PICHA NA HABARI JUMA KAPIPI
Na Mwandishi Wetu
Benki ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa kwa wodi ya akina mama
wajawazito
vyenye thamani ya shilingi milioni 15,640,000 kwa hospitali
ya Amana katika uzinduzi wake wa wiki ya jamii.
Akizungumza katika hafla fupi ya mabidhiano ya vifaa hivyo
yaliyofanyika hospitalini hapo, Mkuu wa kitengo cha masoko na jamii wa
benki ya KCB Christine Manyenye alisema Msaada huo unalenga kupunguza
vifo vya akina mama na watoto.
Manyenye alisema, Benki ya KCB
inatambua umuhimu wa afya ya mama na mtoto na ndiyo maana iliona kuwa ni
jambo zuri kuelekeza msaada huo muhimu kwa kundi hilo Kila mwaka.
"Kwa kawaida
tunaangalia sehemu yenye mahitaji sana msaada na kutoa mchango sehemu
hiyo, Kwa mfano tumegundua kuwa hospitali zetu haswa hizi zinazohudumia
watu wenye kipato cha chini zina matatizo mengi na ndiyo maana leo
tumekuja kutoa mchango hapa Amana,alisema Manyenye
"Ni matumaini yetu kuwa,
vifaa hivi vilivyotolewa na Benki ya KCB vitachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha
utoaji huduma kwa akina mama na watoto na hivyo kujenga taifa lenye
jamii ya watu wenye afya bora," aliongeza.
Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo Dokta Shani Mwaruka
aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasaidia kuboresha huduma kutokana na kupatiwa vifaa hivyo.
"Hali za
hospitali zetu hizi za serikali siyo nzuri sana kutokana na ukosefu wa
vitendea kazi, hakika tunahitaji msaada ili tuweze kutoa huduma bora na
ndiyo maana tunatoa shukrani za pekee kwa benki ya KCB, alisema Dk.Shani
Vifaa
vilivyotolewa ni pamoja na mashine ya joto kwa watoto wachanga
waliozaliwa bila kutimia, vitanga vya kujifungulia 5, vifaa vya
kusaidia wakati wa akina mama wajawazito kujifungua 10, mashuka 116, drums 20 na
Cord clamp 100.
MWANANYAMALA
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, jana ilipokea msaada
wa mashine ya joto kwa watoto waliozaliwa bila kutimia (baby warmer )
yenye thamani ya shilingi 7,850,000 kutoka katika Benki ya KCB Tanzania.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, mkuu wa kitengo cha
masoko wa benki hiyo Christine Manyenye alisema msaada huo umetolewa
baada ya kubaini uwezo mdogo wa hospitali za umma kuhudumia watoto
wanaozaliwa bila kutimia (pre mature)
"Kabla ya kufukia uamuzi wa kutoa msaada huu tulichunguza na kugundua
kuwa huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa bado si
nzuri kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo tuliona ni jambo zuri kuelekeza msaada
wetu kwa kundi hili" alisema Manyeye huku akibainisha kuwa benki ya KCB imekuwa
ikielekeza zaidi misaada yake kwenye makundi yenye mahitaji makubwa na
yenye uchache wa rasilimali za kutatua matatizo za aina mbalimbali.
Kwa upande wake Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo ya Mwananyamala Dokta
Chrispian Kayolai aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa
utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa watoto wanaozaliwa
kabla ya muda wao.
"Tunachangamoto nyingi ambazo tunakutana nazo wakati wa
kutoa huduma na haswa kwa ajili ya vitendea kazi,Msaada huu
tumeupokea leo utasaidia sana kuboresha huduma na tuna kila sababu ya
kuishukuru sana benki ya KCB," alisema Dk Kayolai
Kwa mujibu wa Manyenye, katika
kuadhimisha wiki ya jamii hospitali za KCMC Moshi, Mwembeladu Zanzibar,
Morogoro na Mount Meru ya Arusha itanufaika na misaada itakayogharimu
shilingi milioni 79,040,000/-
No comments:
Post a Comment