Wednesday, May 8, 2013

LHRC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOANI KUHUSU HAKI ZA BINADAMU KWA UFADHILI WA EU -DAR ES SALAAM


Balozi wa nchi za Ulaya(EU)nchini Tanzania Filberto Sebregond(kulia )akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchi inayohusu masuala ya haki za binadamu,Kwenye ukumbi wa  Wanyama Hotesl Jijini Dar Es Salaam.

Picha ya pamoja Kati ya Balozi wa nchi za Ulaya(EU)nchini Tanzania Filberto Sebregond na washiriki na waandaji wa wa mafunzo ya haki za binadamu

Rose Mwalongo ambaye ni afisa habari wa kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC)akisalimiana na Balozi wa nchi za Ulaya(EU)nchini Tanzania Filberto Sebregond


waandishi wakimfanyia mahojiano Balozi wa nchi za Ulaya(EU)nchini Tanzania Filberto Sebregond

KISIMA CHAENDELEA KUUA WATU,WANANCHI WAKUMBWA NA HOFU KUBWA KILOLENI-TABORA MJINI

Askari wa kikosi cha zimamoto mjini Tabora wakiutoa mwili wa mwanamke ambaye amekutwa amekufa katika kisima cha maji maarufu Bombamzinga kilichopo kata ya Kiloleni Tabora mjini,Mwanamke huyo ametambulika kwa jina la Hawa Ramadhani Mzee ambaye alikuwa na umri wa miaka 42 ambaye pia inasemekana alikuwa na matatizo ya akili.
Diwani wa kata ya Kiloleni Bw.Juma Matalu (katikati)akishuhudia tukio la kifo cha mwanamke huyo katika kisima ambacho kimekuwa kikihusishwa na matukio ya mauaji ya watu kadhaa kwasasa hali inayotishia amani kwa wakazi wa kata ya Kiloleni.
Baadhi ya Askari wa Jwtz,Polisi na wa kikosi cha zimamoto Tabora mjini waliposhirikiana kuutoa mwili wa mwanamke huyo.



MAHAFALI YA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TPSC YANAFANYIKA TABORA HIVI SASA.

 

 Mahafali ya 14 ya chuo cha utumishi wa umma TPSC yanafanyika hivi sasa mkoani Tabora.

AJALI KAZINI ?


 ASKARI HUYO AMBAYE JINA LAKE HALIKUPATIKANA MARA MOJA ALIKUWA ANATAKA KUSHUKA ILI HAWAI KAZINI NDIPOM GARI LIKAONDOKA NA KUNGUKA HUKU AKIWA NA BUNDUKI KIFUANI KAMA UNAVYOONA

CCM YA TUPILIA MBALI ZIARA ZA MADIWAN ZA MILL,82.3





 NA LUCAS RAPHAEL NZEGA



 

CHAMA cha mapinduzi ccm wilayani nzega mkoani Tabora kimetupilia mbali ziara iliyopangwa kufanywa na Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya, iliyokadiliwa kutumia kias cha Mill,82.3 katika mikoa ya Arusha,Singida,Dodoma pamoja Moshi kwa muda wa siku kumi na nne(14) kwa malengo ya kujifunza mambo malimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mwenyekiti wa chama hicho wilaya Amosi Majire kanuda alisema kuwa kamati ya siasa wilaya ilikutana na kutoa uamzi huo kutokana na kuona wilaya inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

Alisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Resolute ulilipa halmashauri hiyo kias cha shilingi Bill 2.4 kama malipo ya ushuru wa huduma wa madeni nyuma,fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya amana hadi April 15 zilipo toa faida ya shilingi Mill 82.3

Alisema kwa kiwango hicho kilichotengwa kufanyia ziara kwa madiwani hao kimebadilishwa badala yake fedha hizo zielekezwe katika mambo ya maendeleo mengine yenye tija kwa wananchi.

Alisema Baraza hilo lilipanga kufungua Benki ya kijamii itakayo weza kukopesha wananchi lengo likiwa ni kuinua uchumi na kukuza wajasilia mali,kamati hiyo imetengua uanzishwaji wa benk hiyo badala yake fedha hizo kila kata itapatiwa kias cha shilingi Mill,50 hadi 61 iliwananchi waweze kufanya mambo ya maendeleo.

Kanuda alifafanua sababu za kuzuia benk hiyo ni kutokana na kuwepo kwa Taasisi mbalimbali za kibenk wilaya hapa hivyo wananchi wanafursa ya kukopo na kujiendeleza kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla.

‘’madiwani wanapaswa kuiangalia jamii kwanza inataka nini sio kujiangalia wao kwani ziara hiyo inatija lakini wananchi kwanza kunakero mbalimbali zipo hapa tumeamua fedha hizo wazigawe kwa kila kata na wananchi watasema wanataka nini kwani fedha hizo ni zawananchi’’alisema mwenyekiti huyo.

