Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiwasisitizia wahitimu na
wageni (hawako pichani) waliofika katika mahafali ya kwanza na ya pili
ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora kuwa serikali lazima ijenge Chuo
KIkubwa Cha Ufugaji Nyuki Tabora.
|
Ahadi hiyo imetolewa mwishoni
mwa wiki na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda aliyekuwa Mgeni Rasmi katika
mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora
alipokuwa akiwahutubia wahitimu kabla ya kuwatunuku vyeti na zawadi.
Mhe.
Pinda alisema pamoja na mapungufu ya chuo hicho yaliyotokana na tabia ya kuhamisha
mafunzo yake mara kwa mara kwenda kwenye vyuo mbalimbali vya Wizara ya
Maliasili na utalii nchini, chuo kina umuhimu mkubwa kutokana na kuwa ni chuo
pekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
“Siku za
nyuma chuo kiliweza kupata watu kutoka nchi za nje kuja kujifunza, hivyo
serikali haiwezi kukiacha solemba! Kama tumeweza kujenga Chuo kikubwa cha
Serikali za Mitaa, Hombolo kinachotufanya tushindwe kujenga chuo kikubwa hivi ni nini? Kwamba hatuoni thamani
yake? Si kweli, miaka kumi ijayo thamani yake itaonekana tu,” alisema Mhe.
Waziri Mkuu.
Aliongeza
kuwa, tatizo la kutoendelezwa kwa chuo hicho wakati mwingine kunatokana na
viongozi kutojua kinachoendelea, hivyo aliomba uongozi kuwakilisha mpango
mkakati wake ili serikali iweze kuipembua na kuona wapi pakuanzia.
Aidha,
Mhe. Pinda aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uamuzi wake wa
kukirudisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora na kutoa onyo kwa
yoyote atakayetaka kujaribu kukihamisha tena kutofanya hivyo ili serikali iweze
kujipanga na kusonga mbele.
Aliongeza
kuwa, Tanzania ina hifadhi za misitu na maji ya kutosha inayotoa fursa ya
kuzalisha asali nyingi, hivyo amewaasa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili
kuiwezesha nchi kushika namba moja kwa nchi za Bara la Afrika zinazozalisha
asali.
“Tanzania
hivi sasa inapitwa na Ethopia kwa uzalishaji asali, nchi ambayo haina misitu
yakutosha, hili haliwezekani tuangalie mpango mikakati yetu. Ufugaji asali
hauhitaji mtaji mkubwa, na soko lake ni la uhakika, tumshinde Ethiopia na hili
linawezekana kama tutapanua mawazo yetu juu ya sekta hii,” alisema Mhe. Pinda.
Kwa
upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki,
alimshukuru Waziri Mkuu kwa moyo wake wakusimamia kidete sekta ya ufugaji nyuki
nchini na kutoa fursa za ajira kwa wananchi wengi.
Aidha,
Mhe. Pinda alisisitiza kiu yake ya kuona Tanzania inazalisa asali nyingi kwa
kuwaahidi wahitimu kuwapa zawadi ya mizinga 100 endapo wataunga na kuunda
kikundi cha ufugaji nyuki na kutumia elimu waliopata kuweza kujipatia kipato.
Katika kusisitiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bi. Fatma Mwasa naye aliwahidi wahitimu ambao ni wakazi wa mkoa wake, kuunda vikundi vya watu waiopungua kumi kwa kikundi ili aweze kuwapatia mtaji wa mizinga.
No comments:
Post a Comment