Tuesday, August 6, 2013
CCM NA MADIWANI WAKE TABORA MJINI WAVUTANA UCHAGUZI WA NAIBU MEYA
![]() |
| Ofisi ya CCM wilaya ya Tabora mjini |
KUMEZUKA hali ya sintofahamu miongoni mwa madiwani wa halmashauri ya
manispaa Tabora, uongozi wa CCM, baaada ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Tabora Hassan Wakasuvi kuahirisha uchaguzi wa naibu meya wa manispaa
hiyo.
Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike tangu julai 31,2013 ambapo uchaguzi
huo hufanyika kila mwaka na nafasi hiyo hadi uchaguzi huo unafanyika
ilikuwa ikishikiliwa na diwani wa kata ya Ipuli Bw.Waziri Mlenda.
Hata hivyo licha ya uchaguzi huo kuhairishwa hakuna taarifa yoyote ya
mkoa ilioonyesha ni lini uchaguzi huo utafanyika,lakini imedaiwa kuwa
kuna mipango ya kutaka kuchakachua wagombea wasiotakiwa na baadhi,
vigogo wa mkoa wa Tabora ndani ya CCM na kuweka anayetakiwa.
CCM wilaya ilipendekeza majina ya wagombea ambao ni Musa Msamazi,Salum
Luzila,Shaban Kaombwe,Alfonce Shushi, Waziri Mlenda ambaye imedaiwa
alipata alama mbaya kwenye usahili na Ndaki ambapo CCM wilaya Tabora
mjini ilipanga uchaguzi wake mwezi julai 31 mwaka huu kabla ya
kuhairishwa ghafla.
Baadhi ya madiwani wameudokeza mtandao huu kuwa mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Tabora,Hassan Wakasuvi ameaharisha uchaguzi huo kutokana na kile
kilichodaiwa kuwa kuna mgombea mmoja alikuwa hamtaki huku akimtaka
mwingine ambaye imedaiwa kuwa ndiyo chaguo lake.
Kutokana na hilo baadhi ya madiwani wamesikika wakitamka kuwa ipo siku
CCM Tabora viongozi wake watakiingiza chama kwenye mgogoro usioisha
kwani wamekuwa wabinafsi sana kwenye chaguzi mbalimbali zinapokuja na
kwa maana hiyo wapinzani hasa CHADEMA wanaweza kupata nafasi.
Madiwani hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa wapo wagombea wana
ualakini wa vyeti vya shule hali ambayo inapingwa na baadhi madiwani
wakidai ‘wakubwa’ wanawabeba kwa maslahi yao.
Chanzo cha taarifa toka ndani ya CCM mkoa kimesema uchaguzi huo wa
naibu meya wapo viongozi wa CCM mkoa kila mtu ana mgombea wake huku
mstahiki meya wa manispaa Ghulam Remtulah akidaiwa kumbeba diwani wa
Ikomwa Musa Msamazi,lakini Ghalam amekana na kudai hataki kujiingiza
kwenye mgogoro huo.
Wakati hayo yakisemwa mwenyekiti wa CCM mkoa Hassan Wakasuvi amedaiwa
na baadhi ya madiwani kuwa anataka naibu meya wa zamani Waziri Mlenda
arejee kwenye kiti hicho na ndiyo chanzo cha uchaguzi kuarishwa hali
ambayo tayari imerejesha mgogoro wa pande mbili wa madiwani hao.
Aidha taarifa hizo zimesema kuwa CCM mkoa wa iliketi kikao kujadili
majina ya wagombea mwezi julai 24, mwaka huu ambapo pamoja na kubariki
uchaguzi ufanyike licha ya wagombea kadhaa kupewa alama ‘D’ ambayo
kimsingi haina sifa ya kuwa mgombea.
Tayari hadi sasa madiwani hayo wamesema kuwa kuna rushwa inanukia
kwenye uchagzi huo na wametishia kwenda TAKUKURU kushitaki endapo
mizengwe itaendelea ili kuuvuruga uchaguzi huo kwa maslahi ya viongozi
wachache wa CCM.