Alisema chama cha mapinduzi kina madiwani wengi kimeshauri mambo hayo ya msingi kwa kujali masirahi ya wananchi na kuongeza kuwa ziara za madiwani ni kwa mujibu wa kisheria hivyo ziara zao watakwenda ilikuweza kuleta maendeleo.

Alisema kabla ya kuanza ziara hiyo madiwani hao watapaswa kuwaeleza wananchi madhumuni ya ziara yao na kuwahakikishia mafanikio ya zaira hizo ili kuweza kushirikisha wananchi katika maamuzi thabiti tofauti na hili lilivyo kuwa limejitokeza pamoja na matumizi makubwa ya fedha huku wananchi wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kero.

Aliwataka wabunge na madiwani wote kwa ujumla kuwa Baraza la madiwani la halimashauri hiyo lijalo kubadilisha Bajeti ndogo ya fedha za ushuru wa Huduma shilingi Bill 2.4 zielekezwe kwenye mipango ya maendeleo itakayo gusa wananchi.

Hata hivyo mwenyekiti  huyo wa chama cha mapinduzi wilaya ya nzega alivitaka vyama vya upinzani kutowaposha wananchi juu ya fesha hizo bali kuwaeleza kweli wananchi hao matumizi sahihi juu ya fedha hizo kwani fedha hizo zilitowalewakwa ajili ya matumizi ya wananchi wa wilaya ya nzega.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi alipoulizwa suala hilo alisema kuwa serikali imechukua hatua za awari za kusimamisha ziara hiyo hadi pale uchunguzi na matumizi thabiti yatakapo patikana ya fedha hizo.

Alisema kuwa wilaya ya Nzega inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa na uhaba wa madawa,madawati pamoja na zaidi ya nyumba 354 za wananchi kudondoka kutokana na mafuriko yaliyotokea mwezi March na April.

 Baraza la madiwani la halmashauri hiyo lililofanyika kati ya April 24 na 25 mwaka huu lilipitisha mchanganuo wa bajeti ndogo ya fedha za ushuru wa huduma zilizo lipwa na mgodi wa dhahabu wa resolute Bill,2.4 huku ziara ya madiwani na wabunge wawili kutumia Mill,82.3, Mill,300.7 kulipa madeni ya halmashauri pamoja na Bill,2 uanzishwaji wa Benk ya kijamii,aidha Fedha hizo zitaendelea kuwekwa kwenye akaunti ya amana hadi mchakato utakapo kamilika.

Mwisho.
 


WIALYA ZA URAMBO NA KALIUA KUKUMBWA NA BAA LA NJAA .



NA LUCAS RAPHAEL,URAMBO 

 
Wakazi wa wilaya za Urambo na Kaliua watakumbwa na baa la njaa iwapo serikali na wananchi wenyewe hawata siamamia ipasavyo utunzaji wa chakula walichovuna  kutokana na mvua kuharibu vibaya asilima  35 za hekta ya zao la mahindi  yaliyolimwa msimu huu.   Akijibu hoja za madiwani kuhusu hali ya chakula katika wilaya hizo afisa kilimo  Erasto Konga alisema kuwa  uzalishaji wa mazao ya chakula msimu huu hasa mahindi siyo mzuri kutokana na kuharibiwa na ukame  kutokana na kutonyesha mvua wakati wa mwezi   wa pili na watatu.   Konga amebainisha kuwa makadirio ya chakula kwa wakazi  564,895 wa wilaya hizo mbili ni tani 195,776  hivyo  akatoa  wito kwa madiwani hao  kuwaelekeza wananchi  kununua chakula  hasa mahindi  kutoka maeneo mengine hapa nchini.   Aliongeza kuwa zaidi ya tani 90,000 za chakula kinachozalishwa na wakulima wa wilaya hizo ni  cha wanga huku wananchi wakipendelea kutumia  kwa wingi mahindi  kama chakula   japo wananalima  mpunga ambao ufanywa kama zao la biashara.   Afisa kilimo huyo ameliambia gazeti hili kuwa kiashiria moja wapo ambacho  kinaonyesha kuwepo kwa tatizo la njaa ni kutokana na kutoshuka kwa bei ya mahindi hadi sasa kwani debe la mahindi kung’ang’ania  shilingi 9000/= badala ya thsh 3500/= au 4000/= wakati wa msimu wa mavuno hali ambayo inaonyesha kwamba mahindi hayapo.   Konga ameongeza kwamba bado wimbi la walanguzi linatishia hali ya chakula katika wilaya hizi mbili  kwani pamoja na serikali kuwahimiza wananchi wasiuze chakula lakini wengi wao ulazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kujipatia mahitaji.   Amesema kuwa uzalishaji wa zao la muogo pia utapungua msimu huu kutokana na zao hilo kukumbwa na ugonjwa wa BATO BATO KALI  hivyo kuongeza .   Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2012 / 2013 zilipangwa kulimwa hekta 
135, 704 za mazao ya  chakula  ambazo zilitarajia kuzalisha tani 325,465
ambapo hekta za mazao ya chakula zilizolimwa ni 131, 785 sawa na asilimia
 97 ya lengo.

 

Naye mkuu wa wilaya hiyo Anna  Magowa aliwataka watendaji kutafuta ni 
jinsi gani watakabiliana na tatizo hilo la upungufu wa chakula hasa mahindi 
ambao umekuwa ukiikumba wilaya hiyo mara kwa mara.

 

Aliongeza kuwa watafute uwezekano wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji
hasa utumiaji wa matone kwani ndio hatumii maji mengi kwenye mazao ya 
mahindi  kutokana na tatizo la upungufu wa mvua.

 

MWISHO.

SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI KUWA NA NIDHAMU MAHALI PAKAZI

Na Lucas Raphael ,Siginda




SERIKALI imewataka viongozi wa kada mbalimbali pamoja na wananchi kuwa na nidhamu na uwajibikaji mahali pakazi ili iwesehemu kubwa ya mabadiliko ya kimaendeleo ya kiuchumi na sayansi na Teknolojia hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Ubinafisishaji na uwekezaji Dkt,Merry Nagu wakati akifunga mkutano wa kuhamasisha matumizi ya sayansi na Tekinolojia kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi kanda ya kati singida.

Alisema Serikali imelenga kukuza uchumi kwa wafanya Biashara wakubwa na wadogo kupitia sayansi na Tekinolojia ikiwa na kuzingatia nidhamu na uwajibikaji mahali pakazi.

Alisema kuwa baadhi ya viongozi hawatambui wajibu wao kwa kukosa ni dhamu na uwajibikaji mahali pakzi badala yake husababisha miradi mingi ya kimaendeleo kudorola.

Alesema viongozi wanapaswa kujitambua na kujua uwepo wao katika nafasi husika ili waweze kutekeleza kero za wananchi ikiwa na kuleta maendeleo dhabiti kwa maeneo husika.

Alisema kuwa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) linahakikisha mikutano hiyo inaendelea kupitia makundi mbalimbali ikiwepo na ngazi za mikoa,wilaya na kata lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi watumie sayansi na tekinolojia katika kukuza uchumi wa ndani nje.

Waziri Nagu alisema kuwa yote hayo yanatokana na nidhamu kwa viongozi,wadau pamoja na uwajibikaji mahali pakazi ilikuweza kufikia malengo hayo.

Alisema Baraza la Biashara Tanzani TNBC limeweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2025 litafikia malengo hayo ya kukuza uchumi kwa watanzania hususani wajasilia mali wa dogo na wa kubwa na kuondokana na umasikini.

Alisema Baraza hilo limeweka vipaumbele vitavyo changia kukuza uchumi huku vikiendelea kufanyiwa malekesho ilikufikia malengo hayo ni pamoja na upatikanaji wa maji safi,Kilimo na mifugo,miundombinu ambayo ni Barabara,Reli na Bandari lengo likiwa ni kuimalisha miundombinu hiyo.

Vipaumbele vingine ni pamoja na kuimalisha nisharti na madini ilikuweza kukuza uzalishaji,ukusanyaji madhubuti wa mapato ya ndani na je pamoja na kutoa elimu mbadala kwa wananchi dhidi ya miradi husika.

Kwaupande wake kamishina  msaidizi,mwandamizi wa polis makao makuu Dar es salaam Lucas Kusima akiwasilisha maada ya umuhimu wa usalama wa watu na mali zao katika mageuzi ya kiuchumi ya sayansi na tekinolojia kwa jamii.

Alisema kuwa jeshi hilo limejipanga kukabiliana na majambazi yanayotumia Tekinolojia  hiyo ikiwepo na huduma ya kibenki A T M,Simu za kiganjani,mitandao ya kijamii pamoja na mitandao mingne.

Kusima amewataka wananchi kutoa ushirikia wa kutosha kwa wahalifu hao kupitia Teknolojia za mawasiliano ilikuweza kukuza uchumi huo na kuimalisha ulinzi na usalama kwa mali za wananchi ikiwa na wananchi kwa ujumla.

Mkutano huo wa kuhamasisha matumizi ya sayansi na tekinolojia kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi umeyakutanisha makundi mbalimbali wakiwepo wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na mikoa pamoja na wakuu wa mikoa kwa mikoa mitatu ikiwa ni Singida,Tabora na Dodoma.

Mwisho.