NA LUCAS RAPAHEL
Baada
ya miaka 12 kupita hatimaye mkoa wa Tabora umefanikiwa kupata timu itakayoshirikia
katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara
msimu ujao wa 2013/2014 kupitia timu ya
Rhino Rangers inayamilikwa na jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kabla
ya timu hiyo kuweka rekodi mpya kwa mara
ya mwisho timu ya Milambo ya Tabora ilishuka ligi daraja la kwanza Tanzania bara
mwaka 2000 ,timu ambayo chanzo chake ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora kwa
wakati huo Dk Laurent Gama kwani alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM ndio ukawa
mwanzo wa timu hiyo kupoteza mwelekeo katika medani ya soka nchini. .
Lakini
historia ya soka la mkoa wa Tabora imechukua sura mpya kufuatia timu pekee ya
Jeshi la wananchi Watanzania, Rhino Rangers kujihakikishia nafasi ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya
kuongoza kundi C la ligi daraja la kwanza lililokuwa na ushindani wa aina yake ikiwa
imefikisha pointi 29 huku ikiwa na mchezo mmoja,pointi ambazo hazitaweza kufikiwa
na timu yoyote katika kundi hilo.
Timu
ambazo zilizopo katika kundi c ni Kanembwa
JKT, Polisi Dodoma, Polisi Tabora, Mwadui, Pamba, Polisi Mara, Molani ya mkoa
wa Manyara na Rhino ambaye ndio mbabe wa kundi hilo.
Akizungumza
na mwandishi wa makala haya mlezi wa timu hiyo ya Rhino Mnadhimu Mkuu wa
Mafunzo na Utendaji wa Kivita wa Faru ya Brigedi Kanali Simon Hongoa amesema
kwamba mafanikio ya timu hiyo hayakuja kama mvua bali wampitia
vikwanzo vingi na hatimaye mafanikio ambayo yanaonekana hii leo .
Amesema
kwamba Rhino Rangers ilianza mwaka 1994 baada ya kuvunjika kwa timu ya divisheni
ya 20 mwaka 1993 na kuanzia hapo Rhino ilianza kusukwa ili iwe timu ya
ushindani ndani na nje ya mkoa wa Tabora.
Kanali
huyo wa JWTZ amesema kwamba timu
hiyo ilianzia daraja la nne, kupanda hadi kufikia daraja la tatu na la pili kupitia mfumo wa zamani wa FAT kabla ya
mabadiliko ya ushiriki wa madaraja ya
soka kufanywa na shirikisho la soka nchini TFF..
Amesema
kwamba katika vipindi tafauti ya mashindano hayo kunzia mwaka 1995 hadi mwaka
1999 walishindana kwa kila hali kupanda daraja la kwanza lakini walikutano na
vikwanzo vingi ingawa hawakukata tamaa ya kushiriki katika ligi hiyo licha ya
kuwa mabingwa wa mkoa mara kadhaa .
Katika
jitiada zao waliweza kufikia nafasi ya tano kwa makundi ,kwa mfano mwaka 1998
walishiriki ligi daraja la kwanza na kufakikiwa kushika nafasi ya tano na kuachwa
na timu zingine zikipanda ligi kuu.
Katika
harakati za kufanya vizuri timu hiyo ilivunjwa kwa mara nyingine mwaka 1999 hadi mwaka 2006 ilipofufuliwa tena baada ya ujuo wa kanali huyo wa jeshi la
wananchi kufika katika kanda hii ya Magharibi.
Kanali
Hongoa amesema wakati timu hiyo ilikuwa na mambo mengi yaliyopelekea kufutwa tena kwenye anga la soka.Mwaka 2007 ilishiriki ligi daraja la tatu ngazi ya taifa
na kufanikiwa kuwa bingwa wa mkoa wa Tabora mwaka wa 2008.
Amesema
jitiada zao zilianza mwaka 2009 na mwaka 2010 waliweza kushika nafasi ya tano
kati ya timu zilizoshiriki katika ligi ya makundi wakati huo iilifanyikia mkoa
wa tanga na kufaniwa kuingiza timu za Costal Union,Villa Squad,oljoro JKT na Moro
utd ..
Lakini
aliendelea kusema kwamba jitihada zao walitegemea wangeweza kupanda ligi
kuu mwaka 2011 lakini walitimuliwa vumbi na timu za Polisi moro ,JKT Mgambo,na Prison
ya Mbeya ambazo zilifanikiwa kuingia ligi ya kuu ya Vodacom wakati huo ligi ya
makundi ilifanyika nkoa wa Morogoro..
Pamoja
na vikwazo hivyo hawakukata tamaa ya kuendelea kushiriki na kuwania nafasi ya
kupanda ligi kuu huku wananchi wa mkoa
wa Tabora waliweza kuwatia moyo na jitiada za wachezaji wake wamefanikiwa
kuingia ligi kuu hiyo ya Vodacom Tanzania bara.
