Na matukiodaimaBlog
WANANCHI
wa kijiji cha KIlondo kata ya Kilondo wilayani Ludewa
mkoani Njombe
wamempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa kuwa
mbunge pekee katika jimbo hilo kufika kulala chini ardhini kwenye
nyumba isiyo na mlango wala dirisha (Pagale) katika
kijijini hicho
toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961.Mbunge
Filikunjombe na msafara wake wa watu zaidi ya 15 walifika katika
kijiji hicho cha Kilondo kilichopo mwambao mwa ziwa nyasa kwa lengo
la mbunge huyo kuwaanzishia mchakato wa kupatiwa umeme kupitia
shirika lisilo la kiserikali la Kilondo Investment linalofadhiliwa na
mradi wa usambazaji vijijini (REA)
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho mwenyekiti wa serikali ya
kijiji hicho Bw Laurian Kyula alisema kuwa jimbo hilo limepata
kuwa na wabunge zaidi ya 5 ila hakuna mbunge ambae alifika na
kukubalia kulala katika kijiji hicho kutokana na kuwa na miundo
mbinu mibovu na kutokuwa na nyumba ya kisasa ya
kulala wageni zaidi
ya nyumba za wananchi ambazo nyingi zipo kienyeji zaidi hazina hadhi .
“Kweli tumeshindwa kuamini kuona mbunge anaamua kulala kijiji hapa
hata bila kuwepo kwa maandalizi mazuri ya kulala tumekuwa na wabunge
wengi sana ila wapo baadhi yao hata kukejeli kuwa kijiji hakina
hadhi ya kulaza waheshimiwa hadi watakapoboresha mazingira kati ya
viti ambavyo hatukupata kufikiria ni pamoja na
kuja kupokea mgeni wa kiwilaya kuja kulala hapa kijijini ila
wewe mheshimiwa wetu Filikunjombe umekuwa ni kiongozi wa aina yake”
alisema mwenyekiti huyo
Akimpongeza mbunge huyo kwa jitihada zake za kuwasogezea huduma ya umeme
kijijini hapo mwenyekiti huyo alisema kijiji hicho ni moja kati
vijiji ambavyo vipo mwambao mwa ziwa nyasa na uwezekano wa
kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa kutoka Ludewa mjini ama
Kyela mkoani Mbeya ni vigumu kutokana na kuzungukwa na milima na maji
hivyo kwa upande wao waliamini kabisa kamwe hawatakuja fikiwa na
huduma za umeme.
“Tunashindwa kujua ni kiasi gani mbunge wetu unavyotuhangaikia kwa
mambo ambayo wengine waliotangulia walituhakikishia kuwa ni vigumu
kufikiwa na huduma ya umeme kwa kuwa ni porini labda
haditutakaposogea karibu na vijiji vya nje ya Mwambao kauli ambazo
vilitufanya kukata tamaa kabisa kwa umeme kwetu ni huduma isiyo
wezekana ila tunashangazwa leo kupitia mbunge wetu Jembe
Filikunjombe unatuletea wataalam wa kuanza kujenga mradi wa umeme hapa
kijijini”
Bw
Kyula alisema kati ya mambo ambayo wao hawata kuja kusahau
maishani mwao ni utendaji kazi wa mbunge huyo na maendeleo makubwa
aliyoyafanya katika jimbo hilo la Ludewa kwa kipindi cha miaka minne
ya ubunge wake huku wapo waliokaa miaka mitano bila kufanyajambo
linaloonekana kwa wananchi wao.
Hivyo alisema iwapo chama cha mapinduzi (CCM) kitataka kulipoteza jimbo
hilo la Ludewa ni pamoja na kujaribu kufanya maamuzi yasiyo hitajika
kwa wananchi yakiwemo ya kukata jina la mbunge wao katika mchakato
wa kuomba kugombea ubunge jimbo hilo la Ludewa na kumpa nafasi mtu
wa kwao watashangazwa na maamuzi magumu ya wananchi kwa kulitoa
jimbo hilo upinzani kama fundisho kwa CCM kupenda wanachopenda wao na
sio wananchi.
Awali mkurugenzi mtendaji wa mradi wa Kilondo Investment Bw Erick
Mwambeleko akielezea mradi huo alisema kuwa mpango wa kuwaunganisha
wanakijiji hao na umeme ulikuwepo toka wakati mbunge Profesa Raphael
Mwalyosi akiwa madarakani ila cha kushangaza kila alipomfuata kutaka
kusaidia kufanikisha kuanzishwa kwa mradi huo aliishia kutoa kauli
za kukatisha tamaa kuwa haweza kusaidia kupeleka umeme kijijini hapo
kwa kuwa ni gizani sana hakuna faida yoyote .
“Ni kweli kijiji hiki cha Kilondo kipo porini zaidi ila kuna
watu wanaishi hata mimi Mwambeleko ni mzaliwa wa hapa hivyo
nimesoma sayansi na kutumia elimu yangu nikaona ngoja nishirikiane na
mbunge Filikunjombe kuleta ukombozi wa umeme huku kwa kupitia
kampuni yangu ya Kilondo Investment kampuni ambayo mchango wa mbunge ni
mkubwa zaidi hadi leo tunaanza mchakato wa kuleta umeme hapa”Alisema
kuwa tayari fedha kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 300 zimepatikana
kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo ambapo fedha hizo kiasi
zimetoka REA na nyingine ni fedha ambazo ni mchango wa mbunge
Filikunjombe .
Pia alisema umeme huo utazalisha kijijini hapo kupitia maporomoko ya
maji ya mto Makete ambayo yanaingia katika ziwa nysa na kuwa
maporomoko hayo yana nguvu ya kuzalisha umeme KV 50 na kasi ya maji
katika maporomoko hayo ni lita za ujazo 9312 kwa sekunde maji ambayo
yanatosha kabisa kwa uzalishaji wa umeme wa kutosha kaya zote
kijijini hapo na kijiji cha jirani.
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe akielezea sababu ya kulala
kijijini hapo alisema kuwa moja kati ya ahadi yake kwa wananchi wa
Ludewa ni kufikisha maendeleo kila kona ya jimbo hilo na kuwa akiwa
katika ziara pale ambapo jua litazamia ndipo atakapolala bila kujali
uwepo wa maandalizi ama lah.
“Wananchi wote wa Ludewa ni wapiga kura wangu hivyo imekuwa ni kawaida yangu
kuwa nao wakati wote na kulala popote na kula chochote ambao wao
wanakula siku zote hivyo jua linapozamia nikiwa
ziarani
nitalala hapo bila kujali maandalizi lengo kuona nashirikiana na
wananchi wangu kwa mazingira yoyote yale nimefurahi sana leo kulala
katika nyumba hii inayojengwa ambayo haina sakavu ,milango wala
madirisha (Pagale) mimi ni siufanyi ubunge kama ufalme kuwa nikija mimi
ziarani wananchi wangu wasumbuke kufanya maandalizi yasiyo ya
kawaida”
Kuhusua mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa lengo lake kuona
wananchi hao wanapatiwa umeme mapema zaidi ikiwezekana ndani ya mwaka
huu wananchi hao waweze na umeme katika makazi yao hivyo kuwaomba
wananchi kutoa ushirikiano kwa mafundi waliofika kijijini hapo
kuanza utekelezaji wa mradi huo pamoja na kuwasaidia kufanya tathimini
ya mahitaji ya taa na ufungaji umeme katika nyumba zao.
|
No comments:
Post a Comment