Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika mkutano huo.
Wanachama
wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano
wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na
wanachama kutoka mikoa yote.
Dotto Mwaibale
JAJI
Mkuu Mohamed Chande, amewataka wanawake nchini kutoa taarifa katika
ngazi husika pindi wanapoombwa rushwa ya ngono ili sheria ifuate mkondo
wake.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake
Tanzania (TAWJA), alisema kunaidadi kubwa ya wanawake ndani ya jamii
wanaoombwa rushwa ya ngono lakini wamekuwa wahoga kutoa taarifa.
"Katika
rushwa ya ngono lazima sheria mahususi zichukuliwe,hivyo tunawasihi
wanawake baada ya kufanyiwa matukio hayo wafikishe malalamiko mahakamani
au sehemu husika na sheria itafuatwa," alisema Jaji Chande.
Kadhalika,
serikali itaendelea kuboresha mazingira ya majaji wanawake ili
kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya mahakama katika ngazi
zote.
Mwenyekiti
wa TAWJA, Engera Kileo, alifafanua katika kesi za rushwa ya ngono
mahakama kupitia kifungu cha 25,muhusika atakayebainika kujihusisha na
kitendo hicho atatozwa faini au adhabu ya kifungo cha miaka 30.
"Mahakama
imeweka adhabu hiyo kutokana na ongezeko la matukio kufanyika ndani ya
jamii na wanawake kujengewa woga wa kutoa taarifa kwa wakati, hivyo
tunachokifanya kuangalia namna ya kuongeza adhabu kwasababu ngono
imetawala katika sekta mbalimbali," alisema Kileo.
Lakini
kwa sasa chama hicho kinatoa elimu juu ya rushwa ya ngono katika jamii
na matumizi mabaya ya ngono zembe ili kuwalinda na magonjwa ya
kuambukizwa kama Maambukizi ya Ukimwi(VVu), na yale ya zinaa.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment