Sunday, April 27, 2014
RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO
CCM WILAYA YA TABORA MJINI WAADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO KWA VITENDO!!!
![]() |
| Baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Tabora ambao walishiriki shughuli za ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Kitete |
![]() |
| Katibu wa siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Rashid Ramadhani au maarufu Kamanda Tolu |
Friday, April 25, 2014
MKUU WA MAJESHI AFUTWA KAZI SUDAN KUSINI
Generali James Hoth Mai amefutwa kazi na Salva Kiir ingawa Rais huyo hajatoa sababu ya hatua yake
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri
iliyotolewa na Rais kupitia kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James
Hoth Mai ataondolewa katika wadhifa wake mara moja.
Hata hivyo Rais Kirr hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali huyo.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia
imekosoa serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya
halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo.
Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri
wa mambo ya nje wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli
alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi
katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada
ya waasi kuuteka mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia
na ambao walikuwa wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na
hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata
hivyo waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar
wamekanusha madai ya UN kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio
na hatia huku vituo vya redio katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.
RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KISASA KIJIJINI MLOGANZILA

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL
wakikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa
Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa
24 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi
wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 24,
2014.

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chungh IL
wakiweka udongo kwa pamoja wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila Kilometa 25 kutoka jijini
Dar es salaam, April 2014.

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL na
viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la
ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe
Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, April 24, 2014.

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA)
Mhe John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria
uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya
Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini
Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 24, 2014.

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika sherehe za kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa
Pwani leo April 2014. 

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea nchini Mhe
Chung IL wakiwa mbele ya mchoro wa mfano wa Hospitali ya Chuo Kikuuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya
Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini
leo April 2014.

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na msanii Mrisho Mpoto baada ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo
Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila
maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa
kuliko zote nchini leo April 2014. leo April 2014. PICHA NA IKULU
UNHWA YA KOREA KUSINI KUISAIDIA NIMR KATIKA UGUNDUZI WA DAWA KWA KUTUMIA MIMEA

Na Father Kidevu Blog, Dar es Salaam
Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea ambapo kampuni hiyo itaisaidia NIMR teknolojia mpya ya kufanya ugunduzi wa dawa za binadamu kwa kutumia mimea.
Makubaliano
hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam pembezoni mwa kongamano la 28 la
kisayansi la NIMR, ambapo mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dk. Mwele
Malecela amesema hatua hiyo ni muhimu katika shughuli za utafiti wa afya
nchini na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.
Dk.
Mwele amesema teknolojia hiyo itaongeza uwezo wa kiwanda cha taasisi
cha kutengeneza dawa kwa kutumia mimea kilichopo eneo la Mabibo External
jijini Dar es salaam na kwamba itawezesha taasisi kujikita zaidi katika
utengenezaji wa dawa za saratani mbalimbali pamoja na za kusaidia
udhibiti wa virusi vya ukimwi.
Kwa
upande wake afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya NHWA bw. YOUNG WOO
JIN amesema kampuni yake imefikia hatua hiyo kutokana na mchango wa NIMR
katika masuala ya tafiti na ugunduzi wa dawa ambapo ameahidi kuendelea
kushirikiana na taasisi hiyo katika kiteknolojia
ili kuiongezea uwezo.
ili kuiongezea uwezo.
KWA MUJIBU WA JARIDA LA PEOPLE, HUYU NDIYE MWANAMKE MZURI ZAIDI DUNIANI MWAKA 2014
| Lupita Nyong'o mwanamke mrembo zaidi duniani mwaka 2014. |
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.
Jarida la People limemtaja Lupita kuwa mwanamke mrembo
Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.
Hatua ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.
Subscribe to:
Posts (Atom)



