Thursday, October 25, 2012

MHE .HAMAD RASHI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA UKAGUZI WA HAESABU ZA NDANI IPU


Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akifuatilia Mjadala wa  kamati ya Chama cha Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mjini Quebec, Canada, kuhusu maswala ya umoja wa mataifa. Mada kubwa ilikuwa kuangalia kama kweli Umoja wa Mataifa unalichukulia swala la demokrasia duniani kwa dhati.Picha  na Owen Mwandumbya
 ……………………………………………………….

Mbunge wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N’Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia  kutoa taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU.
Katika hatua nyingine, Wabunge vijana wametakiwa kuwa chachu ya maendelo katika nchi zao kwa kushawishi kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa ajira kwa vijana katika kipindi hiki cha uchumi wa kitandawazi.
Hayo yamesemwa jana na Mtaalamu wa maswala ya ajira kutoka shirika la la kazi la umoja wa mataifa (ILO) alipo toa maada katika mjadala wa Wabunge Vijana kujadili na namna ya kupunguza ajira kwa vijana hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa utandawazi.
Mtaalamu huyo amesema ni wajibu wa wabunge kuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali zao na baadhi ya taaisisi zinazotoa ajira ili kuwa na sera madhubuti kwa ajira za vijana hususani wanaomaliza vyuo kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

UN YATIMIZA MIAKA 67 NA CHANGAMOTO KIBAO



Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwake.

Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaa leo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akimtambulisha Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.


Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa baada ya kutimiza miaka 67 ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meha Jenerali Raphael Muhuga wakiwa Meza kuu.
Pichani Juu na Chini ni viongozi wa Madhehebu ya Dini nchini wakiomba Dua kwa ajili ya kubariki sherehe za kutimiza miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.Mh. Sitta alifafanua katika kilele cha sherehe hizo umuhimu wa kupitia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo ya millennia.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho ya umoja huo katika viwanja vya Karimjee alisema matatizo ya njaa, kupanda kwa bei za mafuta na mtikisiko wa uchumi duniani ni kati ya changamoto kubwa ambazo Umoja wa Mataifa inakabiliana navyo katika dunia ya leo. Dtk Kacou pia aliipongeza Tanzania katika juhudi zake za kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua na watoto ili waweze kufikia malengo ya millennia itakapofika 2015.Mratibu Mkazi wa UN alisema Tanzania imepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo alisema umoja wa mataifa imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha vijana wa bara la Afrika. Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya afya ya uzazi na ugonjwa wa Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa nchini Tanzania katika harakati ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa huo na afya ya uzazi kwa vijana.

Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya miaka 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati wa gwaride la watoto wa shule ya Heritage baada ya kuonyesha mbwembwe katika kupamba sherehe hiyo.

MKUTANO MKUU WA VIJANA DODOMA,WAMPATA MWENYEKITI MPYA

 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk.Ali Mohamed
Shein,alipokuwa akizumgumza wakati akiufunga   Mkutano Mkuu wa nane wa
Jumuiya hiyo uliofanyika  Mjini Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha
Mipango,uliomchagua  Mwenyekiti Mpya wa jumuiya ya UVCCM Khamis Saifa
Juma, na Makamo Mwenyekiti wa UVCCM,Mboni Mohamed Mkita. [Picha na
Ramadhan Othman,Dodoma.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk.Ali Mohamed
Shein,alipokuwa akiagana na Mwenyekiti Mpya wa jumuiya ya UVCCM Khamis
Saifa Juma, alipomaliza shuhuli ya kuufunga   Mkutano Mkuu wa nane wa
Jumuiya hiyo uliofanyika  Mjini Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha
Mipango. [Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.
 
Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Mboni Mohamed
Mkita,akinyanyua mikono juu kwa furaha baada ya kutangazwa,baada ya
kushinda katika uchaguzi mkuu wa nane uliofanyika Mjini Dodoma katika
ukumbi wa Chuo cha mipango.[Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati) Katibu Mkuu wa CCM Taifa Willson Mkama,Naibu katibu
Mkuu CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,(kulia) wakiwapongeza Mwenyekiti Mpya
wa UVCCM Khamis Saifa Juma,(wa pili kushoto) na Makamo Mwenyekiti wa
UVCCM,Mboni Mohamed Mkita,(kushoto) baada ya kutangazwa kushika nafasi
hizo katika uchaguzi Mkuu wa Nane (8) uliomalizika jana katika ukumbi
wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.[[Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.]
 
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa UVCCM
wakishangilia baada ya kutangazwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo
Khamis Sadifa Juma,baada ya kushika nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu
uliomalizika jana katika ukumbi wa  Chuo cha Mipango Mjini Dodoma,na
kufunga na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo
pichani).[Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.]
 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa
UVCCM Taifa,wa Mikoa mbali mbali wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti

Mpya Khamis Sadifa Juma,(hayupo pichani) baada ya kutangazwa kuwa

mshindi katika mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo uliofanyika  Mjini

Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha  Mipango. [Picha na Ramadhan

Othman,Dodoma.]

BARABARA KUFUNGWA ZANZIBAR KUPISHA SHEREHE ZA EIDDI

Na Mwanshi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
 ……………………….
Jeshi la Polisi zanzibar limetangaza kuzifunga baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar ili kuwawezesha wananchi wakiwemo watoto wadogo kusherehekea siku kuu ya Eddi el Haji kwa usalama na amani.
 Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amezitaja baadhi ya barabara zitakazofungwa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa wiki hii hadi Jumatatu wiki ijayo kuwa ni ile inayotoka Mnazi Mmoja hadi Viwanja vya michezo vya Maisala, barabara ya kutoka Ofisi ya Baraza la Wawakilishi la Zamani kuelekea Viwanja vya Maisala na Barabara ya ya kutoka Ukumbi wa CCM kuelekea Mnazi Mmoja.
 Inspekta Mhina, amesema kuwa barabara hizo zitafungwa kuanzia majira ya saa 9.00 arasili hadi saa 4.30 usiku kwa kila siku muda ambao watu wengi watakuwa wamesharejea majumbani kwao baada ya kusherehekea siku hiyo.
 Awali akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Zanzibar, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Ungauja ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa sherehe hizo zitaadhimishwa kwa muda wa siku nne mfululizo zitaanza Ijumaa ya Oktoba 26 hadi Jumatatu ya Oktoba 29 2012.

KONGAMANO LA HAKI ZA WANAWAKE NA KATIBA

 
Maria Sarungi mmoja wa waandaaji wa kongamano hili , akiwasomea  majumuisho ya yote yaliyojadiliwa katika kongamano hili lililohusisha wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali nchini lilifanyika kwa siku tatu mfululizo katika hotel ya Blue Pearl,Ubungo Plaza,jijini  Dar es Salaam
Kazi na dawa na raha pia wakijipa…kuna nyimbo zao wenyewe wanaimba….wanawakee wa Tanzania!!
HII NDIO KAMATI YA UFUNDI WA KONGAMANO HILI, LILILOHUSISHA WANAHARAKATI,WAJASIRIAMALI NA WANAWAKE MBALIMBALI KUTOKA KILA SEKTA ZA MIJINI NA HATA ZILE ZILIZOKO PEMBEZONI

Mwenyekiti Mary Rusimbi akikusanya maoni ya mwisho ili kupata majumuisho wa kongamano hilo.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAZINDUA HUDUMA YA (Tigo Prepaid Internationl Roming)


Afisa masoko wa kampuni ya Tigo(kushoto)Bi. Jaequline Nnunduma  akiongea na waandishi wa habari jana kwenye Hotel ya Southen Sun jijini Dar es salaaam wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo Prepaid Internationl Roming ambapo wateja wanaotumia huduma za malipo ya kabla wataweza kuwasiliana kutumia namba zao za tigo wakiwa katika nchi za Africa mashariki kwa bei nafuu kupitia huduma ya Tigo Prepaid Internationl Roming nchi hizo ni Kenya Uganda na Rwanda katikati ni  Afisa uhusiano wa  Tigo Bi.Tuli Mwaikenda(kulia)meneja wa bidhaa za simu za kimataifa Tigo Bi. Mwajuma Mwenda
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria katika uzinduzi huo jana
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG.COM

NHC YAZINDUA RASMI UUZWAJI WA NYUMBA ZA MINDU MANISPAA YA ILALA

Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara Shirika la nyumba Tanzania Bw.David Shambwe akiongea na waandishi wa habari jana kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa mradi wa nyumba zilizoko mtaa wa Mindu mansipaa ya Ilala jijini Dar es salaam nyumba hizo ni  mahsusi kwa watu wenye kipato cha juu na kati ambapo wananchi wametakiwa kununua nyumba hizo kwa kiasi cha shilingi milioni  272, wengine katika picha katikati ni  meneja mtafiti na masoko Bw.Itandula Gambalagi,(kushoto)meneja wa shirika la nyumba mkoa wa Ilala Bw.Benedict Kilimba
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mradi huo mpya wa nyumba za Mindu ili kujionea nyumba maendeleo ya mradi  wa ujenzi wa nyumba hizo
Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara shirika la nyumba Tanzania Bw.David Shambwe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea nyumba hizo.