Thursday, April 24, 2014

WATAFITI WAWASILISHA RIPOTI ZA TAFITI ZAO MKUTANO WA NIMR


 Mtafiti wa Magonjwa ya Binadamu kutoka Taasisi ya Utafiti ya  Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR), Dk. Kijakazi Mashoto akiasilisha utafiti wake juu ya Ugonjwa wa Kipindupindu alioufanya Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Kisarawe.

NIMR wameingia katika siku ya pili ya mkutano wao wa 28 wa Mwaka pamoja na Kongamano la Wanasayansi Watafiti linaloendelea jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wanasayansi Watafiti wakisikiliza ripoti hiyo ya Utafiti kutoka kwa Dk Kijakazi Mashoto wa NIMR.
 Mtafiti kutoka DUCE, Dk. Jared Bakuza akiwasilisha tafiti yake aliyoifanya juu ya hali ya ugonjwa wa Kichocho cha tumbo kwa Wilaya ya Kigoma vijijini ambapo utafiti ulibaini  80% ya waliofanyiwa utafiti ambao walikuwa watu  470 walikutwa wana maambukizi ya ugonjwa huo mabapo pia 10%  ya Nyani 150 waliofanyiwa utafiti katika Msitu wa Gombe pia wamekutwa na maambukizi ambayo kwa mujibu wa utafiti huo hakuna tofauti kati ya vimelea vilivyokutwa kwa binadamu na nyani hao.
 Wanasayansi watafiti wakifuatilia kwa makini..
  Mtafiti, Dk. Safari Kinung'h  akiwasilisha utafiti wake.
 Dk. Upendo Mwingira akiwasilisha ripoti ya utafiti wake wa magonjwa ya binadamu mbele ya watafiti wenzake hii leo.
 Mkurugenzi wa NMR, Dk. Mwele Malecela akichangia katika tafiti zilizowasilishwa.
 Mtafiti Mwandamizi kutoka Maria Stop Tanzania, Mengi Ntinginya akizungumza mara baada ya kuwasilisha tafiti yake ya utikanaji wa huduma za afya ya uzazi kwa watu wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment