Na Mwandishi wetu, Tabora
BENKI ya CRDB imetoa mikopo yenye thamani ya dola za Kimarekani mil. 42 katika mwaka wa fedha 2012/13 kwa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku vipatavyo 143 vilivyo chini ya Chama kikuu cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi, WETCU Ltd.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo cha benki
hiyo,Taitus Tumaini alisema kiasi hicho kilikopeshwa kwa Vyama hivyo vya msingi
msimu wa mwaka 2012/13 na Vyama 85 tayari vimefanikiwa kurejesha mikopo yake.
Alieleza kuwa urejeshwaji wa Mikopo
hiyo ni kiasi cha asilimia 85 wakati kiasi kilichobaki cha dola za kimarekani mil 7.4 bado zinadaiwa kwa Vyama vya Msingi.
Alisema kutokana na hali hiyo Benki
hiyo imeamua kuviongezea muda wa kulipa deni hilo Vyama vya msingi
ambavyo vimeshindwa kulipa deni kutokana na uzalishaji mdogo wa zao la tumbaku.
“Benki
imeamua kuviongezea muda
zaidi vyama vya Msingi hamsini na nane kutokana na kushindwa kulipa deni
kwa wakati hivyo watalipa deni lao katika kipindi cha Miaka Mitatu”
alisema.
Aidha aliweka bayana kuwa pamoja na Vyama
hivyo vya msingi kuongezewa muda wa kulipa deni hilo pia vimepewa mikopo
ya ziada ili wanachama wake waweze kulima tumbaku.
Tumaini aliongeza kuwa mazungumzo
yalifanyika baina ya Benki hiyo na Chama Kikuu cha ushirika wa wakulima wa
Tumbaku Kanda ya Magharibi na kukubaliana namna ya kulipa deni hilo.
Alieleza kwamba benki ya CRDB
inamjali mkulima na ndio maana inahakikisha anawezeshwa ili aweze kunufaika na
kilimo chake.
Mwenyekiti
wa bodi ya WETCU, Hassan Wakasuvi katika mkutano mkuu wa 21 wa
wakulima wa tumbaku uliofanyika hivi karibuni mjini Tabora, alivitaka
Vyama vya msingi ambavyo havijalipa madeni yake vilipe kwani
dawa ya deni ni kulipa na sio kulikimbia.
No comments:
Post a Comment