NA LUCAS RAPHAEL NZEGA
MKUU wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora
Bituni Msangi amsema huduma ya maji vijijini imeboreshwa kwa kiasi
kikubwa hadi hadi kufikia asilimia 40% kutoka asilimia 36%
mwaka 2005.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana
Ofisini kwake alisema huduma hiyo ya maji safi na salama imepatikana kwa
kuchimba visima virefu vya maji pamoja na visima vifupi ambavyo vimechimbwa
katika kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Alisema kuwa hapo awari wananchi waishio vijijini
walikuwa wakipata shida kubwa ya maji kutokana na uhaba wa vyanzo vya
maji nakuongeza kuwa vijiji vilivyo bahatika kupata visima hivyo vya maji
vitumie kwa uangalifu miradi hiyo .
Msangi alisema kuwa Richa ya kuwa na 40% ya
upatikanaji wa maji safi vijijini bado kuna uhaba wa maji kwa baadhi ya vijiji
ambapo serikali imejipanga kukabiliana na tatizo hilo ilikuhakikisha wananchi
wanapata maji kwa asilimia 100% hasa kwa kukamilika mradi mkubwa wa maji kutoka
ziwa Victoria hadi Tabora.
Alibanisha kuwa katika miradi hiyo visima vilivyo
chimbwa mwaka 2005 vilikuwa visima 472 ambapo mwaka 2012 visima hivyo vimefikia
idadi ya 538 kati ya hivyo visima virefu ni 203 huku visima vifupi vikiwa 335.
Amewataka wananchi wananchi wa wilaya ya Nzega
kutuma visima hivyo kwa uangalifu ili kuepuka adha ya maji kwa musimu wa
masika.
Alisema serikali wialayani hapa imeweka sheria
ndogo za kuhakikisha utunzaji wa vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na
kuhakikisha wananchi wanapata Elimu ya maji safi na salama ili kila mwananchi
apate kuelewa ikiwa na kutunza vyanzo vya maji.
Msangi alisema kuwa upatikanaji wa maji mjini ni
kwa asilimia 59% kwa mwaka 2005 ambapo mwaka 2012 upatikanaji wa mjini ulikuwa
61% huku upatikanaji huo wa maji kwa ukiwa ni 40% kwa mwaka 2012 wakati mwaka
2005 ulikuwa 36%.
Mwisho.