NA Lucas
Raphael,Tabora
TYNF
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Tanzania Yourth
new Fashion (TYNF) wilaya ya Sikonge mkoani limepatiwa msaada wa kiasinm cha
shilingi milioni 30 kutoka Asasi ya PETER JOHANES ROGAAR FOUNDATION-(PJRF)kutoka
Uholanzi kwa ajili ya shughuli mbali mbali za maendeleo ya shirika hilo.
Akitoa msaada huo kwa TYNF mwakilishi wa shilika hilo
kutoka uholanzi ,Michael Rogaar alisema kwamba baada ya kutembelea Taasisi hiyo
mwaka 2011 shirika lake liliridhika na uendeshaji wa sghughuli mbalimbali
zinazofanywa na asasi hiyo ya kitanzania iliyopo wilayani sikonge.
Alisema kuwa msaada huo wa fedha kwa ajili ya kufanyia
kazi kwa miradi midogomidogo inayolenga kuleta mabadiliko katika jamii ya watu
wanaishi katika mazingira hatarishi ndani ya wilaya na nje.
Rogaar aliendelea kusema kwambafedha zilizotolewa na
shirika lake ni kwa ajili ya kuchimba visima viwili kwenye eneo la asasi hiyo
,kujenga uzio na kuboresha mazingira ili yawe rafiki kwa watoto wakati wa
kujifunza na kuongeza kuwa mpango wake wa baadaye ni kujenga Maktaba katika
asasi hiyo .
Hata hivyo mwakilishi huyo wa asasi ya PJRF aliweka
jiwe la msingi la ujenzi wa karakana ya ufundi itakayogharimu shilingi milioni
27 mara baada ya kukamilika kwa jingo hilo .
Kukamilika kwa karakana hiyo kutawezesha kutoa mafunzo
kwa vijana mbalimbali katika fani za Useremala,makanika,Ushonaji,na uchomeaji
wa vyuma.
Aidha mkurungezi wa Asasi ya Tanzania Yourth New
Fashion ya wilaya ya sikonge ,Poul Sipemba alilishukuru shirika la PJRF la
Uholanzin kwa msaada wake kwa asasi yake ambayo imekuwa ikifundisha watoto
yatima na wale wanaishi katika mazingiri hatarishi katika fani za ufundi
mbalimbali kwa ajili ya kuwasidia kuondokana na mazingira hayo hatari kwao kwa
kuwajengea uwezo wa kuweza kujitengemea wenyewe mara baada ya watakapomaliza
masomo yao .
Hata hivyo alisema licha ya chuo hicho kutoa mafunzi
ya ufundi lakini puia utoa masomo ya sekondari kwa kufuata mfumo wa masomo ya
elimu ya watu wazima ..
Mwisho.
No comments:
Post a Comment