wa igunga pamoja na kwa wanasiasa.

‘’Daraja hili nitishio kubwa sana kwa wananchi watu wengi wamekufa hapa kutokana na kubebwa na maji wakati wa mvua za masika tunaiomba serikali ifuatilie suala hili mapema hata viongozi wa siasa wanalijua hili’’alisema Evalist.

Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu aliwaha kikishia wananchi wa Igunga kuwa serikali inaendelea na ujenzi huo wa Daraja kwa viwango vikubwa ili kuhakikisha linatumika mapema.

Alisema kuwa Mkandarasi wa ujenzi huo yupo kazini anaendelea na kazi hata hivyo kuhusu suala la kivuko mkuu huyo hakuweza kuzungumzia suala hilo.

Aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kuwa watulivu kwa kipindi hiki na kuwataka kuwa kazi zote za kimaendeleo zitaendelea kufanyika kama hapo awari jinsi zilivyo kuwa zikifanyika.

Mwisho.