Na Mwandishi wetu Tabora.
Baadhi ya watumishi wa Serikali waliojiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tabora wamelalamikia kutopata kwa uhakika huduma za afya licha ya kuwa wamekuwa wakichangia kwa viwango tofauti tofauti.
Akizungumza na mtandao huu mmoja kati ya watumishi hao wa Serikali ambaye hakutaka jina lake litajwe,alisema amekuwa akichangia kiasi cha shilingi 52,000 tangu mwaka 2002 lakini cha kushangaza amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya macho tangu Julai 2013 na hivyo kutakiwa kupata miwani yenye thamani ya shilingi 20,000/= lakini hadi sasa amekuwa akisumbuliwa na kupigwa dana dana.
Hata hivyo mtumishi huyo ambaye anashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na kukosa huduma ya kupata miwani hiyo,amebaisha kuwa tayari alikwisha jaza fomu za maombi kutoka katika mfuko huo wa huduma ya afya hapa mjini Tabora tangu mwezi Julai na kupata maelekezo ya kupatiwa huduma hiyo katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako amedai kuwa kumekuwa na ubabaishaji usiokuwa wa lazima na kuleta usumbufu mkubwa kwa wateja wa mfuko huo wa huduma za Afya mkoani Tabora.
Aidha kwa upande mwingine baadhi ya wanachama wa mfuko huo wamekuwa wakifika katika hospitali na vituo vya afya wamejikuta wakipata usumbufu mkubwa wa kutothaminiwa hatua ambayo imezidi kuwasononesha na kuona kuwa mfuko huo hauna manufaa kwao wakati wanapokuwa na matatizo ya magonjwa.
Mtandao huu unafanya juhudi za kuwasiliana na uongozi wa Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya ili kujiridhisha kuhusisna na kadhia hiyo ambayo kwasasa ni kero kubwa kwa wanachama wa mfuko huo.

No comments:
Post a Comment