Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mpango mkakati huo mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi |
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimkabidhi mpango mkakati huo unaolenga kuimarisha afya za akinamama wajawazito na watoto wachanga na kupunguza vifo. |
Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewji akipokea mpango mkakati huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tabora kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila. |
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akifungua mkutano wa uzinduzi wa mpango mkakati huo wa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga. |
Baadhi ya wadau wa Afya kutoka sekta mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kupunguza vifo vya watoto wachanga na kinamama wajawazito. |
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila ameonya vikali waganga wakuu
wa wilaya na waratibu wa huduma ya Afya ya mama na mtoto wanaoshindwa
kutekeleza wajibu wao ipasavyo hali inayosababisha kuendelea kuongezeka kwa
vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga mkoani humo.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo hilo katika mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto uliofanyika jana katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya kutoka wilaya zote za mkoa huo, taasisi, mashirika na waandishi wa habari.
Alisema takwimu za idadi ya akinamama wajawazito na watoto wanaofariki kwa kukosa huduma au kutohudumiwa kwa wakati inazidi kuongezeka mkoani Tabora na vifo vingine vinavyotokea hata wataalamu wa afya hawana taarifa, jambo hili sio zuri, lingeweza kuthibitiwa na watoa huduma katika vituo vya afya.
Alisema hakuna sababu ya mama mjamzito kupoteza maisha anapojifungua au mtoto wake kufariki kisa amekosa huduma wakati uwezekano wa kujifungua salama upo, rasilimali chache zilizopo zinaweza kutumika kuokoa maisha ya mama na mtoto wake kama watoa huduma watafanya kazi yao ipasavyo.
‘Kuanzia leo waganga wakuu wa wilaya (DMO’s) ni lazima mtoe taarifa za kifo chochote cha mama mjamzito kitakachotokea katika kituo chako na utoe sababu kwa nini kimetokea ili mhusika aliyezembea achukuliwe hatua mara moja’, alisema.
Mwananzila aliwapongeza madaktari wote wanaotoa huduma za uzazi katika mradi wa Millenium ulioko katika vijiji 16 mkoani humo ambapo taarifa za utendaji zinaonyesha kwamba katika kipindi cha mwakamzima hakuna kifo hata kimoja cha mama mjamzito kilichotokea katika vijiji hivyo.
‘Nawapongeza madakatri na watoa huduma wote walioko katika mradi huu, mmekuwa mfano wa kuigwa,wataalamu wa afya katika kila halmashauri acheni kufanya kazi kwa mazoea, tumieni rasilimali zilizopo ipasavyo, alionya Mwananzila .

Mkuu
wa mkoa aliwataka wakurunguzi , wakuu wa wilaya , waganga wa wilaya , waratibu
wa afya ya uzazi, makatibu Tawala wa wilaya na ,madiwani, watendaji,
madaktari na wauguzi wote kusimamia zoezi hiloipasavyo katika maeneo yao ili
kuepusha vifo vyote vitokanavyo na uzazi.
Aidha aliagiza halmashauri zote kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea wataalamu wapya wa afya na kada nyinginezo wanaopelekwa katika halmashauri hizo ili wafurahie mazingira ya kazi na waweze kuwa msaada mkubwa katika maeneo hayo.
Kuondoka kwa wataalamu wengi katika halmashauri nyingi kunachangiwa na halmashauri zenyewe kutoandaa mazingira mazuri ya kuwapokea wataalamu wapya wanaoletwa na serikali.
Akitoa neno la shukrani Mratibu wa Huduma ya Uzazi kwa mama na mtoto Kanda ya Magharibi . Martha Mlimba aliwataka waganga wakuu, waratibu wa afya na watoa huduma ya uzazi kwa mama na mtoto katika kila halmashauri kuzingatia agizo la RC katika utendaji kazi wao ili kupunguza vifo hivyo.

mwisho