Mh Tundulisu akitoa Vyeti kwa wana chaso katika Haflahio,
WAANDISHI wa habari wapo katika hatari kubwa ya kutoweka nchini kutokana na kuandika maovu yanayofanywa na viongozi wa serikali.
Haya yamezungumzwa na Mbunge wa Singida
Mashariki na mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu katika
mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa (CHASO)
katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kilichopo katika Manispaa ya Iringa.
Lissu alisema waandishi wa habari wapo
katika hatari ya kutoweka hasa kwa kuuawa kutokana na ukweli wao
wanaouandika hasa kuyaweka madudu ya baadhi ya viongozi wa serikali.
Alisema hasa katika ripoti ya uchunguzi
ya mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ya tume iliyoundwa na
vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) inaonesha wazi juu ya
hatari walionayo waandishi wa habari.
Alitaja chanzo cha kuwamaliza waandishi
hao kuwa ni polisi wanaotumiwa na viongozi hao kama njia ya kuzuia
kuendelea kuandika madudu yao.
Hata hivyo alisema waajiri wa waandishi
ni chanzo moja wapo cha kinachochangia waandishi kuwa katika hatari hiyo
kwa kuwatengenezea mazingira mabovu ya utendaji wao hasa wawapo kazini.
Lissu alisema waandishi wa habari ambao
wapo katika hatari kubwa ni wa Iringa ambao tayari wapo katika listi ya
kupotezwa kwa namna yoyote kwa kile kilichoelezwa kuwa hawaandiki habari
zao kwa unafiki.
"Tuwalinde sana waandishi wa habari kwa
kweli wapo katika hatali kubwa sana. Kila mmoja awe mlinzi wa waandishi
hawa na ifike mahali tukasema hatutaki Mwangosi mwingine. Hasa waandishi
hawa wa Iringa wapo katika wakati mgumu sana" alisema.
Pia aliwaasa wanafunzi waliomaliza kwenda kuungana na wananchi kuendeleza harakati za Mageuzi kuanzia katika Mashina,kata, na Majimbo ili kufanikisha mpango wa kuelekea ikulu vinginevyo ni ndoto hapondipo utatokea ukombozi wa Waalimu, Madaktari, na Wanasheria
Wasio na kazi kwasababu ya Mipango mibovu ya utawala uliopo kupata furusa ya kuitumikia nchihii kukiandaliwa mipango mizuri ya ajira,
Historia inaonyesha hakuna Mzee aliefanikisha mapinduzi ya kisiasa katika nchiyake kama hakuanza wakati akiwa kijana na kuelekea katika Mafanikio ndipo uzee unamkuta akiwemo ndani ya Harakati,