Friday, July 26, 2013

RC FATMA MWASSA AKEMEA RUSHWA SIKUKUU YA MASHUJAA TABORA


Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa,kulia ni mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya na kamanda wa Polisi wilaya ya Tabora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika kimkoa kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Uamuzi wa Busara manispaa ya Tabora.

Silaha za Jadi zilizowekwa na viongozi akiwemo mkuu wa mkoa wa Tabora kuzunguuka Mnara wa Uamuzi wa Busara  ikiwa ni hatua ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho hayo wakionesha ukakamavu wa hali ya juu.
Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hapa mkoani Tabora zilikuwa hivi.

Wednesday, July 24, 2013

MWENGE WA UHURU WAWASILI TABORA KWA NDEGE KUTOKA RUKWA

MKUU WA MKOA WA TABORA AKIKABIDHI MKIMBIZA KWENGE WA UHUU KWA AJILI YA KUANZA MBIO HIZOM KATIKA MKOA WA TABORA BAADA YA KUPOKEA KUTOKA MKOA WA RUKWA
MKUU WA MKOA WA TABORA FATMA MWASSA AKIWA KATIKA VAZI LA SCAUT AKISOMA TAARIFA YA MWENGE YA MKOA MARA BAADA YA KUUPOKEA MWENGE HUO KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA RUKWA .
MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MKOA WA RUKWA MUSA MOSHI CHANG'A AKIWA NA AFISA MIRADI WA ASASI ISIYOKUWA YA KIRESKALI YA TDFT DEO KAHUMBI KATIKA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG STELLA MAYANYA AKIMKABITHI MWENGE WA UHURU MKUU WA WA TABORA FATMA MWASSA KATIKA MAPOKEZI YALIYOFANYIKA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA TABORA


VIONGOZI WA NKOA WA RUKWA WAKIWASILI KATIKA UWANJA WANDEGE WA  TABORA WAKIULETA MWENGE WA UHURU


Na Lucas Raphael,Tabora

Mkoa wa tabora jana uliupokea mwenge wa uhuru kutoka mkoa wa Rukwa ukiongozwa na mkuu wa mkoa huo Eng Sttela mayanya na kupokewa na mkuu wa mkoa wa tabora , Fatma Mwasaa katika uwanja wa ndege wa Tabora .


Mwenge huo katika mkoa wa tabora utakangua miradi mbalimbali ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 10.4 katika sekta za Afya ,Elimu,maji,barabara na vikundi vya ushirika.

MAOFISA WA TATU WA KAMPUNI YA CCCC WAFIKISHWA MAHAKAMANI

WACHINA WAKITIKA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI WILAYA YA NZEGA KUJIBU MASHTAKA YA KUPIGA NA KUJERUHI WAFANYAKAZI WAO
 
 
RAIA WA WAKICHINA WAKISHUKA KWEYE MAGARI YAO KATIKA VIWANJWA VYA MAHAKANAI WILAYA YA NZEGA MKOANI TABORA


NA LUCAS RAPHAEL NZEGA

MAOFISA wa Tatu wa kampuni ya Chanines  Communication and Construction Campany(CCCC) inayohusika na ujenzi wa barabara kutoka nzega hadi Tabora, wenye athiri ya bara la Asia wamefikishwa katika mahakama ya Hakim mkazi wilaya ya Nzega kwa tuhuma za kuwapiga walinzi watatu na kuwajeruhi vibaya.

Mapema jana katika mahakama hiyo waendesha mashitaka wa Jeshi la polis wilaya wakiongozwa na Inspector Fadhili mpimbwe wameiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa watatu wa kampuni ya CCCC wanatuhumiwa kwa makosa ya kupiga na kujeruhi.

Mpimbwe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Afisa Utawala wa kampuni hiyo Long Quan(28) mkazi wa Itilo raia wa china, Fundi wa magari Wang Dong Liang(35)mkazi wa Itilo raia wa china Pamoja na Afisa  Usalama Zhang Han Pang(37) mkazi wa itilo raia wa china.

Mwendesha mashita aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakim mkazi Slvester Kainda kuwa manamo July 21 mwaka huu majira saa saba usiku katika kijiji cha Mwanhala watuhumiwa hao waliwapiga na kuwajeruhi vibaya walinzi watatu wa kampuni hiyo ya ujezni ya CCCC na kuongeza kuwa upelelezi bado unaendelea.

Mpimbwe aliwataja walinzi hao waliopigwa na maofisa wa kampuni hiyo kuwa ni Juma sira,Martin Marco pamoja na Samweli Kuli wote wakiwa wafanya kazi wa kampuni hiyo ya ujenzi katika Idara ya ulinzi,ambapo majeruhi wawili wamelazwa katika Hosptal ya wilaya ya Nzega huku majeruhi mmoja akiwa amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya Nkinga wilayani Igunga.

Watuhumiwa hao wamekana kuhusika na tuhuma hizo za kuwa piga na kujeruhi walinzi wa kampuni hiyo.

Mahakama hiyo imetoa uhuru wa dhamana kwa watuhumiwa hao huku ikitoa masharti matatu ya kuzingatia katika dhamana hiyo kuwa ni kila mtuhumiwa kupata mtu mmoja na pesa Tsh,1,000,000, kuwasilisha hati za kusafiria zote pamoja na kutosafiri nje ya wilaya ya Nzega mpaka kibali maalum cha mahakama.

Mahakama hiyo imeahilisha shauri hilo hadi mwezi july 30 mwaka huu itakapo anza kusikilizwa.


