Na Lucas Raphael Sikonge
MVUA
zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Sikonge, zimeleta madhara
kadhaa, baada ya watu wanne wa familia moja kulazwa hospitalini kutokana
na mshituko wa radi.
Akizungumza
na gazeti hili diwani wa kataka Kilolelo Boniface Mlimakala Mtani,
alisema tukio hilo la radi lilitokea hivi karibuni, ambapo familia hiyo
ilipata mshituko na kulazwa hospitalini huku mbwa wanne na mbuzi mmoja
wa familia hiyo wakipigwa radi na kufa hapohapo.
Mtani
alisema kuwa tukio la radi lilitokea ,ajira ya saa nane mchana,mwezi
machi 8,mwaka huu katika kitongoji cha Maweni B,kijiji cha
Kanyamsenga,kata ya Kiloleli.
Aliwataja
waliojeruhiwa na kulazwa hospitali,(DDH),wilayani Sikonge,kuwa ni
Aloyce Masima,(45),ambaye alijeruhiwa sehemu ya mguuni kama amemwagiwa
maji ya moto,Paulo James(18), Hoka Kazinza (16),na Gabriel Aloyce (2).
Mtani
aliongeza kuwa familia hiyo ililazwa hospitali kwa siku moja kabla ya
kuruhusiwa kurejea nyumbani,kati yao watoto watatu walipata mshituko wa
radi huku baba yao akibabuliwa mguuni na radi hiyo.
Akiongea
zaidi diwani huyo alisema baada kupata taarifa hizo alifika nyumbani
walipokuwa wakiishi na kukuta wamepoteza fahamu huku mbwa wanne na mbuzi
mmoja wakiwa wameshakufa kwa kupigwa na radi hiyo.
Hata
hivyo diwani huyo alisema kuwa licha ya familia hiyo moja kupigwa na
radi,hakukuwa na mvua yoyote kijijini hapo zaidi ya kuwepo mawingu,huku
mvua ikiwa inanyesha kilomita moja toka eneo la tukio.
Katika
hatua nyingine Mtani aliongeza kuwa zoezi la kuwasaka watoto
wanaotakiwa kuingia sekondari baada ya kufaulu bado linaendelea na
limeanza kuzaa matunda.
No comments:
Post a Comment