WATAALAM WA MAABARA WATAKIWA
KUTOCHANGANYA SIASA NA TAALUMA YAO
Na Lucas Raphael,Tabora
WATAALAM wa Maabara za tiba Tanzania (MeLSAT), wametakiwa
kutojiingiza katika mambo ya Siasa na badala yake wajikite zaidi katika kazi
yao ya kutoa huduma kwa wagonjwa.
Wito huo
ulitolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi Fatuma Mwassa wakati akifungua kongamano
la 26 la Sayansi na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Maabara za
tiba Tanzania uliofanyika katika ukiumbi wa chuo cha utumishi wa umma mjini
Tabora.
Bi Mwassa
alisema kwamba kwa mtaalam wa maabara kujihusisha na Siasa ni kutoitendea haki
jamii, hivyo akawataka kuacha maramoja kujihusisha mambo ya siasa ili kuongeza
ufanisi kazini kwa kuwahudumia wagonjwa kikamilifu.
“Mimi huwa
inauma sana wanasayansi kujiingiza katika msuala ya siasa, na nilikuwa nasubili
mahala pa kusemea, sasa leo nimepata sehemu hii napenda sana nisisitize jambo
hili, achani kabisa kutamani siasa, mtaua watu ninyi ni watu muhimu sana kwa
taifa” alisisitiza Bi Mwassa.
“Ndugu
wanasayansi nawaomba sana mpiganie taaluma yenu msije mkajiingiza kabisa kwenye
mambo ya haya ya kisisa” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Aidha mkuu huyo
wa mkoa alisema kuwa kongamano hilo liwe chachu ya kuleta mabadiliko katika
sekta ya mabara za tiba hapa nchini na kwamba wataweza kupata fursa ya
kubadilishana uzuefu, kuwajengea uwezo zaidi wa kuwahudumia wagonjwa pamoja na
kujadili changamoto zinazowakabili sehemu zao za kazi.
“Taaluma ya mtu
wa maabara ni mhimu sana kwa wagonjwa maana hawezi kwenda kwa daktari kutibiwa
bila kupitia kwa mtaalam wa kupima magonjwa” alisema Bi Mwassa.
Mkuu huyo wa
mkoa alisema kwamba, kwa kuwa wataalam wa maabara ni msingi wa kupata tiba kwa
mgonjwa, hivyo hawana budi kufanya kazi kwa bidii ili jamii iweze kupata huduma
hiyo muhimu kikamilifu.
Aliwataka
kuimarisha uhusiano na kuongeza ubunifu sanjali na kutafuta fursa pamoja na
kuzitumia vivuri katika maeneo yao ya kazi, kwa lengo la kuboresha huduma za
uchunguzi katika hospitali wanazofanyia kazi.
Awali Rais wa
chama cha wataalam wa maabara za tiba hapa nchini Bw. Sabas Mrina alisema
kwamba kongamano hilo limelenga zaidi kuimarisha ushirikiano ili kuendelea
kutoa huduma bora zaidi kwa jamii wanayoihudumia.
Alisema kuwa pia
kongamano hilo limelenga kuleta ushirikino baina ya madaktari na wataalam wa
maabara za tiba,
lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa kutoa huduma hiyo muhimu kwa wagonjwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment