Na
Lucas Raphael,Tabora
Mdahalo
Katiba.
Wananchi wa kata ya Igalula Wilaya ya Uyui
mkoaniTabora wamesema kwamba katiba mpya ya Tanzania iwe na kipengele
kinachowakataza viongozi kwenda kutibiwa njue ya nchi na baadala yake watibile
humu humu nchi.
Lengo la viongozi hauo kutibiwa humu nchi ni
kuhakikisha huduma nzuri za matibabu zinatolewa kwa wananchi wote na sio kwa
kundi moja la watu wachache .
Hayo waliyaeleza kwenye mdahalo wa kuwahamasisha wananchi kujitokeza
kutoa mawazo na michango yao katika mchakato wa kuunda katiba mpya pindi tume
ya kukusanya maoni itakapopita kijijini hapo kwa ajili ya kazi hiyo.
Akizungumza
katika kijiji cha Igulalu kaya ya Igalula mmoja wa washiriki wa mdahalo huo
,Maneno Keye alisema huduma za Afya sio nzuri kwa sasa kwani wananchi wanapata
dawa ambazo muda wake umeshakkwisha .
Alisema
kwamba kiti cha dawa kinacholetwa katika zahanati hakuna dawa bora ambazo
zinazoweza kuwatib wananchi kwa kipindi hicho ,ndio hata Hospital za Rufaa pia
hakuna huduma bora zinaweza kuwafanya viongozi kutibiwa huko .
Keye
aliendelea kusema kwamba hali hiyo ya huduma mbovu za hospital zetu ndio maana
viongozi mbalimbalui wanakimbilia kutibiwa nje ya nchi na kuziacha hospital
zetu hazina madawa ya kutofa hata vifaa vya kuwez kuwatibu watanzania.
“katibu
ikatanze viongozi kwenda kutibiwa huko nje kwa kufanya hivyo serikali
itaboresha miundombinu ya hospital zetu kwani matibabu huyo yanawahusu
watanzania wote “alisema keye.
Hata
hivyo alisema kwamba iwapo zahanati hospital na zile za Rufaa zitakuwa na vifaa
vya kutosha na waatalaam wazuri katika fani hiyo ya tiba hakika hakuna kiongozi
ambaye hatakwenda kutibiwa huko nje ya nchi.
Aidha
madam Hadija Shoo alisema kwamba katiba mpya ijali usawa wa kijinsia
kwani wanawake wengi wa vijiji wamekuwa kama ni watumwa kwa waume zao kwani
waliowengi wanaolewa kama wafanyakzi wa ndani na sio wake kwa upendo hakuna.
Awali
mwezeshaji wa mdahalo huo ,Christopher Nyamwanji aliwataka wananchi wa Igalula
kushiriki kikamilifu kutoa mawazo na michango yao katika mchakato wa uundwaji
wa katiba mpya wakati tume ya kukusanya maoni kwa wananchi itakapopita kwa
ajili kufanya kazi hiyo.
Alisema
kwamba iwapo kila mwananchi atatoa maoni kikamilifu na kupendekeza kuwa katiba
ijayo iwe na muundo upi, hakika matukio kama. ambayo yamekuwa
yakijitokeza hivi sasa hapa nchini
Nae
Mwenyekiti Shirika la Mtandao wa Maendeleo ya wananchi wilaya ya Uyui (UCODEN)
ambao ndio waandaaji wa Mdahalo huo, Ally Magoha alisema kuwa katiba ni
wananchi, mafanikio na machungu ya watanzania, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja
kutoa mchango na mawazo yake katika mchakato wa kuunda katiba mpya ili kuweza
kupata katiba ambayo itakidhi matakwa ya umma wa watanzania.
UCODEN
ni Shirika lisilo la kiserikali ambalo limekuwa likijishughulisha na kazi za
maendeleo wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambapo kwa mujibu wa Magoha wanatarajia
kufanya midahalo kama hiyo katika vijiji vya Bukumbi, Ilolangulu na Kizengi, na
kwamba lengo kuu la kufanyika kwa midahalo hiyo ni kutoa uamsho kwa wananchi
kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la katiba.
Mdahalo
huo ulioendeshwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la UCODEN na kufadhili na
foundation For Civil Society.
Mwisho
No comments:
Post a Comment