Saturday, February 14, 2015

TABORA WAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA





Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akizindua Mpango mkakati wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga,uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora ambao umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.

Baada ya kuzinduliwa mpango mkakati huo,wakuu wa wilaya za mkoa wa Tabora walipatiwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji,Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mpango mkakati huo mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mpango mkakati huo unaolenga kuimarisha afya za akinamama wajawazito na watoto wachanga na kupunguza vifo.
Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewji akipokea mpango mkakati huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tabora kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila.
Mganga mkuu mkoa wa Tabora Dr.Gunini Kamba akitoa maelezo mafupi kuhusu changamoto za huduma ya afya zinazoukabili mkoa wa Tabora na namna ambavyo mpango mkakati huo utakavyosaidia kuboresha huduma za afya kwa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito  na watoto wachanga.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akifungua mkutano wa uzinduzi wa mpango mkakati huo wa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga.
Baadhi ya wadau wa Afya kutoka sekta mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kupunguza vifo vya watoto wachanga na kinamama wajawazito.


 
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila ameonya vikali waganga wakuu wa wilaya na waratibu  wa huduma ya Afya ya mama na mtoto wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo hali inayosababisha kuendelea kuongezeka kwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga mkoani humo.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo hilo katika mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto uliofanyika jana katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora
uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya kutoka wilaya zote za mkoa huo, taasisi, mashirika na waandishi wa habari.

Alisema takwimu za idadi ya akinamama wajawazito na watoto wanaofariki kwa kukosa huduma au kutohudumiwa kwa wakati inazidi kuongezeka mkoani Tabora na vifo vingine vinavyotokea hata wataalamu
wa afya hawana taarifa, jambo hili sio zuri, lingeweza kuthibitiwa na watoa huduma katika vituo vya afya.

Alisema hakuna sababu ya mama mjamzito kupoteza maisha anapojifungua au mtoto wake kufariki
 kisa amekosa huduma wakati uwezekano wa kujifungua salama upo, rasilimali chache zilizopo zinaweza kutumika kuokoa maisha ya mama na mtoto wake kama watoa huduma watafanya kazi yao ipasavyo.

‘Kuanzia leo waganga wakuu wa wilaya (DMO’s) ni lazima mtoe taarifa za kifo chochote cha mama
mjamzito kitakachotokea katika kituo chako na utoe sababu kwa nini kimetokea ili mhusika aliyezembea achukuliwe hatua mara moja’, alisema.

Mwananzila aliwapongeza madaktari wote wanaotoa huduma za uzazi katika mradi wa Millenium ulioko
 katika vijiji 16 mkoani humo ambapo taarifa za utendaji zinaonyesha kwamba katika kipindi cha mwakamzima hakuna kifo hata kimoja cha mama mjamzito kilichotokea katika vijiji hivyo.

‘Nawapongeza madakatri na watoa huduma wote walioko katika mradi huu, mmekuwa mfano wa kuigwa,wataalamu wa afya katika kila halmashauri acheni kufanya kazi kwa mazoea, tumieni rasilimali zilizopo ipasavyo, alionya Mwananzila .
 
Mkuu wa mkoa aliwataka wakurunguzi , wakuu wa wilaya , waganga wa wilaya , waratibu wa afya ya uzazi,  makatibu Tawala wa wilaya na ,madiwani, watendaji, madaktari na wauguzi wote kusimamia zoezi hiloipasavyo  katika maeneo yao ili kuepusha vifo vyote vitokanavyo na uzazi.

Aidha aliagiza halmashauri zote kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea wataalamu wapya wa afya na
kada nyinginezo wanaopelekwa katika halmashauri hizo ili wafurahie mazingira ya kazi na waweze kuwa msaada mkubwa katika maeneo hayo.

Kuondoka kwa wataalamu wengi katika halmashauri nyingi kunachangiwa na halmashauri zenyewe kutoandaa
mazingira mazuri ya kuwapokea wataalamu wapya wanaoletwa na serikali.

Akitoa neno la shukrani Mratibu wa Huduma ya Uzazi kwa mama na mtoto Kanda ya Magharibi .
Martha Mlimba aliwataka waganga wakuu, waratibu wa afya na watoa huduma ya uzazi kwa mama na mtoto katika kila halmashauri kuzingatia agizo la RC katika utendaji kazi wao ili kupunguza vifo hivyo.

 
mwisho



No comments:

Post a Comment