MWIGULU MCHEMBA AIPASHA CHADEMA.
Na,LUCAS RAPHAEL IGUNGA
MWEKAHIZINA wa chama cha mapinduzi ccm taifa
,Mbunge wa jimbo la Iramba Maghalibi Mwigulu Mchemba amesema kuwa chama cha Demokrasia na maendeleo
chadema kina weka chuki kwa wananchi wa Tanzania na pamoja na kusababisha
mauaji ya raia wema.
Alisema hayo jana katika mkutano wa chama cha
mapinduzi(CCM) uliofanyika katika viwanja vya sokoine wilayani Igunga kuwa
chadema wanasababisha mauaji ya raia kwa
masirahi yao huku
akitolea mifano ya mikoa ya Arusha,Morogoro pamoja na jimboni kwake Iramba
Maghalibi.
Alisema chadema kinafanya kazi kupandikiza chuki
kwa wananchi kwa kutumia mikutano yao
ikiwa na mauaji kila kielekeapo chama hicho pamoja na kukazana kulituhumu jeshi
la polis kuhusika na mauaji hayo.
’’chadema wanaeneza mauaji kasha wanawasingizia
polis lakini mauaji hayo yote yana sababishwa na chadema hivyo wananchi
waogopeni hawa ni mashetani’’alisema Mbunge huyo.
Alieleza kuwa chadema hawafurahii maendeleo ya
wananchi kwa kile walicho kifanya cha kukata rufaa katika ubunge wa Dkt,Kafumu
kwa kushinikiza malalamiko yasiyo ya msingi.
Alisema hoja zilizo pelekwa na chadema katika
mahakama kuu ya kanda ikiwa ni pamoja na ugawaji wa mahindi,ahadi za daraja la
mbuntu,kutoa kauli ya bakwata na hoja yingine zilizo somwa na mahakama hiyo sio
za msingi kutengua jimbo hilo ambapo shuguli za ugawaji mahindi na mambo
mengine ya kiserikali yalikuwa yakiendelea kama kawaida kwa nyakati mbalimbali.
Alisema wananchi wa Igunga walikuwa na njaa hivyo serikali
iliweza kupeleka misaada hiyo kwa wananchi wake pamoja na kutekeleza ahadi yake
ambaqyo ilikuwepo katika irani ya chama hicho cha ujenzi wa daraja la mbutu.
Mwigulu alisema kuwa wapinzani wote hawajapata sera
mbadala ya kuwa ongoza wananchi hivyo bado hawana uwezo wa kuweza kuongoza nchi
hii.
Aliongeza kuwa Jaji aliye toahukumu hiyo ya
Dkt,Kafumu anakaa kijiji kimoja na
mwenyekiti wa chadema Freemani Mbowe hivyo ilikuwa lazima jaji huyo awasaidie
katika kesi hiyo.
Ambapo jaji aliye kuwa akiendesha kesi hiyo ni
Jaji Mery Nsimbo shangali
‘’Jaji huyo aliye amua toa hukumu hiyo anakaa
kijiji kimoja na mwenyekiti wa chadema mbowe hivyo lazima awapendelee katika
maamuzi hayo ili mahusiano yawe mazuri zaidi’’alisema.
Alisema viongozi wa chadema hawana upeo zaidi wa
kuona mbali hasa kwa kushangilia mambo yasiyo ya msingi ikiwa ni pamoja na
kutuhumu rais kikwete kwa kuendekeza suala la dini.
Alisema hata kama uchaguzi mdogo ukifanyika
jimboni Igunga ccm itashinda kwa kishindo kutokana na chama hicho kuweka mizizi
sehemu mbalimbali za jimbo hilo.
‘’Iwe usiku,mchana,mashariki,maghalibi,kazikasini,kusini
lazima ccm itashinda kwani jimbo hilo
nilakwetu lazima tushende’’alisema mchemba.
Akiwa hakikishia siku chache zijazo chama hicho
kitakata rufaa katika mahakama kuu ya rufaa kwa kutumia hoja mbandala ambazo
zilizo chambuliwa na wana sheria wa chama hicho.
Alisema hoja hizo nitofauti na zile alizo kuwa
akidai katibu mkuu wa chadema Dkt, slaa kuwa ccm haina uwezo wa kukata rufaa
hiyo kutokana na hoja zilizo mbele ya mahakama ya rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya ccm vilidai kuwa
chama hicho kimefanya mkutano huo kutokana na chadema kufanya mkutano katika
eneo hilo kwa
kutoa maneno juu ya m aamuzi ya mahakama hiyo.
’’Lengo ni kujibu hoja za chadema hivyo ndio maana
tumeamua na sisi tufanye mkutano huo ilituwe wazito hapa mjini igunga’’kilisema
chanzo hicho.
Awari ya hapo katibu Mkuu wa
chama cha Demokrasia
na Maendeleo(chadema) Dkt,Willbrod slaa akiwa katika viwanja hivyo vya sokoine
wiki chache zilizo pita alikitahadhalisha chama cha mapinduzi kukata rufaa kisije
kika umbuka katika mahakama ya rufaa.
Akitoa mifano mbalimbli ya rushwa zilizo fanyWa na
chama cha mapinduzi CCM na mweka hazina wa chama cha mapinduzi ccm mwigulu
mchemba kutoa rushwa katika sehemu mbalimbali katika jimbo hilo.
Alisema kuwa chama hicho kimejipanga kukabiliana
na rufaa hiyo na kuahidi kuwa rufaa hiyo itakuwa ya aina yake kwani chama hicho
kitafungua kesi nyingine juu ya vigogo wa chama hicho katika uchaguzi huo
mdogo.
Katibu huyo aliwashutum mwekahazi wa chama cha
mapinduzi ccm,kutoa Rushwa,katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi ccm Willson
Mukama kudai kuwa chadema ilileta makondo pamoja na waziri wa Ujenzi Pombe
Magufuli kutoa ahadi za ujenzi wa Daraja la mbuntu pamoja na ahadi ya kugawa
mahindi.
MWIsHO.
No comments:
Post a Comment