Bondia
Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu
na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya
wafanyakazi wake kwenye bar yake iliyopo Morogoro.
Muda
mfupi uliopita Francis Cheka ameongea na millardayo.com na kusema ndio
alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue
karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua
hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10
nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.
No comments:
Post a Comment