Tuesday, September 25, 2012

MWENGE WA UHURU WAZINDUA NYUMBA BORA ICHEMBA


 Na Lucas Raphael,Tabora
WANANCHI wilayani Kaliuwa mkoani Tabora wametakiwa kujenga nyumba bora zitakazo weza kudumu kwa muda mrefu tofauti na sasa baadhi yao hujenga nyumba zisizo bora kulingana na vipato vyao vya  kilimo cha tumbaku katika wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa jana na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Capt Honest Mwanosa wakati akizundua nyumba bora ya diwani wa kata ya Ichemba John Kadutu yenye thamani ya million 40.
Alisema kuwa baadhi ya wakulima wa maeneo hayo hulima mazao ya biashara lakini kipato hicho hutumika kwa matumizi yasiyo ya msingi ikiwa na ulevi pamoja na kuoa wake wengi kuzidi uwezo wao.
Honest akiwahutubia wanan chi wa Kata ya Ichemba alisema kuwa ujen zi wa nyumba bora kwa mkulima ni mhimu zaidi kuliko kuendelea na ulevi pamoja na anasa mbalimbali.
Aliwataka wananchi hao wabalike na kuiga mfano wa Diwani huyo pamoja na wananchi wengine katika kata hiyo ili kubadili maisha pamoja na mazingira ya kata hiyo.
Akitoa maelekezo kwa wafanya kazi wa sekta mbalimbali kiongozi huyo wa mbio za mwenge aliwataka nawao kujenga nyumba bora kama hiyo ili kuwa mfano kwa wananchi wengine pamoja na kujijengea msingi bora wa maisha.
Daadhi ya wananchi wa kata hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti walimpongeza Diwani huyo kwa kuonesha mfano bora wa nyumba hiyo na kutoa ahadi ya kuiga mfano huo.
John Kitudu Diwani wa kata hiyo alisema kuwa nyumba hiyo imeghalimu kiasi cha shilingi milioni  40 kwa ujenzi wake na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuiga mfano huo.
Alisema kuwa wananchi wa kata hiyo wanakipato kikubwa lakini baadhi yao hutumia kipato hicho kwa matumizi ya pombe pamoja na starehe na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kubadilika kutokana na hali hiyo.
Katika wilaya hiyo mwenge huo umezindua miradi yenye thamani ya shilingi milioni 300 ambapo bado upo mkoani hapa ukiendelea kuzindua miradi mingine kwa wilaya nne zilizo salia.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment