Monday, August 25, 2014

WAKULIMA WAWAFYEKA MIGUU NG'OMBE 14 KULIPA KISASI KWA WAFUGAJI-KIGOMA

 
Na Magreth Magosso,Kigoma

IMEELEZWA kuwa,ng`ombe 14 wapo hatarini kupoteza uhai,baada  ya kukatwa miguu yote minne na jamii ya wakulima wa Kijiji cha mgambazi kata ya Igalula wilaya ya uvinza mkoani hapa.huku viongozi 11 wa chama cha Chadema walala lupango.

Hali hiyo inachangiwa na mgogoro uliopo baina ya  kundi la wafugaji wa kisukuma kukaidi kwenda kuishi kwenye maeneo yaliyotengwa kwa malisho katika kijiji hicho ,ili kuondoa mgogoro wa mifugo hiyo kutoendelea  kuharibu  mashamba ya wakulima.

Pia  changamoto hiyo,imepelekea diwani wa kijiji cha mgambazi Abel Chiza(chadema) na mtendaji wa kijiji hicho kuswekwa mahabusu kwa siku nne ili kutoa ufafanuzi juu ya jeuri  inayofanywa na wafugaji  kugoma kuhamisha mifugo katika maeneo ya wakulima na kuathiri  uhai wa ng`ombe hao.

Akizungumzia  hilo  Katibu  Mkuu wa chama cha chadema Mkoani hapa Shaban Madede  alisema,alipewa taarifa na wananchi wa kijiji hicho kuwa viongozi wa chama cha Chadema watiwa nguvuni kutokana na mgogoro mkubwa wa wakulima na wafugaji .

“leo ng`ombe 200 zimeingia kinyemela bila idhini ya kijiji ,wakulima wanawafukuza ,mkurugenzi aliwapa siku 14 wafugaji wakaishi katika maeneo yao lakini hawataki mkuu wa mkoa na katibu tawala wawajibike waache siasa” alisema Madede.

Jamboleo likazungumza na Kamanda wa Polisi wa hapa Jaffar Mohamed  juu ya hilo alisema  watu saba wapo mahabusu ambapo wakulima watatu na wafugaji wane kwa upande wa wafugaji wamekiuka sheria na taratibu za mazingira kwa kupeleka mifugo  maeneo yenye vyanzo vya maji na kwa upande wa wakulima wamehukumu mifugo kinyuume cha sheria na taratibu husika.

Mohamed alisema,hawajakamata viongozi wa chadema ila waliokiuka sheria na hilo lilipelekea kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo  kuweka ulinzi kwa raia kwa kupeleka  askaripolisi  kutoa kituo cha kati na  uvinza  katika kijiji cha mgambazi kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao .

Pia  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Nicholas Kombe kama  alitoa siku 14 wafugaji kuondoa mifugo katika maeneo ya wakulima , Kombe  akiri hilo na kudai shida  ipo kwa wafugaji kukiuka sheria,taratibu na kanuni za kijiji hicho na kusisitiza sheria izingatie uhalisia wa chanzo cha kukatwa miguu kwa ng`ombe hizo.

Kijiji kina mpango  bora wa ardhi katika kijiji cha mgambazi na Lukoma kata ya igalula  ambao ni mahususi kwa jamii ya wakulima na wafugaji kwa lengo la kuondoa mgogoro wa kuvamiana kulingana na shughuli zao.

Hivyo,kuswekwa mahabusu kwa diwani wa chadema na mtendaji wa kijiji ni moja ya hatua ya kubaini uihalisia wa mgogoro usioisha kwa wakazi hao,ambapo wao ni watendaji wakuu wa kijiji hicho na kudai uwepo wa askaripolisi kule ni kuimarisha ulinzi wa umma.

No comments:

Post a Comment