Na Father Kidevu Blog, Dar es Salaam
Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea ambapo kampuni hiyo itaisaidia NIMR teknolojia mpya ya kufanya ugunduzi wa dawa za binadamu kwa kutumia mimea.
Makubaliano
hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam pembezoni mwa kongamano la 28 la
kisayansi la NIMR, ambapo mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dk. Mwele
Malecela amesema hatua hiyo ni muhimu katika shughuli za utafiti wa afya
nchini na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.
Dk.
Mwele amesema teknolojia hiyo itaongeza uwezo wa kiwanda cha taasisi
cha kutengeneza dawa kwa kutumia mimea kilichopo eneo la Mabibo External
jijini Dar es salaam na kwamba itawezesha taasisi kujikita zaidi katika
utengenezaji wa dawa za saratani mbalimbali pamoja na za kusaidia
udhibiti wa virusi vya ukimwi.
Kwa
upande wake afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya NHWA bw. YOUNG WOO
JIN amesema kampuni yake imefikia hatua hiyo kutokana na mchango wa NIMR
katika masuala ya tafiti na ugunduzi wa dawa ambapo ameahidi kuendelea
kushirikiana na taasisi hiyo katika kiteknolojia
ili kuiongezea uwezo.
ili kuiongezea uwezo.
No comments:
Post a Comment