Wednesday, September 12, 2012

ASKARI WA JWTZ WAWILI WAKAMATWA WAKIWA WAMEVUNA MISITU PORI LA AKIBA.


NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Askali wawili wa jeshi la ulinzi nchini - JWTZ wa kambi ya MIlambo
mkoani Tabora ni miongoni mwa watu tisa waliokamatwa na kikosi cha
kuzuia ujangiri wakiwa na gaeri la serikali likiwa limeshehena mbao
ndani ya hifadhi ya Uggala mkoani hapa.

Koplo Moshi Jumanne na Mustapha Yusuf walikamatwa siku ja ijumaa saa
mbili usiku wakiwa na gari lenye namba za usajiri 5659 JW 09 aina ya
IVECO  wakiwa na mama mmoja aitwaye Sophia Shigemela  ndani aya pori
la akiba la Kigosi eneo la Ulyankulu wilaya ya Urambo.

Mkurugenzi wa mipango na matumizi ya raslimari za misitu Nchini  (
TFS) Vallentine Msusa amewaambia waandishi wa habari kuwa alipewa
taarifa za hizo za kusikitisha juu ya kukamatwa kwa watumishi hao
waserikali  wakiwa na maliasili hizo bila kuwa na kibali kitendo
ambacho ni cha aibu kwa taifa.

Msusa amesema kuwa gari lililokamatwa bado linahifadhiwa katika kambi
iliyopo ndani ya pori la akiba la Kigosi likiwa limapakia mbao 630
zenye urefu wa futi  8/1 bila kuwa na kibali.

Amebainisha kuwa siku za karibuni watu wengi wamekuwa wakitumia magari
ya serikali kusafirishia maliasili za misitu kwa vile hayakaguliwi
kwenye vizuizi na kupeleka kupakwa matope watumishi wizara hiyo kuwa
ndiyo wahusika wa uvunaji holela.

Mkurugenzi huyo wa TFSamesema kuwa kitndo cha watendaji wa serikali
kutumia magari yao kusafirishia mazao ya maliasili kimesaidia
majangiri nao kuingia ndani ya mapori na kuvuna mali zilizopo kwa
kujiamini.

Msusa ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo hicho na kusema,
"TULITEGEMEA TAASISI ZA UMMA ZINGESAIDIA ULINZI WA MISITU NA RASLIMALI
ZILIZOMO LAKINI KUMBE SIVYO'

Amesema kuwa askali hao na watu wengine waliokamtwa na magari yakiwa
yamebeba mbao hizo wanatarajiwa kufikishwa mahakami ili wajibu tuhuma
zinazowakabili.

Katika hatua nyingine Msusa amesema kwamba kumekuwa na matukio
yasiyofurahisha kwani wiki mbili zilizopita askali wa JWTZ wa kikosi
cha Milambo walimpiga mtumishi mmoja wa idara ya misitu mjini hapa
huku wakimtishia kumuua.

Habari zilizopatikana toka ndani ya kambi kikosi cha kuzuia ujangiri
iliyopo pori la akiba  ya Kigosi  Ulyankuru zimesema kuwa magari ya
JWTZ yamekuwa yakibeba mbao ndani ya pori hilo mara mbili kwa wiki
wakidai kuwa wanaenda kutumia katika ofisi zao.

Zimeongeza kuwa askali hao wawili mara baada ya kukamatwa wakiwa na
mama Sophia huku wameshehema mbao hizo walidai kuwa wao wamekodishwa.

Na baada ya mahojiano walieleza kuwa wao wanatokea huko Biharamulo na
walikuwa wamesafirisha maiti lakini wamekosa mafuta ya kuwarudisha
kwao ndipo wakakubali kukodiwa ili waweze kupata fedha za mafuta ya
kurudia.

Watu wengine waliokamatwa siku hiyo wakiwa na gari lenye namba za
usajiri T 761 BCV aina ya Fusso likiwa na mabo zaidi ya 350 ni Kiwele
William na Sultan Hamda dereva wa fusso hiyo, Richard Samweli , Msina
John, Bashiba Lugaka na Gaspar Kugatwa.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment