Saturday, September 8, 2012

NA Lucas Raphael,Tabora

[TYNF]
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Tanzania Yourth new Fashioni (TYNF) wilaya ya Sikonge mkoani limepatiwa msaada wa kiasinm cha shilingi milioni 30 kutoka Asasi ya PETER JOHANES ROGAAR FOUNDATION-(PJRF)kutoka Uholanzi kwa ajili ya shughuli mbali mbali za maendeleo ya shirika hilo.

Akitoa msaada huo kwa TYNF mwakilishi wa shilika hilo kutoka uholanzi ,Michael Rogaar alisema kwamba baada ya kutembelea Taasisi hiyo mwaka 2011 shirika lake liliridhika na uendeshaji wa sghughuli mbalimbali zinazofanywa na asasi hiyo ya kitanzania iliyopo wilayani sikonge.

Alisema kuwa msaada huo wa fedha kwa ajili ya kufanyia kazi kwa miradi midogomidogo inayolenga kuleta mabadiliko katika jamii ya watu wanaishi katika mazingira hatarishi ndani ya  wilaya na nje.

Rogaar aliendelea kusema kwambafedha zilizotolewa na shirika lake ni kwa ajili ya kuchimba visima viwili kwenye eneo la asasi hiyo ,kujenga uzio na kuboresha mazingira ili yawe rafiki kwa watoto wakati wa kujifunza na kuongeza kuwa mpango wake wa baadaye ni kujenga Maktaba katika asasi hiyo .

Hata hivyo mwakilishi huyo wa asasi ya PJRF aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa karakana ya ufundi itakayogharimu shilingi milioni 27 mara baada ya kukamilika kwa jingo hilo .

Kukamilika kwa karakana hiyo kutawezesha kutoa mafunzo kwa vijana mbalimbali katika fani za Useremala,makanika,Ushonaji,na uchomeaji wa vyuma.

Aidha mkurungezi wa Asasi ya Tanzania Yourth New Fashion ya wilaya ya sikonge ,Poul Sipemba alilishukuru shirika la PJRF la Uholanzin kwa msaada wake kwa asasi yake ambayo imekuwa ikifundisha watoto yatima na wale wanaishi katika mazingiri hatarishi katika fani za ufundi mbalimbali kwa ajili ya kuwasidia kuondokana na mazingira hayo hatari kwao kwa kuwajengea uwezo wa kuweza kujitengemea wenyewe mara baada ya watakapomaliza masomo yao .

Hata hivyo alisema licha ya chuo hicho kutoa mafunzi ya ufundi lakini puia utoa masomo ya sekondari kwa kufuata mfumo wa masomo ya elimu ya watu wazima ..

Mwisho.



No comments:

Post a Comment