Tuesday, June 17, 2014

NAPE ATINGISHA JIMBONI MNYIKA


*ASEMA CHADEMA SASA INAKUMBATIA UKAWA KUJARIBU KUPOZA MIGOGORO YA NDANI INAYOKIMALIZA.

*ATABIRI MAISHA YA  CHADEMA KUKOMA BAADA YA AJENDA YA KATIBA  MPYA KUMALIZIKA

*ASEMA, 'PANGO' LA MYIKA UBUNGO LINAISHIA 2015,  AKAE MKAO WA KUONDOKA
Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
 
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,  leo ametoboa siri kwamba, viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wamelazimika kukumbatia kinachoitwa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA), ili kujaribu kupoza migogoro iliyopo ndani ya chama hicho ambayo inakiua.

Amesema, siyo kweli kwamba Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Woilbrod Silaa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe wanahangaika na muungano huo unaoitwa wa kutafuta Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kusaidia wananchi bali ni kujaribu kupoza makali, baada ya kuona kwamba chama chao kimo katika mgogoro mkubwa wa ndani ambao si mda mrefu utaua.

"Chadema wapo katika mgogoro mkubwa kutokana na baadhi ya viongozi wake hasa wa ngazi za juu kukiendesha chama katika misingi ya ubaguzi.. na ndiyo sababu leo au hata kesho, Mbowe hawezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu la chama hicho, na akijaribu kufanya hivyo anatimuliwa", alisema Nape.

Nape pia hakumuweka kiporo Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mwinyika, badala yake alimpasha kwenye mkutano huo kwamba, baada ya wananchi wa jimbo hilo kudanganyika na kumpa ubunge, sasa akae mkao wa kuondoka baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika 2014.

"Mnyika na Chadema yake tunawambia pango lao hapa jimbo la Ubungo  linamalizika rasmi mwaka 2014 na hatuma mpango wa kumuongezea, kilichobaki sasa ajiandae tu kuondoka taratibu", alisema Nape.

Alisema, Mnyika kama walivyo wabunge katika maeneo ambako wananchi walijaribu kuwachagua wapinzani, anachofanya yeye na Chama chake cha Chadema ni kupambana na kujenga misingi ya chama chao kuendelea kuwa kuishi na kamwe hawashughulikii matatizo ya wananchi.

"Na hili niliwaambia miaka mingi iliyopita, nilisema hapa ubungo kwamba mkimchagua mpinzani kazi yake itakuwa kutafuta njia za kuimarisha chama chake, na kamwe hataweza kujihusisha na masuala ya maendeleo yenu", alidai Nape na kuongeza;-

"Mnyika kama kweli una lengo la kuwatumikia wananchi wa Ubungo, umefika wakati wa kuacha sasa na mambo ya kudai kila mara hoja binafsi bungeni, sasa udai na hoja za wananchi, maana ukiendelea kudai hoja binafsi zaa wananchi utadai lini?"

Alisema, ni kutokana na wapinzani akiwemo Mnyika na chama chake cha Chadema, kutokwa mapovu midomoni kila kona ya nchi wakihangaika na Katiba mpya, tena wanachozungumzia zaidi serikalikali tatu na kusingizia kwamba ndiyo mahitaji ya wananchi huku wakijua wazi kwamba wanachohitaji wananchi kama wa Ubungo ni maji, elimu na afya na siyo idadi ya serikali.
 
Nape alisema hivi sasa wananchi wameshastukia vyama vya upinzani kwamba vipo kwa maslahi ya wachache ni si ya wananchi kama vinavyovyojinadi.

Alisema, miongoni mwa dalili za wananchi kuvistukia vyama cya upinzani, ni hali ilivyojitokeza wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alkizofanya akiambatana na Nape mwenyewe mikoani.

Nape alisema, katika ziara hizo hadi sasa wanachama  12, 430 walijiunga CCM huku karibu nusu yao wakiwa wametoka katika vyama vya upinzani vikiwemo Chadema na CUF.

Katika mkutano huo ulioandaliliwa na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Nape alipokea wanachama wapya 480, wengi wao wakiwa wamehamia CCM kutoka katika vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti.


 Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Ramadham Madabiba akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape  Nnauye alipowasili katika Kata ya Kimara kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua uhai wa Chama katika kata hiyo, leo Juni 15, 2014.
Vijana wa Chipukizi wa CCM, wakimvisha skafu Nape alipowasili katika kata hiyo kuanza ziara ya siku moja leo,Juni 15, 2014. Kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge

Nape akizindua Shina la wakereketwa wacheza bao, tawi la Jumuia ya Wazazi la 770, Kimara, wakati wa ziara hiyo.
Nape akicheza bao na Augustine Bathoromew (66), baada ya kuzindua shina la wacheza bao la Jumuia ya Wazazi tawi la 770 Kimara akiwa katika ziara hiyo. Wanaoshuhudia ni Madenge (kulia) na katikati ni Madabiba na Juma Simba ambaye ni Katibu Mwenezi mkoa wa Dar es Salaam.
Nape akisalimia wananchi baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA, kuhutubia mkutano wa hadhara mwishoni mwa ziara yake ya siku moja katika Kata ya Kimara.
Wananchi  wakimshangilia Nape baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA
Wananchi wakiselebuka wakati Nape akicharaza gita na bendi ya Vijana Jazz, baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA,wakati wa ziara hiyo.
Madabida akimkaribisha Nape kuhutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia kwenye mkutano huo, mwishoni mwa ziara yake katika kata ya Kimara
Nape akimkabidhi kadi ya CCM, Domina Emmanuel, wakati wa mkutano wa hadhara Kimara TRA. Jumla ya wanachama wapya 480 wakiwemo waliohamia CCM wakitoka vyama vya Chadema na CUF walipewa kadi baada ya kujiunga na CCM
Nape akiongoza viongozi wengine kuwaunga mkono wanachama wapya kula kiapo baada ya kuwakabidhi kadi za CCM kwenye mkutano huo.
Wanachama waliopewa kadi kwenye mkutano huo, wakila kiapo.
Nape akiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara Uwanja wa Kimara TRA. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

KANISA LA ‘TAG’ LATENGA MIL.270 KWA AJILI YA MISAADA YA KIJAMII


 


Na Allan Ntana, Tabora

IKIWA ni miaka 75 sasa tangu kuanzishwa kwa kanisa la Tanzania
Assemblies of God hapa nchini, jumla ya sh mil.270 zimetengwa kwa
ajili ya kutoa misaada mbalimbali ya kijamii katika sherehe za
maadhimisho ya Jubilee ya kanisa hilo hapa nchini.

Hayo yalibainishwa jana na Askofu Mkuu wa kanisa hilo hapa nchini Dr
Barnabas Mtokambali katika ibada maalumu iliyofanyika katika uwanja wa
ofisi mpya za jimbo mjini Tabora.

Alisema katika kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo
hapa nchini kanisa limeandaa kiasi cha sh milioni 270 kwa ajili ya
kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa makundi ya watu mbalimbali
wenye uhitaji.

Dr Mtokambali alifafanua kuwa watatoa vyandarua, damu na vitu
mbalimbali kwa jamii ya watanzania wenye uhitaji pasipo kujali dini ya
mtu, rangi wala kabila, lengo likiwa ni kumshukuru Mungu kwa
kuliwezesha kanisa hilo kutimiza miaka 75.

Alisema sherehe za maadhimisho ya Jubilee ya kanisa hilo
lililoanzishwa mwaka 1932 hapa nchini na sasa likiwa na waumini zaidi
ya milioni 5 tayari zilishaanza katika makanisa ya TAG hapa nchini na
zinaendelea katika majimbo yote 32 ya kanisa hilo.

Kilele cha maadhimisho hayo ya kihistoria  yatakayohudhuriwa na maelfu
ya watu wakiwemo maaskofu , wachungaji, viongozi wa taasisi,
mashirika, dini mbalimbali, viongozi wa serikali na wananchi kitakuwa
tarehe 13Julai 2014 jijini Mbeya na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema.

