Na Lucas Raphael,Nzega
walamikia kuuziwa kwa Damu hospitali ya wilaya ya Nzega
BAADHI ya wananchi Wilayani Nzega Mkoani Tabora
wamewalalamikia baadhi ya wahudumu wa
Kitengo cha Maabara katika Hospitali ya
wilaya ya Nzega kwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza Damu.
Wakizungumza na
waandishi wa habari kwa nyakatati tofauti wananchi hao walisema kuwa baadhi ya
watumishi wa kitengo hicho cha maabara wanajihusisha uuzaji wa damu pindi
wangonjwa wanapo hitaji huduma hiyo.
Walisema kuwa
kitendo cha kuuza dama ni kinyume na taratibu za utendaji wa kazi hiyo na
kuongeza kuwa baadhi ya watu hushindwa kumudu gharama hizo na kupelekea
kuhatarisha maisha ya watu na wengine kupoteza maisha yao kutokana na biashara hiyo haramu.
Taarifa hizi za
biashara haramu ya damu zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu
lakini hakuna hatua zinazo chukuliwa mpaka kupelekea wagonjwa kadhaa kupoteza
maisha kutokana na upungufu wa dama wakati huo huduma hiyo ipo hospitalini
hapo.
Wameziomba
taasisi mbalimbali ikiwepo na takukuru kuchunguza kwa umakini tatizo hilo ilikukomesha
Biashara hiyo haramu ya damu ikiwa na kuchukua maamuzi magumu ya kuwafikisha
mahakamani watuhumiwa watakao bain ika.
‘’Mimi nilikuwa
na dada yangu anajifungua bahati mbaya alitoka damu sana
tukaambiwa anahitaji damu lakini tulijitokeza wengi kupima tukaambiwa damu zetu
haziko sawa na ya mgonjwa wakasema kuna mtu anajitolea kutoa damu lakini mpatie
chochote hali hiyo iliendelea mpaka dada yangu alipoteza maisha’’alisema mmoja
ya wananchi jina lake
limehifadhiwa.
Waliongeza kuwa
damu hiyo huuzwa kuanzia shilingi 50,000 mpaka 40,000 na zaidi ya bei hizo
kutokana na mteja atakae jitokeza.
Kisasu Sikalwanda
ni katibu wa hospitali hiyo ya wilaya alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikiri kuwepo
kwa malalamiko hayo ya wananchi kuuziwa damu na kudai kuwa kitendo cha kuuza
damu ni kosa katika idara hiyo.
Alisema tayari
hatua za awali zimechukuliwa na kupelekwa ngazi za juu za uongozi zinaendelea
kufanyiwa kazi na kuongeza kuwa damu katika hospitali hiyo ipo kwa sasa na
kuwataka wananchi hao kutoa ushirikiano katika uongozi husika.
Aliwataka
watumishi wa kitengo hicho cha maabala na watumishi wengine wafuate taratibu na
maadili ya utendaji kazi sambamba na kuachana na vitendo hivyo haramu.
Sikalwanda
alisema kuwa wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema kwa uongozi na hatua kari
zitachukuliwa aliongeza kuwa taasisi mbalimbali ikiwepona takukuru ziwasaidie
wananchi hao kukomesha vitendo hivyo vichafu katika Hospitali hiyo ya wilaya.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment