Saturday, February 14, 2015

TABORA WAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA





Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akizindua Mpango mkakati wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga,uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora ambao umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.

Baada ya kuzinduliwa mpango mkakati huo,wakuu wa wilaya za mkoa wa Tabora walipatiwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji,Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mpango mkakati huo mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mpango mkakati huo unaolenga kuimarisha afya za akinamama wajawazito na watoto wachanga na kupunguza vifo.
Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewji akipokea mpango mkakati huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tabora kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila.
Mganga mkuu mkoa wa Tabora Dr.Gunini Kamba akitoa maelezo mafupi kuhusu changamoto za huduma ya afya zinazoukabili mkoa wa Tabora na namna ambavyo mpango mkakati huo utakavyosaidia kuboresha huduma za afya kwa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito  na watoto wachanga.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akifungua mkutano wa uzinduzi wa mpango mkakati huo wa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga.
Baadhi ya wadau wa Afya kutoka sekta mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kupunguza vifo vya watoto wachanga na kinamama wajawazito.


 
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila ameonya vikali waganga wakuu wa wilaya na waratibu  wa huduma ya Afya ya mama na mtoto wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo hali inayosababisha kuendelea kuongezeka kwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga mkoani humo.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo hilo katika mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto uliofanyika jana katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora
uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya kutoka wilaya zote za mkoa huo, taasisi, mashirika na waandishi wa habari.

Alisema takwimu za idadi ya akinamama wajawazito na watoto wanaofariki kwa kukosa huduma au kutohudumiwa kwa wakati inazidi kuongezeka mkoani Tabora na vifo vingine vinavyotokea hata wataalamu
wa afya hawana taarifa, jambo hili sio zuri, lingeweza kuthibitiwa na watoa huduma katika vituo vya afya.

Alisema hakuna sababu ya mama mjamzito kupoteza maisha anapojifungua au mtoto wake kufariki
 kisa amekosa huduma wakati uwezekano wa kujifungua salama upo, rasilimali chache zilizopo zinaweza kutumika kuokoa maisha ya mama na mtoto wake kama watoa huduma watafanya kazi yao ipasavyo.

‘Kuanzia leo waganga wakuu wa wilaya (DMO’s) ni lazima mtoe taarifa za kifo chochote cha mama
mjamzito kitakachotokea katika kituo chako na utoe sababu kwa nini kimetokea ili mhusika aliyezembea achukuliwe hatua mara moja’, alisema.

Mwananzila aliwapongeza madaktari wote wanaotoa huduma za uzazi katika mradi wa Millenium ulioko
 katika vijiji 16 mkoani humo ambapo taarifa za utendaji zinaonyesha kwamba katika kipindi cha mwakamzima hakuna kifo hata kimoja cha mama mjamzito kilichotokea katika vijiji hivyo.

‘Nawapongeza madakatri na watoa huduma wote walioko katika mradi huu, mmekuwa mfano wa kuigwa,wataalamu wa afya katika kila halmashauri acheni kufanya kazi kwa mazoea, tumieni rasilimali zilizopo ipasavyo, alionya Mwananzila .
 
Mkuu wa mkoa aliwataka wakurunguzi , wakuu wa wilaya , waganga wa wilaya , waratibu wa afya ya uzazi,  makatibu Tawala wa wilaya na ,madiwani, watendaji, madaktari na wauguzi wote kusimamia zoezi hiloipasavyo  katika maeneo yao ili kuepusha vifo vyote vitokanavyo na uzazi.

Aidha aliagiza halmashauri zote kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea wataalamu wapya wa afya na
kada nyinginezo wanaopelekwa katika halmashauri hizo ili wafurahie mazingira ya kazi na waweze kuwa msaada mkubwa katika maeneo hayo.

Kuondoka kwa wataalamu wengi katika halmashauri nyingi kunachangiwa na halmashauri zenyewe kutoandaa
mazingira mazuri ya kuwapokea wataalamu wapya wanaoletwa na serikali.

Akitoa neno la shukrani Mratibu wa Huduma ya Uzazi kwa mama na mtoto Kanda ya Magharibi .
Martha Mlimba aliwataka waganga wakuu, waratibu wa afya na watoa huduma ya uzazi kwa mama na mtoto katika kila halmashauri kuzingatia agizo la RC katika utendaji kazi wao ili kupunguza vifo hivyo.

 
mwisho



Friday, February 6, 2015

MKUTANO MKUU WA SABA WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA(TAWJA) WAFANYIKA JIJINI DAR


 
 Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika mkutano huo.
 Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.
Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.

Dotto Mwaibale
JAJI Mkuu Mohamed Chande, amewataka wanawake nchini kutoa taarifa katika ngazi husika pindi  wanapoombwa rushwa ya ngono ili sheria ifuate mkondo wake.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), alisema kunaidadi kubwa ya wanawake ndani ya jamii wanaoombwa rushwa ya ngono lakini wamekuwa wahoga kutoa taarifa.

"Katika rushwa ya ngono lazima sheria mahususi zichukuliwe,hivyo tunawasihi wanawake baada ya kufanyiwa matukio hayo wafikishe malalamiko mahakamani au sehemu husika na sheria itafuatwa," alisema Jaji Chande.

Kadhalika, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya majaji wanawake ili kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya mahakama katika ngazi zote.

Mwenyekiti wa TAWJA, Engera Kileo, alifafanua katika kesi za rushwa ya ngono mahakama kupitia kifungu cha 25,muhusika atakayebainika kujihusisha na kitendo hicho atatozwa faini au adhabu ya kifungo cha miaka 30.

"Mahakama imeweka adhabu hiyo kutokana na ongezeko la matukio  kufanyika ndani ya jamii na wanawake kujengewa woga wa kutoa taarifa kwa wakati, hivyo tunachokifanya kuangalia namna ya kuongeza adhabu kwasababu ngono imetawala katika sekta mbalimbali," alisema Kileo.

Lakini kwa sasa  chama hicho kinatoa elimu juu ya rushwa ya ngono katika jamii na matumizi mabaya ya ngono zembe ili kuwalinda na magonjwa ya kuambukizwa kama Maambukizi ya Ukimwi(VVu), na yale ya zinaa. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

ASKARI POLISI ALIYEULIWA KIKATILI MKOANI DODOMA AAGWA LEO, MUUAJI NAYE AULIWA NA WANANCHI

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu akiongoza jana waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI aliyeuwawa huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI SIRIL MALYA.
Wasifu wa marehemu ukisomwa 
Maombolezo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa

Na Sylvester Onesmo wa  Jeshi la Polisi Dodoma. 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kama Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa jana tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi Askari huyo.

Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua Askari. 

 Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. 
 Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua. 
 Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi. 
Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

WAZIRI WA UJENZI AKAGUA BARABARA MKOANI KATAVI


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya mara baada ya kukagua barabara za mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Col.Ngemela Eslom Lubinga akisoma taarifa ya mafanikio ya Serikali ya wilaya hiyo  kwa Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Sehemu ya barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75- ambayo ujenzi wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 60.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiimba pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Wilayani Nkasi mara baada ya kuwasalimia alipokuwa njiani kukagua mradi wa barabara unaopita  karibu na shule hiyo.
Sehemu ya barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga km 112 ambayo ujenzi wake unaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Kibaoni kuhusu kuwasimamia makandarasi wanaojenga barabara za Kanazi-Kizi-Kibaoni kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wakazi wa Kibaoni Wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa na Mama mzazi wa  Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi. Waziri wa Ujenzi alipita kumsalimia mara baada ya kuwahutubia wakazi wa Kibaoni kuhusu masuala mbalimbali ya barabara na nyumba za Serikali.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Katavi kuhusu miradi mikubwa ya barabara katika mkoa huo.
Waziri wa Ujenzi akiagana na wananchi wa Katavi mara baada ya kuwahutubia.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

Thursday, February 5, 2015

DKT. NCHIMBI ASEMA CCM HAINA TATIZO LA KIMUUNDO WALA MFUMO


 

nchimbi 3



nchimbi 4




nchimbi 2



nchimbi 1

CCM TABORA YAWATUNUKU VYETI MAKADA WAKE WALIOKISAIDIA CHAMA HICHO KUPATA USHINDI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akimkabidhi cheti mmoja kati ya makada wa chama hicho Bw.Emmanuel Mwakasaka waliokisaidia kupata ushindi wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wilaya ya Tabora mjini ambapo CCM ilipata ushundi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akizungumza katika maadhimisho ya 38 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kijiji cha Mwisole wilayani Uyui ambapo aliwataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kwakuwa kimewaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu wa Taifa.
Hawa ni makada mahili wa CCM mkoa wa Tabora("MAJEMBE YA CCM TABORA")ambao wametambulika michango yao katika kukisaidia chama kwa hali na mali na kuhakikisha chama kinaendelea kujenga heshima yake katika kuwaongoza wananchi.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini ambaye ni kada wa chama hicho  Bw.Emmanuel  Mwakasaka akionesha heshima ya utii mbele ya viongozi baada ya kupokea cheti cha kumpongeza na kutambua mchango wake katika kukisaidia chama kupata ushindi uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wa mwaka 2014 ambapo CCM iliibuka mshindi dhidi ya vyama vya upinzani.



POLISI TABORA WAFANIKIWA KUMTIA NGUVUNI KIJANA MMOJA AKIWA NA RISASI 356 ZA SMG


Jumla ya risasi 356  za SMG zilizokamatwa askari Polisi  kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Wolfram Msemwa(32) huko katika mtaa wa Kazehill kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora.
Kitambulisho cha mtuhumiwa aliyekutwa na risasi hizo ambaye kabla ya kukamatwa tarehe 2/2/2015 aliwahi kuwakimbia askari Polisi  mnamo tarehe 23/11/2014 na kutelekeza begi alilokuwa amehifadhi bunduki aina ya SMG na risasi 17 katika eneo la Mazinge hospitali ya wilaya ya Sikonge

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akiwaonesha waandishi wa habari risasi zilizokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanikiwa kumtia nguvuni kijana huyo Wolfram Msemwa anayedaiwa amekuwa na mtandao na baadhi ya waharifu kutoka nchi jirani na Tanzania kwa upande wa Magharibi.