Aidha Mtokambali alipongeza jitihada thabiti za kimaendeleo
zinazofanywa na uongozi wa TAG jimbo la Tabora chini ya uongozi wa
Askofu Paul Meivukie kwa kuwa na mikakati endelevu ya kuimarisha kazi
ya Mungu jimboni humo sambamba na uanzishwaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.

‘Askofu Meivukie hongera sana kwa moyo wako wa kujituma, naomba
mwendelee kushirikiana hivi hivi ili mikakati yenu ya kuanzisha miradi
ya maendeleo kama mlivyosema ifanikiwe, naahidi kuwapeni ushirikiano
kama kiongozi wenu’, alisema.

Akizungumzia mchakato wa katiba mpya unaoendelea hapa nchini, Dr
Mtokambali alishauri kipengele cha muundo wa serikali 1,2 au 3 ambacho
kinaonekana kuwagawa wabunge wa bunge hilo maalumu kiletwe kwa
wananchi ili wao ndio waamue, kwani wananchi wanao uwezo wa kuamua kwa
busara badala ya kuendeleza malumbano.

‘Kama suala hilo limeshindikana kuamuliwa, tunaomba bunge liturudishie
tutoe uamuzi sisi wenyewe, tunahitaji katiba itakayotuletea maendeleo
katika ngazi zote vijijini na mijini na itakayodumisha uhuru na amani
katika nchi na katika kuabudu’, aliongeza.

Pia aliwataka wachungaji wote wa TAG hapa nchini kuhamasisha waumini
wao kujiunga na vyama vya siasa sambamba na kugombea nafasi mbalimbali
za uongozi huku akionya wachungaji hao kutokuwa  wanachama wa chama
chochote cha siasa.

Awali askofu wa jimbo la Tabora Paul Meivukie alimweleza Askofu Mkuu
Mtokambali kuwa wameazimia kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii
ikiwemo kuanzisha vituo 2 vya kuhudumia watoto yatima katika wilaya za
Sikonge na Uyui,  tayari vimeanza kazi.

Mradi mwingine ni mradi wa kufyatua matofali ya kuuza (interlock)
mashine yenye uwezo wa kufyatua tofali 1000 kwa siku moja tayari
imenunuliwa na ujenzi wa kituo cha jimbo la Tabora nao tayari umeanza.

Miradi inayotarajiwa kuanzishwa ni pamoja na ujenzi wa Chuo Kikuu cha
Wachungaji, ujenzi wa shule 2 za sekondari, uchimbaji visima 3 vya
maji na ujenzi wa kituo cha afya katika eneo la Ipuli katika manispaa
ya Tabora.

Sunday, June 15, 2014

BAADA YA MUFTI SHAABAN SIMBA KUONDOKA MGOGORO MSIKITI MKUU WA IJUMAA TABORA SASA WAPAMBA MOTO


Msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni mjini Tabora.
HALI MBAYA YA VURUGU YANUKIA MSIKITI MKUU WA GONGONI
Katika hali ambayo haikutarajiwa kutokea msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni mjini Tabora,hivi sasa kumekuwa na hali ya kukaniana baina ya Waislamu wa pande mbili waliogawanyika katika msikiti huo mkuu.

Waislamu wa mjini Tabora wakiwemo waumini wa msikiti huo wamegawanyika kutokana na kile kinachodaiwa kuwa mtafaruku wa baadhi ya  viongozi wa dini ya kiislam ambao walimwandikia na kumlalamikia Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Simba kuhusu ubadhirifu unaofanywa na viongozi wa Msikiti huo wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Tabora Shaaban Salum ambaye amesimamishwa wadhifa wake kutokana na malalamiko hayo.

Uamuzi wa Mufti wa Tanzania Shaaban Simba wa kumvua madaraka Sheikh wa mkoa wa Tabora umewachukiza baadhi ya waumini wa dini ya kiislam mkoani Tabora na kuamini  kuwa mbali ya kumdhalilisha Sheikh Shaaban Salum pia umedhalilisha uislamu kwakile walichoeleza kuwa Shaaban Salum ni kiongozi wa kwanza kuonesha nia ya kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika msikiti huo kwakuwa tangu aingie madarakani amekuwa akifanya miradi mbalimbali ya maendeleo kutokana na michango midogo ya fedha zinazochangwa na Waislam katika msikiti huo.

