Na Lucas Raphael,Nzega
CHAMA cha Msaraba Mwekundu wilayani
nzega Mkoani Tabora kinatarajia kuanza kuchangisha damu kwa wanachama wake ili
kuondoa tatizo la upungufu wa dama katika Hospitali ya wilaya Nzega.
Kauli hiyo imetolewa baada ya Hospital ya wilaya
ya Nzega kuwa na tuhuma za kuuza damu kwa wananchi mpaka kupelekea baadhi ya
wagonjwa kupoteza maisha yao.
Akizungumuza katika uzinduzi wa chama hicho jana Mwenyekiti
wa chama hicho wilaya ,Gabriel Gibson alisema kuwa chama hicho kimejipanga kutoa
Elimu ya utoaji damu kwa wana chama wake pamoja na wananchi.
Lengo la kutoa damu ni kutaka kukabiliana na
upungufu wa damu uliopo katika Hospitali ya wilaya ya Nzega na kuwa saidia
wananchi watakao bainika wana upungufu wa damu.
Aliwataka wananchi kwa ujumla wilayani hapa
kukipokea kwa mikono miwili chama hicho cha msaraba mwekundu ilikiweze kuleta
uzalendo kwa wananchi na kurejesha nyuma upendo kwa jamii husika tofauti.
Akitoa angalizo kwa wananchama watakao jiunga
katika chama hicho kuwa wasiingie kwa masirahi yao binafsi bali waingie kwa kujitolea kwa
jamii ilikuweza kuleta ufanisi zaidi katika kujitolea kwa shuguli mbalimbali za
kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi ambaye ni
mlezi wa chama hicho alisema kuwa wananchi wanapaswa kujitolea katika kuchangia
damu pindi zoezi hilo
litakapo anza kupitia chama hicho.
Aliongeza kuwa chama hicho nichaki jamii zaidi
hivyo wanapaswa kujitolea zaidi na kuwa wazaledndo kwa nyakati tofauti ili
kuleta upendo katika jamii pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii
ikiwepo na majanga ambayo hutokea mara kwa mara katika jamii husika.
Mratibu wa chama hicho wilaya ,Liliani Kuhasi
akitoa angalizo alisema kuwa dam itakayo changwa na wananchi itatunzwa kwa
uangalifu pamoja na matumizi sahihi ya wagonjwa watakao hitaji hudum hiyo
muhimu na kuongeza kuwa ulinzi mkali utaimalishwa katika utunzaji wa dam hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment