Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri
iliyotolewa na Rais kupitia kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James
Hoth Mai ataondolewa katika wadhifa wake mara moja.
Hata hivyo Rais Kirr hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali huyo.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia
imekosoa serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya
halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo.
Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri
wa mambo ya nje wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli
alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi
katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada
ya waasi kuuteka mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia
na ambao walikuwa wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na
hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata
hivyo waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar
wamekanusha madai ya UN kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio
na hatia huku vituo vya redio katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.
No comments:
Post a Comment