Mufti ambaye anaaminika ndio kiongozi mkubwa wa dini ya kiislamu nchini alimteua Sheikh Ibrahim Mavumbi kushika wadhifa wa Sheikh wa mkoa wa Tabora jambo ambalo limendelea kupingwa na wengi licha ya kuwa Mufti Shaaban Simba alijaribu kufika mkoani Tabora kwa nia ya kutaka kutoa ufafanuzi kuhusu uamuzi aliouchukia ingawa ufafanuzi huo aliutoa kwa njia ya Redio za Kijamii jambo ambalo halikuwafurahisha baadhi ya Waumini wa dini ya kiislam. 

Askari wa Jeshi la Polisi wamelazimika kuendelea kuzunguukia eneo la Msikiti huo nyakati za Ibada kulinda usalama  kwakile kilichoelezwa kuwa baadhi ya waumini wa dini ya kiislam hawamtaki Sheikh mteule Ibrahimu Mavumbi aendeshe ibada katika msikiti huo mkuu wa Ijumaa ambao wanadai ni mali ya Waislam kuliko inavyoaminiwa na upande wa pili wa mgogoro huo ambao umekuwa ukidai ni mali ya Baraza kuu la Waislamu nchini Bakwata.

Hata hivyo wachunguzi wa mambo wameshauri kuwa ni vema pande hizo mbili za Waumini wa dini ya kiislam wakae katika meza ya mazungumzo badala ya kuwepo kwa mvutano huo wa ushabiki unaoelekea kupoteza amani katika msikiti huo.

WADAU WAPITISHA MAAZIMIO 13 KUBORESHA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA TABORA


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui Bw.Said Ntahondi akizungumza katika ufungaji wa Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tabora ambapo alisisitiza wadau hao kutekeleza kwa vitendo maazimio 13 yaliyofikiwa katika mkutano huo yakiwa na lengo la kuboresha huduma za mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  NHIF pamoja na kuhamasisha jamii ijiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ambapo utaratibu wa Tiba kwa Kadi utasaidia jamii kupata huduma za matibabu kwa kila Kaya.



Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  katika mkutano Tabora mjini

UTUMIKISHWAJI WATOTO KWENYE MASHAMBA YA TUMBAKU WILAYANI SIKONGE NI ASILIMIA 48.4


Baadhi ya Watoto wa Shule ya Msingi Udogo wilayani Sikonge wakifanya maandamano wakati wa Sherehe ya Siku ya kupinga utumikishwaji watoto iliyofanyika wilayani humo iliyoandaliwa na Mradi wa Prosper ambao unashughulikia kuondoa ajira mbaya kwa Watoto.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge Bw.Robert Kamoga akizungumza katika sherehe za Siku ya kupinga utumikishwaji watoto ambapo aliwataka wazazi na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto na badala yake kuwapa muda mwingi na kuwawezesha kielimu.
Mkurugenzi wa Mradi wa Prosper Bw.Bahati Nzunda akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha muda wa miaka minne pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika kumkomboa mtoto na ajira mbaya hasa katika mashamba ya tumbaku.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge Bw.Robert Kamoga akisalimiana na wanamichezo wa mpira wa pete wa Shule ya msingi Udongo.
Wachezaji wa ngoma ya asili  RADU wakionesha vitu vyao wakati wa Sherehe hizo za Siku ya kupinga ajira mbaya kwa watoto.