Amesema
kwa hiyo ni faraja kwa Jeshi la Wananchi kwa kupata hata timu moja inayoshiriki
ligi kuu ya soka nchini kwani timu zinazoshiriki
ligi hiyo zinamilikiwa na Jeshi la Kujenga
Taifa JKT na zinafanya vizuri kwa sasa .
Kamanda
huyo kwa jina maarufu “babu” amesema kwamba jitihada zilizopo ni kuhakikisha Rhino
inafanya usajiri wa kufa mtu kwani wanataka kuwa na timu bora na sio bora timu.
“hatutaki
kunusa tu katika ligi hiyo na mwaka unaofuata tusiwepo hilo kwetu hatulitaki
kusikia bali mshikamano kutoka kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kwani ndio nguzo
kubwa toka mwanzo kwa ligi hii inayotarajiwa
kumalizika tarehe 17 mwezi huu” .Amesema kanali Hongoa.
Ametaja
kikosi kilichoweza kupandisha timu hiyo ya Jeshi la wananchi wa Tanzania kuwa makipa
ni Idd Kihulya,Charles Mpinki na Abdullakarim Mtumwa.
Mabeki
wa pembeni kulia na kushoto ni Salum Mambo ,James Barton ,Frank Konye ,Ally
Mwanyiro ,Stanley Mlay na Joseph Mapunda.
wengine
ni viungo ambao ni Stanlaus Mwakitosi ,Ramadhani Sheweji ,Emanuel Noel ,Steven
Maztudd ,Bakari Maadhi na Salum Majid.
Pia
amewataja viongo wa kati ni Julias Masunga, Issa Salum, Ayub Iddy, Joseph
Sangadata na Ussi Makeme ,hao wakifuatiwa na washambulia wa Timu hiyo ambao ni
Shija Joseph ,Magesa omary ,Doi Mobi ,Msafiri Mbilinyi, Samwel Mwamasangura,shija
Mvugo Abdallh Simba,Victor Anghaya Abbas Mohamed na Mchembi Maganga.
Hata
hivyo kanali Hongoa amewashukuru wakazi
wa mkoa wa Tabora wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan
Wakasuvi, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya Tabora na wadau wote wa soka ambao
wamejitolea kwa hali na mali ili kufanikiwa kwa timu hiyo kufika hapo ilipofika
leo.
Aidha
kocha wa timu hiyo ya Rhino Renatus Shija amesema kwamba halipofika katika timu
hiyo aliangali history ya Rhino na baada
ya kuangali aliweka mkakati wa kuhakikisha wana maliza raun di ya kwanza
wakiwa wanaongoza ligi daraja la kwanza na hivyo kuhakikisha watoki katika
nafsi hiyo hali iliyowasaidia sana kufika hapa walipofikia.
Mara
baada ya kumaliza raundi ya kwanza na kuongoza kundi C kwa pointi 17 wakapanga kuhakikisha wanashinda
michezo mitano waliyopangiwa kucheza katika uwanja wa nyumbani wa Ally Hassan Mwinyi katika mzunguko wa pili
wa ligi hiyo ili waweze kuongoza na kupanda daraja jambo ambalo wamefanikiwa.
Amesema
kwamba amependa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa timu hiyo ya Jeshi na
wananchi wa mkoa wa Tabora kuwapa sapoti
ya nguvu kwa wameina timu hiyo kama yako.
Kwa sasa wanampango wa kuhakikisha wanapata timu bora yenye
wachezaji wenye uzoefu na ligi hiyo ,kwani ligi kuu ni mambo mengi ambayo yanabidi kuyafanyika kazi kabla
ya ligi hiyo kuanza na kuongeza kwamba anataka tinu hiyo ya Rhino kuweka
history ya kuchukua ubingwa wa bara mwakani .
Kapteni wa Timu ya Rhino
Shija Joseph amesema kwamba mafaniko ya timu hiyo ni mikakati ya
viongozi wa jeshi hilo ,viongozi wa serikali pamoja na wananchi wa mkoa wa
Tabora kwa kupatia ushirikiano mkubwa na kuhakikisha wanafika hapo walipofika
leo.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora (TAREFA) , Yussuph
Kitumbo alisema kwamba lengo la kukikisha timu mojawapo ambazo zilishirikia
kwenye ligi daraja la kwanza mwaka huu mkooani hapa zinapanda na hilo,limewezekana
“Nina imani kuwa sisi
kama TAREFA,serikali ya mkoa,wadau na wapenzi tukishikamana nina imani kubwa
soka ya Tabora inakuwa kwa kasi kwani kuna vipaji vingi sana mitaani ambavyo
vijana waliopo wanapaswa kuendelezwa katika michezo mbalimbali.” Alisema
Kitumbo.
Amesema kwamba baada ya timu ya Rhino kufikia hapo ilipofikia
basi uzalendo kwanza ili tuonyeshe mapenzi ya kweli na timu hiyo ambayo kwa
sasa ni ya wana Tabora wote .
Mwisho
No comments:
Post a Comment