MAKAMU ASKOFU MKUU WA KANISA LA FPCT WILSON LAZARO WAKATI AKIZUNDUA UFUNGUZI WA KANISA HILO KILOLENI TABORA MJINI JANA |
AKIKATA UTEPE KUHASHIRIA KUFUNGUZI RASMI WA KANISA HILO LA FPCT |
MTOTO FARAJA MUSA MWANAFUNZI WA SHULE YA AWALI KILOLENI AKISHEREHESHA UFUNGUZI WA KANISA HILO |
WAUMINI WA KANISA HILO WAKIWA KATIKA MISA MAALUMU KWA AJILI YA UFUNGUZI RASMI WA KANISA HILO |
Na Lucas Raphael,Tabora
KANISA la Free Pentecostal Church
Tanzania (FPCT) limelaani vikali vitendo vionavyofanywa na baadhi ya watu
kuwakata mikono walemavu wa ngozi Albino kwa imani za kishirikina.
Kauli hiyo ilitolewa na Makamu
Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Wilson Lazaro kwenye sherehe za uzinduzi wa
Kanisa la FPCT Palishi ya Kiloleni mjini Tabora.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Askofu Lazaro alisema vitendo vinaendelea kufanywa na watu kuamua kukata mikono
ya mlemavu kwa tama ya kupata utajili wa haraka havina budi kulaaniwa na watu
wote.
Askofu Lazaro aliiomba Serikali
kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwanyima dhamana watu wanaofikishwa katika
vyombo vya sheria kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watu wenye ulemavu wa ngozi
Albino, lengo nikudhibiti matukio kama hayo yasiendelee kutokea katika jamii.
“Wewe kama huna fedha za kuendesha
maisha yako hapa duniani nenda shamba ukalime sio kuamua kumkata mwenzako
mikono eti tu umedanganywa na mganga wako wa kienyeji” alisema Askofu Lazaro
Kuhusu mchakato wa upatikanaji wa
katiba mpya, Askofu huyo aliwaomba watanzania kuliombea kwa Mungu bunge la
kutunga katiba, ili liweze kutunga katiba ambayo itaweza kukidhi
mahitaji, majawabu na matarajio ya watanzania wote.
Aliwataka wajumbe wa bunge la katiba
kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi ya vyama vyao ili waeze kujadili
kifungu kwa kifungu, ukurasa kwa ukurasa na hatimaye siku ya mwisho waweze
kuwaletea watanzania katiba bora inayolenga kuinua uchumi wa kila mtanzania.
Katika sherehe hizo za uzinduzi wa
kanisa hilo, pia uliambatana shughuli za kusimikwa kwa mchungaji kiongozi wa
Kanisa la FPCT Kiloleni Peter Shani ambaye ndiye atakuwa mchungaji mkuu wa
kanisa la mahali pale.
Mwisho
No comments:
Post a Comment