Na
Hastin Liumba,Sikonge.
MBUNGE
wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora,Said Nkumba anasikitishwa na kusononeka
kutokana na baadhi ya viongozi wenzake kukaa kimya na kushindwa kupiga kelele
wakulima wa nchi hii wanavyoibiwa.
Nkumba
alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya
kupokewa kwa maandamano na wananchi wa jimbo lake siku chache zilizopita,maandamano
yaliyoanzia kata ya Pangale hadi Sikonge mjini hadi nyumbani kwake.
Alisema
kutokana na kauli yake bungeni ya kutaka mswada wa sheria za ushirika usainiwe
na rais Dkt Jakaya Kikwete,na kutaka
Apex ifutwe kutokana na kukosa msaada, uzalendo wa kweli kwa wakulima nchini
hususani wa zao la tumbaku ndicho kiini cha wananchi wa jimbo lake kumlaki kwa
maandamano.
Alisema
umefika wakati sasa kwa viongozi wenye dhamana kujipanga upya ili kuweza
kusaidia wakulima wa nchi hii ili wasibaki kama yatima kwenye haki zao za
msingi kwani taarifa za sasa zinaonyesha wakulima wengi hawajitambui katika
uwezo wao wa kuendesha ushirika.
“Wanaushirika
wote ndiyo wenye nguzo za kuendesha ushirika na ifikie mahali viongozi wote wasio
waaminifu na wezi kuondolewa mara moja na hii ni njia mbadala ya kumkomboa
mkulima kwani kupewa madaraka isiwe sehemu ya kujitajirisha.”alisema Nkumba.
Alisema
mkulima angefikia mahali pazuri endapo kungekuwa na maamuzi ya kuwajibishana na
itakuwa haina maana kuwa na vyombo vya ushirika vinavyoendelea kukaa kimya
wakati wizi,dhuluma dhidi ya wakulima inaendelea.
Nkumba
alisema ana imani kubwa kwa rais Dkt Jakaya Kikwete atausaini mswada ule…..na hiyo
itakuwa ni ishara tosha sasa mkulima wa nchi hii anakombolewa cha msingi tu
kuwepo na utekelezaji wa maamuzi waliyopewa baadhi ya viongozi.
Hata
hivyo siku chache baada ya mswada huo kupitishwa na kutaka kufutwa kwa Apex
wameibuka baadhi ya viongozi wanaolalamika na kuitisha vyombo vya habari kutaka
rais Dkt Jakaya Kikwete kutosaini mswada huo.
“Haya
yanayolalamikiwa na wale wanaotaka rais asisaini ule mswada inaonyesha kuna maslahi
yao hapa kwa hawa wanaojiita wanaushirika……napata mashaka sana na hawa watu na
hapa jamii inawaona hawajui mbona hawalalamiki mkulima kubeba mzigo mzito kwa
muda mrefu lakini hawakuitisha vyombo vya habari kulalama.”alisema.
Alisema
kamwe hataacha kupiga kelele kumsaidia mkulima hasa wa zao la tumbaku na sasa
moto kauwasha hatauzima na hakuna atayemziba mdomo.
Mbunge
huyo anasema anawashukuru wakulima na wananchi kwa ujumla kwani toka ametoka
bungeni amekuwa akipokea simu nyingi za pongezi toka wananchi wa baadhi ya
mikoa na kumtaka aendelee na mapambano katika kumkomboa mkulima wa nchi hii.
Alisema
wao kama wabunge hawana mipaka ya kutetea wananchi zaidi ni kutetea makundi
yote ya jamii hivyo mtu mwenye kuona kuna mipaka basi huyo ni sehemu ya wale wanaotaka
mkulima aendelee kubeba mzigo mzito hasa wa madeni makubwa na wizi.
No comments:
Post a Comment