"INAUMA SANA SIJUI HAWA ASKARI POLISI NI WATOTO WA VIGOGO?"
HALI HALISI YA MAUAJI YA HASSAN MGALULA:
Askari
Polisi hao wakati wakimchukua kwenye usafiri wa Bajaji ya mizigo huku
wakiwa wamemkanyaga bila kujali hali mahututi aliyokuwanayo marehemu
Hassan Mgalula mara baada ya kipigo kikali kilichosababisha kifo chake
hapo baadaye,INASEMEKANA KUWA WALIPOFIKA KITUONI WALIFUNGUA
JALADA LILILOONESHA KUWA HASSAN AMEPIGWA NA WANANCHI WENYE
HASIRA KALI......(Picha hii kwa hisani ya Nassor Wazambi-Aliyekuwa Mwenyekiti
UVCCM wilaya ya Tabora mjini.)
POLISI wanne waliokuwa wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za mauaji ya mtu mmoja huko Wilayani Urambo ambao walifukuzwa kazi baada ya kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa wamerejeshwa kazini huku yakizuka maswali mengi yasiyo na majiibu juu ya kuachiwa kwao.
POLISI wanne waliokuwa wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za mauaji ya mtu mmoja huko Wilayani Urambo ambao walifukuzwa kazi baada ya kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa wamerejeshwa kazini huku yakizuka maswali mengi yasiyo na majiibu juu ya kuachiwa kwao.
Askari Polisi hao ambao
walifukuzwa kazi mnamo March 5 mwaka 2012 baada ya kubainika wamehusika
na tukio hilo la kinyama la kumpiga hadi kupoteza fahamu marehemu Hassan
Mgalula ambaye baade alipoteza maisha ni namba G 3037 Pc Aidano, namba
G 3836 Pc
Jonathan, namba G 4836 Pc Mohamed na mwingine ni namba G 5382 Pc
Khakimu.
Kuachiwa na kurejeshwa kazini kwa
askari Polisi hao wanne kumezua hali ya sitofahamu kuanzia kwa askari
Polisi wenzao hadi kwa wananchi wa wilaya ya Urambo ambao waliobahatika
kulishuhudia tukio la kumpiga raia huyo wa Urambo marehemu Hassan
Mgalula na baadae kufariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha Polisi
ambako lilifunguliwa jalada kwamba ameuawa na wananchi wenye hasira
kali.
Aidha juhudi za kumtafuta kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Athony Rutha ili kutolea ufafanuzi juu ya
kurudishwa kazini kwa askari hao zinaendelea lakini kumekuwa na dalili
za utata kutokana na askari hao imeelezwa kuwa kuna mikono ya vigogo wa
Jeshi la Polisi ngazi ya juu.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya
Urambo kutokana na tukio la kurejeshwa kazini kwa askari hao wanaodaiwa
kufanya unyama huo mnamo Februari 29 mwaka 2012 wameonesha dalili za
kukosa imani na Jeshi hilo huku wakilalamikia uongozi wa Polisi ngazi za
juu kwa kuendelea kuwabeba baadhi ya askari wanaotenda makosa kinyume
cha sheria.
No comments:
Post a Comment