Na
Lucas Raphael,Tabora
Wanafunzi
wapatao 4000 katika wilayani Igunga mkoani Tabora wameshindwa
kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba kutokana na sababu mbalimbali
ikiwepo na vifo na utoro unaochangiwa na
wazazi wa watoto kuwatka kuchanga mifugo .
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu
katika Mahafali ya pili ya Darasa la saba ya shule ya msingi ya sent Leo
iliyopo wilayani Igunga.
Kingu alisema kuwa wanafunzi hao walianza wakiwa darasa la kwanza
zaidi ya 12800 mpaka kuhitimu darasa la saba 8000 ambapo wanafunzi ambao
hawakufanya mtihani wa kuhitimu darasa hilo walikuwa 4000.
Alisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwafuatilia watoto wao pindi
wanapo anza shule mpaka kuhitimu darasa husika ili kupambana na adui uchinga.
Alisema idadi hiyo ya wanafunzi 4000 kutofanya mtihani niidadi
kubwa hivyo wazazi wanapaswa kubadili mara mmoja ili kuhakikisha kila mtoto
anapata Elimu hiyo ya msingi.
Alisema kuwa mzazi atakaye bainika kuto mpeleka mtoto shule ama
kuchangia mtoto kuto enda shule hatua kali zitachukuliwa ikiwa na kupelekwa
mahakamani kwa mzazi husika atakaye bainika na tuhuma hizo.
’’wakazi wa Igunga badilikeni mjue uchungu wa Elimu kwa watoto
wenu hivyo basi niabu kati ya watoto 12800 watoto 4000 hawajafanya mtihani hii
haipendezi razima mzazi wajibishwe wazazi hawa ni wazembe,atakaye bainika hatua
kari zitachukuliwa ikiwa na kufishwa mahakamani’’alisema Kingu.
Aliwaagiza viongozi wa vijiji,kata pamoja na viongozi wa dini
kutoa hamasa kwa wananchi kuhakikisha watoto wanaandikishwa shule pamoja na
kuwafuatilia watoto hao mpaka hatua ya mwisho ya mitihani yao.
Sababu mbalimbali zilizosababisha mpaka watoto hao kutofanya
mtihani huo ni pamoja na utoro wa kupindukia,kuolewa kwa wan afunzi wa kike,
shuguli za kiufugaji pamoja na shuguli za kilimo.
Meneja wa shule hiyo Coaster Olomi alisema kuwa wazazi wanapaswa
kutambua umuhimu wa Elimu na kuwakazania watoto hao kupenda shule nakuongeza
kuwa jamii za wafugaji zi Elimishwe zaidi ikiwa na kuachana na imani potofu
ambazo bado mpaka sasa zinaendelea.
MWIsHO.
No comments:
Post a Comment