Naibu waziri
wa uchukuzi Dkt Charles Tizeba ameitaka kampuni ya china ya CCECC EAST AFRICHA
LTD kukamilisha kubalilisha reli kwa mujibu wa mkataba wao unavyosema ili
kuruhusu shirika hilo la kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi .
Waziri huyo
aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika reli ya kati aliyoifanya jana akiwa
pamoja na viongozi waandamizi wa shirika hilo kukangua mradi wa kubadilisha
reli ya kati kutoka yenye uzito mwepesi na kuweka yenye uzito wa kila 40
kwa mita moja kwa ajili ya kuwezesha reli hiyo kuweza kupitika kwa urahisi
tofauti na ilivyosasa .
Mradi huo wa
kubadilisha reli wenye urefu wa kilometa 89 kutoka sheshini ya Kitalaka
hadi eneo la Malongwe utakao gharimu jumla ya fedha za kitanzania shilingi
bilioni 29. kwa kipindi cha mwaka mmoja
Akizungumza na
meneja mradi wa kampuni hiyo ya kichina CCECC WU ZEGANG ,alimwambia kuwa
wahakikishe kuwa muda uliowekwa ndio muda huo huo wanakabidhi mradi huyo na
taratibu zote ziwe zimekwisha kulingana na mkataba wa mwaka mmoja .
“Mkataba wenu
na serikali ya Tanzania kupitia rahco uwe umekamilika kwa muda uleule ambao
mlisaini kwa ajili ya kumilisha kazi iliyopo mbele yenu ambayo imeanza toka
septemba 1 mwaka huu”alisema Dkt Tizeba.
Naibu waziri
huyo alisema kwamba kubadilishwa kwa reli hiyo kutalisaidia shirika la Reli
hapa Nchini litakuwa linafanya kazi kwa ufanisi zaidi wa kuweza kupitisha
mizigo mizito tofauri na sasa .
Aidha alisema
matatizo yaliyopo sasa ya reli nyembamba inasababisha reli kuhama hama na
kupatab ajali za mara kwa mara ikiwe na mzigo mkubwa hayo yote
hayatakuwepo tena bali itabaki kwenye madaraja ambayo nayo yatafanyiwa
matengenzo kuruhusu kupitisha mizigo mizito.
Dkt Tizeba
alisema kwamba mradi huo ni ukamilishaji wa kilometa 197 ambazo zilikuwa
zikifanyiwa marekebisho ya kuweka reli zinazoweza kupitsha mabehewa yenye na
mizigo mizito .
Hata hivyo
alisema kwamba reli yetu sio mbaya sana kiasi kwamba ni mbovu kila eneo na kuna
maeneo mengine yamefanyiwa kazi na mengine pia yanahitaji matengenezo.
Kaimu meneja
mradi huo kutoka RAHCO, Mahizo Mgenzi alisema kukamilisha kwa matengenezo hayo
kutakuwa kumeboresha miundombimu ya shirika la Reli na sehemu inayafanyiwa
ukarabati itaweza kupisha treni kwa kasi zaidi na mizigo yenye uzito mkubwa.
Alisema kwamba
kukamilika kwa reli hiyo usalama wa reli ,mabahewa ya aina yote na yatakuwa
kwenye usalama zaidi tofauti na sasa ambavyo mabehewa yanayumbayumba na
kusababisha abiri kuwa na hofu mara wanaposafiri.
Mwisho
No comments:
Post a Comment