CHAMA CHA WALIMU WAUOMBA MFUKO WA BIMA YA AFYA KUSAIDIA HUDUMA YA MENO YA BANDIA KWA WALIMU


Katibu wa Chama Cha Walimu CWT mkoani Tabora Bi.Romana Aloyce Mnyoni akichangia katika majadiliano ya Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi ambapo alichangia kwa kuuomba mfuko huo kusaidia kulipa huduma za matibabu ya meno kwa Mwalimu atakayepata tatizo la kung'oka meno ili kumsaidia aweze kutamka maneno kwa ufasaha mbele ya wanafunzi wakati wa kufundisha.
Bw.Andrew Karyome Mwenyekiti wa Bodi ya Afya wilaya ya Uyui akichangia mjadala katika mkutano huo wa wadau wa Bima ya Afya NHIF mkoani Tabora.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NHIF Bi.Lyidia Choma akijibu maswali ya wadau wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tabora wakati wa mkutano huo.
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tabora



WLF YAOKOA VIFO VYA WAJAWAZITO UKANDA WA ZIWA KIGOMA




IMEELEZWA kuwa,vifo vya kina mama wanaojifungua katika ukanda wa ziwa Tanganyika  Mkoa wa Kigoma vimepungua kutokana na uboreshaji wa huduma ya upasuaji wa dharura katika kituo cha afya cha Buhingu,ambacho awali kilikuwa kiwanda cha vifo hivyo.
 
Akifafanua hilo mbele ya wandishi wa habari kigoma Ujiji  Mtaalamu Magonjwa ya kinamama Dr.Calist Nzambuhakwa alisema awali wanawake wajawazito walikuwa wakihofu kubeba mimba, kutokana na kuzorota kwa huduma hiyo ambapo  kati ya wajawazito 578 kati ya vizazi hai 100,000 walikuwa wakipoteza maisha wakati wa kujifungua 2009-2013.
 
“kumsafirisha mama mjamzito kwenye boti la mbao la abiria ni hatari, na kutoka kituo cha buhingu hadi hospitali  ya rufaa Maweni kigoma mjini masaa 18 ,kifo kwa wenye uzazi pingamizi , wanaovuja damu na  kifafa cha uzazi hali ilikuwa tete,ndo mana kituo kile kiliitwa kiwanda cha kifo kwa wajawazito” alibainisha Dr.Nzimbahukwa.
 
Alisema Mradi wa Afya ya Uzazi wa shirika la World  Lung  Foundation wamekidhi kuondoa idadi ya vifo kwa wahanga hao, kutoka vifo 12 kwa mwaka 2012 hadi  vifo 2 kwa mwaka 2013  kati ya vizazi hai  1000 .
 
Kwa  upande wa wawakilishi wa Mradi wa World Lung Foundation Victoria Marijani na Dr.Ngukie Mwakatundu kwa nyakati tofauti walisema mradi wao umelenga wilaya  ya Kigoma ,Kasulu,Kakonko  kwa kutoa vifaa tiba na mafunzo elekezi kwa wahudumu katika  vituo mtambukwa tisa kikiwemo kituo cha Buhingu.
 
Walisema  huduma yao imeokoa  vifo vya uzazi pingamizi  171 kwa  wanawake waliojifungua kwa njia ya kisu mkoani hapa na kuahidi kutumia tathimini zao  kujenga majengo bora ya mapumziko ya kinamama wajamzito  kutoka vijiji vilivyopo mbali na vituo vya afya,kwa lengo la kuokoa maisha ya mama na mtoto  Huku wakiitaka serikali ichangie katika hilo.
 
Naye Mganga Mkuu huo  alisema 80% ya damu salama inatumika kwa wakina mama na watoto,ambapo changamoto kubwa ya vifo hivyo ni kuvuja damu kwa mlengwa  wakati wa kujifungua ambapo vifo 68 katika vizazi hai 100,000 na kudai kuwa, hali hiyo itakwisha endapo jamii itaendelea na hulka ya kutoa damu kwa hiari .
 
Alisema lengo la serikali na wadau wa afya ni kuboresha huduma za wahanga hao,ambao ni chachu ya maendeleo ya nchi ,Huku akiwaonya wahudumu wanaouza damu kwa wahanga hao na wananchi kwa ujumla,ambapo kisheria ni kosa kuuza damu.
 
Aidha aliwataka wandishi wa habari wajikite kutoa elimu ya umuhimu wa kutoa damu kwa hiari ,ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau hao wanajenga kituo cha kukusanyia damu salama mkoani hapo, kutokana na mwitikio wa umma husika kuchangia asilimia 114 ya damu  salama .