Akizungumzia shutuma dihdi yake mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Tabora,Hassan Wakasuvi alikanusha kuwa na mgombea anayemtaka na kwamba
shutuma hizo zinalenga kumchafua na kumpakazia.
“Sina mgombea ambaye nina maslahi naye wala sijapewa kiwanja wala
fedha….taratibu kadhaa kwa mujibu wa uchaguzi huo hazikukamilika ndiyo
maana tukashauri waahirishe ili kuweza kukamilisha taratibu
hizo.”aliongeza.
Wakasuvi kwa sauti ya mshangao alisema kuhusu baadhi ya wagombea wenye
walakini na vyeti vya shule mamlaka zipo zitachunguza endapo kutakuwa
na umuhimu wa kufanya hivyo lakini chama kama chama hakina mamlaka ya
kufanya hivyo kama vyeti vya wagombea vinavyoonekana kuwa ni sahihi.
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya Abdurahaman Moshi Nkonkota ameuambia
mtandao huu kuwa uchaguzi wa naibu meya uliahirishwa jumatano na
anatarajia kukutana siku ya Alhamis kupanga tarehe ya kufanya uchaguzi
huo.
TAKUKURU YAWANING`INIZA 12 MAHAKAMANI SIKONGE
.NA LUCAS RAPHAEL,SIKONGE
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU),wilayani Sikonge
mkoa wa Tabora,imesema hadi kufikia mwezi julai 31,mwaka huu
imewafikisha watu 12 mahakamani kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.
Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Sikonge,Manyama Tungaraza,alisema hayo
kwenye kikao cha baraza la madiwani wilayani humo.
Tungaraza alisema jumla ya kesi tano zimefunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Tabora mjini.
Alisema baadhi ya kesi hizo ni vyama vya msingi vya ushirika kesi 3,kilimo (PADEP)kesi 3,ujenzi kesi 2.
Alisema kesi nyingine ni jeshi la polisi kesi 1,mipango kesi 1,elimu
kesi 1 na VEO vijiji kesi 1.
Alisema kesi hizo zimekuwepo hasa kutokana na malalamiko ambayo
yamekuwa yakipokelewa na ofisi yake kutoka kwa wananchi na kufanyiwa
kazi.
Tungaraza alisema licha ya kuwepo kwa kesi hizo baada ya kupata
malalamiko toka kwa wananchi bado wameendelea na zoezi la kutoa elimu
kwa wananchi,taasisi na wanasiasa hasa baraza la madiwani kila mara.
Hata hivyo Tungaraza aliwakumbusha madiwani hao jukumu la mapambano ya
rushwa ni la viongozi wote,madiwani na watendaji wa vijiji,vitongoji
kata na kwamba kila mtu atomize wajibu wake.
Aidha licha ya taarifa hiyo,kamanda huyo alitoa mada kwa
watendaji,madiwani na wageni waalikwa akikumbusha majukumu ya
TAKUKURU,kushauri na kuchunguza shughuli za taratibu za jamii,taasisi
za umma,sekta na binafsi.
Kamanda huyo aliongeza kuwa TAKUKURU pia imekuwa ikishauri na
kuchunguza taratibu za jamii,umma,na sekta binafsi ili kuwezesha
kugundua vitendo vya rushwa,ikiwemo usambazaji wa taarifa kuhusu
athari za vitendo vya rushwa kwa umma.
WAISLAMU WAPONGEZA MAHUSIANO BAINA YAO NA WAKRISTO TABORA
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
![]() |
| Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora Sheikh Shaaban Salum akizungumza katika hadhara hiyo. |
![]() |
| Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika hafla ya Futari hiyo. |
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya TABORA mjini, Moshi Abdulrahman-Nkonkota
amekemea vitendo vya ubaguzi wa dini, ukabila na rangi katika jamii kwani
vinahatarisha amani ya nchi.
Amesema
suala la ubaguzi wa dini, ukabila na rangi halifai na halitakiwa katika jamii
kwa lengo la kuimaisha usalama na amani ya wanajamii.
Moshi
alikuwa akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya TABORA mjini, Emmanuel Mwakasaka katika ukumbi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma, tawi la TABORA.
Kwa
upande wake, Sheikh wa mkoa wa TABORA, Sheikh Shaban Salum amempongeza ,Mwakasaka
kwa ushirikiano wake na kuwa karibu na jamii ya kiislamu.
Amesema
kitendo chake cha kuwaandalia futari waislamu, kinaoneyesha jinsi alivyo na
ushirikiano wa karibu na mshikamano na jamii ya waislamu.
Naye
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya TABORA mjini, Emmanuel Mwakasaka
amesema uamuzi wake wa kufuturisha waislamu unatokana na jinsi
anavyothamini jamii hiyo bila kujali tofauti za dini wala rangi.
MAKADA WA CHADEMA WAFUTIWA KESI YA UGAIDI
Na Lucas Raphael,Tabora
MAHAKAMA kuu ya
Tanzania kanda ya Tabora jana imefuta shitaka la ugaidi lilokuwa
likiwakabili makada wa Chama cha demokrasia na mandeleo CHADEMA nakubakiza kesi
moja ya kummwagia mtu tindi kali.
Akitoa uwamuzi huo
Jaji mfawidhi wa Mahakama hiyo Simon Lukelerwa amesema kuwa ametoa maamuzi hayo
kutokana na kutokidhi sababu za kisheria zilizotolewa na upande wa mashitaka.
Jaji huyo aliieleza
mahakama hiyo kwamba kulingana na kifungu (che) cha sheria ya mwenendo wa
mashitaka ya mwaka 1985 kesi hiyo anaamuru ahamishiwe katika mahakama ya wilaya
ya Igunga.
Aidha alisema kuwa
sheria namba 245 kifungu kidogo (1) kinasema nilazima washiatakiwa
wanatakiwa katika mahakama ya sehemu ambayo wanadaiwa kutenda kosa husika.
Jaji Lukelerwa
ameamuru washitakiwa wote wapelekwe wilayani Igunga kwa ajili ya kusikilizwa
upya shauri lao na kwamba dhamana ipo wazi kwa washitakiwa iwapo watakuwa
wamekidhi matakwa ya mahakama ya wilaya hiyo ya Igunga.
Hali ya ulinzi wa
askari Polisi wakiwa na silaha nzito ilikuwa imeimarishwa mahakamani hapo
wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa katika mahakama kuu kanda ya magharibi.
Kesi hiyo ya ugaidi
ilifunguliwa mahakamani hapo mwezi juni 24 mwaka huu,baada ya washitakiwa hao
kuachiwa awali wilayani Igunga,katika kesi ya madai ya kummwagia tindikali kada
wa Chama cha mapinduzi CCM, Musa Tesha.
Watuhumiwa hao ni Evodius Justunian, (30) mkazi wa Bukoba,Osca Kaijage mkazi wa mkoa wa Shinyanga,Seif Magesa mkazi Nyasaka Mwanza,Rajabu Daniel mkazi wa Dodoma na Henry Kilewo.
Watuhumiwa hao ni Evodius Justunian, (30) mkazi wa Bukoba,Osca Kaijage mkazi wa mkoa wa Shinyanga,Seif Magesa mkazi Nyasaka Mwanza,Rajabu Daniel mkazi wa Dodoma na Henry Kilewo.
Mapema mwezi julai 8
mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Tabora,hakimu wa mahakama
hiyo Issa Ibrahim Magori alisema hana mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo na kuihilisha
kwa muda.
Wakili wa upande wa
utetezi katika kesi hiyo Peter Kibatala amewambia waandishi wa habari
kwamba,mahakama kuu imetenda haki na anaimani kubwa na mahakama hiyo.
Aidha alisema kwakuwa washitakiwa hao walikamatwa katika sehemu tofauti hivyo kesi zao zilipaswa kusikilizwa maeneo waliyokamatiwa.
Mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)











