Na Lucas Raphael,Tabora
SOKA
MDAU wa
mchezo wa soka,mkoani Tabora,ambaye ameanzisha mashindano ya kombe la Godfrey
Kasanga Challenge Cup, Godfrey Kasanga,amesema baada ya kufanikiwa katika kombe
hilo kwa kushikisha kila kata, sasa amegeukiwa mashindano kwa mchezo wa mpira
wa pete.
Kasanga
alisema hayo wakati akifanya mazungumzo na gazeti hili,mwanzoni mwa wiki hii.
Alisema
licha kuweka progaramu zake vizuri,na kufanikiwa sana kwenye mashindano ya
kombe la Godfrey Kasanga Challenge Cup,sasa kombe hilo pia naanzisha kwa upande
wa netiboli, ili kuinua vipaji kwa upande huo wa jinsia.
Kasanga
alisema mtindo alioutumia kwenye mashindano ya upande wa wanaume ndiyo
atakaoutumia kwa wanawake na kwamba zawadi hazitapishana sana.
Aliongeza
kuwa siku za kuanza kwa mashindano ya mpira wa pete,atayatangaza hivi karibuni
baada ya kufanikisha miapngo ya udhamini.
Katika hatua
nyingine mdau huyo alisema,pamoja na kuanzisha mashindano hayo,pia natarajiwa
kutoa motisha kwa makocha wa mpira wa soka na pete ili kuweza kutoa nafasi ya
watalaamu hao kuibua vipaji zaidi na kuipenda kazi yao.
“Kutangaza
mashindano pekee haitoshi…..kinachotakiwa sasa ni kuangaliwa kwa makocha katika
suala la motisha kwani hili nina imani kubwa litasaidia kupata timu
zitakazokuwa zinapatiwa mafunzo na makocha wetu.”alisema Kasanga.
Alisema alifanikiwa sana kwenye
mashindano ya kombe aliloanzisha kwa upande wa wanaume,na kwamba safari hii
anatarajia kutafuta udhamini mkubwa zaidi kwa kuboresha zawadi kwani kwa
mashindano yaliyopita alitumia fedha zake za mfukoni.
Hata hivyo
alisema mashindano ya upande wa wanawake kwa maana ya mpira wa pete,alisema
atajikita zaidi maeneo ya kata za mjini kwani hana imani kama vijijini
atafanikiwa kupata timu kadhaa zitakazoshiriki kombe hilo.
Aidha
alisema na kusisitiza kuwa atawasihi viongozi wa pande zote mbili katika
michezi ya soka na pete ili kuweza kuona ni jinsi gani mashindano hayo yanaweza
yatakuwa na mvuto na kuweza kupata wadhamini watakaonogesha zaidi.
“Lakini bado
napenda kutoa wito zaidi kwa wadau wa soka mkoa Tabora,wajitokeze zaidi
kuniunga mkono ili mipango nitakayoianzisha ifanikiwe na kuweza kurejesha
Tabora iliykuwa na timu
ambazo hadi leo zimeweka rekodi ya kimichezo.
Alisema hadi
sasa amejipanga vya kutosha na muda siyo mrefu mashindano aliyoanzissha
yataanza kurindima na kuwataka wakzazi wa Tabora wakae mkao wa kula na burudani
tosha.
Mwisho-
No comments:
Post a Comment