NA LUCAS RAPHAEL,URAMBO
SHIRIKISHO
la vyama vya watu wenye ulemavu wilayani urambo mkoani Tabora (SHIVYAWATA)
limesema kwamba rasmu ya katiba itamke wazi juu ya nafasi za uwakilishi kwa
watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya kijijji na mabaraza ya halmashauri .
Kuwepo
kwa viti vya upendeleo kwa watu wenye ulemavu katika nafasi za uwakilishi
katika mabaraza ya madiwani ili kuweza kupata mtu wakuwasemea walemavu .
Wito
huo umetolewa wakati wakuitimisha mabaraza ya katiba wilayani urambo
yaliyoanyika katika ukumbi wa Cinema Gik na kufadhiliwa na the foundation civel
socerty kwa muda wa siku tatu.
Wakichangia
juu ya rasimu ya katiba mpya Shija Nyanda alisema kwamba walemavu wanatakiwa
wapata mwakilishi wao katika sehemu za maamuazi hasa kwenye ngazi wa udiwani
ili wapate mtu wakusemea watu wenye ulemavu.
Alisema
kwamba uwakilishi huo upate nafasi tatu za uwakilishi kwa kila baraza la
madiwani hivyo itakuwa nafasi mzuri kwa watu wenye ulemavu kupata mtu wa
kuwesemea walemavu hao ndani na je ya mabaraza hayo
.
Wakati
huo huo chama cha walemavu wa ngozi (TAS)wilayani urambo wamependekeza kuwepo
na baraza moja la mitiani la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kuwepo na
kiwango sawa cha elimu, bara na visiwani.
Kauli
hiyo ilitolewa wakati wakuitimisha mabarza ya katiba kwa asasi na makundi
ya watu wenye malengo yanayofanana iliyofanyika katika ukumbi wa Victoria
wilayani humo.
Akichangia
mjadala huo wa rasimu ya katiba mpya Mikael Emamnuel alisema kwamba kuwepo kwa
baraza moja la mitiahani kutasaidia sana kuwepo kwa kiwango cha elimu kilicho
sawa tofauti na sasa .
Alisema
kwamba licha ya kuwa na elimu iliyosawa pia mfumo wa elimu nao utakuwa sawa kwa
upande zote za nchi hii.
Aidha
alisema kwamba swala hilo litapunguza wimbi la wizi wa mitihani na hivyo
uthibiti utakuwepo kutosha kwa kila sehemu kulinda kwa
umakini mkubwa .
No comments:
Post a Comment