Aidha Baadhi ya wananchi waliokuwa nje ya mahakama hiyo wameilalamikia kampuni hiyo ya ujenzi CCCC kutoka China kwa kuwapiga wafanya kazi wake mara kwa mara pamoja na kutokuwa na mahusiano bora na wananchi.

Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Mwanhala aliyejitambulisha kwa Juma hamis Selemani ameiomba serikali iingilie kati kuhakikisha mahusiano bora ya wananchi na wakandarasi hao yanaongezeka.

Mwisho.



MAKAMANDA WA CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA


Makamanda wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya Ugaidi wakiingizwa Mahakama kuu  Tanzania kanda ya Tabora  kwa mara ya kwanza,aliyevaa  gwanda nyeusi ni kiongozi wao ambaye ni kaimu katibu wa Chadema mkoa wa Dar-es-salaam Bw.Henry Kilewo.

 Joyce Kiria mke wa Bw.Kilewo akiwa na baadhi ya makamanda wa Chadema ndani ya ukumbi wa Mahakama kuu kanda ya Tabora wakisubiri kuanza kwa mahakama hiyo.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo makamanda walipakizwa ndani ya gari tayari kwa kurejeshwa mahabusu Gereza la Uyui mkoa wa Tabora.

NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora imeahirisha usikilizwaji wa shauri la jinai linalowakabili wanachama watao wa Chama cha Demokrasia na Maendelo – CHADEMA – hadi tarehe 30 mwezi huu baada ya kutokea ubishani hoja za kisheria kati ya wakili wa serikali na wa utetezi.

Uamzi huo umefikiwa na jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Simon Lukelewa mara baada ya kukubaliana na maombi ya wakili wa serikali Juma Masanja kwamba walichelewa kupata nakala ya maombi yaliyowasilishwa mahakama kuu na wakili wa washitakiwa.

Katika maombi yake wakili wa serikali aliiambia mahakama hiyo kuwa wao walipokea nyaraka hizo tarehe 19/07/2013  hivyo haikuwa rahisi kuweza kuzijibu na pia  aliomba wapewe nakala za mashauri mawili yaliyofunguliwa katika mahakama za wilaya ya Igunga na ile ya hakimu mkazi wa mkoa  dhidi ya wanachama hao wa Chadema.

Wakili Masanja aliiomba mahakama hiyo isiendelee kusikiliza rufaa hiyo  ya mombi ya marejeo namba 53/2013 na iwape mda ili waweze kujibu hoja zilizo wasilishwa na upande wa utetezi .

Katika maombi yao yaliyowasilishwa na wakili Peter Kibatala waliiomba mahakama kuu ipitie  majalada ya kesi hizo mbili  na hiyatolee maamuzi kwani inaonekana wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Wakili Kibatala ameainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwemo kupata dhamana.

Akitoa maamuzi ya hoja za mawakili hao aliutaka upande wa serikali uwe umejibu hoja hizo kabla ya tarehe 29/07/2013 ili ifikapo julai 30 aweze kutoa maamuzi  na kupanga tarehe ya kuanza usikilizwaji wa shauri la maombi ya marejeo lililowasilishwa na wakili Kibatala.

Watuhumiwa hao watano akiwemo kaimu katibu  wa chama hicho mkoa wa Dare salaam Henry John  Kileo wanakabiliwa na mashitaka mawili  kuwa tarehe 09-09-2011 walimjeruhi bwana Mussa Tesha  kwa kutumia tindikali na pia kutenda vitendo vya kigaidi chini ya kifungu cha nne cha sheria.

Wanachama wengine wa CHADEMA wanaokabiliwa na mashitaka hayo mawili ni pamoja na Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta n Rajab Kihawa.

Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa washtakiwa hao,Peter Kibatala,alisema amefurahishwa na maamuzi yaliyotolewa na jaji kwa kuonyesha kutenda haki kama ambavyo walivyotarajia kupata toka Mahakam hiyo ya juu.

Kwa upande wake Mke wa mshtakiwa Henry Kilewo, Joyce Kiria,ambaye alifika mahakamani hapo kufuatilia kesi ya mumewe aliwasisitiza wanawake wenzake kuwa wavumilivu wakati ambapo famiria zao zinapokuwa katika misuko suko ya kimaisha.

Alisema yupo naye katika kipindi hiki na bado anampenda na kuwatia moyo wanawake kuwa begakwa bega  na waume zao pale wanapokumbwa na matatizo.

Shauri hilo lilivutia umati wa wapenzi wa CHADEMA waliojitokeza kwa wingi huku ulinzi ukiwa mkali ambapo Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia walitanda wakiwa na silaha.
 

Monday, July 22, 2013

WAASI WA M23 WAKIHENYESHWA NA JESHI LA KONGO |FARDC

 

WAKATI mapigano yakizidi kuwa makali kati ya wanajeshi wa DR Congo (FARDC) na kundi la waasi wa M23, wanajeshi wa DRC wako hatarani kushitakiwa kwa tuhuma za kuwatesa waasi na kunajisi maiti zao.
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kosa la kukiuka haki za binadamu na sheria za Umoja wa Matifa (UN) inayokataza ukiukwaji wa haki za binadamu huku ukikataza watuhumiwa na mateka wa kivita kufanyiwa vitendo vyovyote vinavyo ashiria kukiuka haki zabinadamu badala yake mateka wote wanatakiwa kushtakiwa kwa muujibu wa sheria.
Maiti ya muasi wa M23 ikinajisiwa na Askari wa Congo,baada ya kukamatwa, kuteswa hadi kufa katika mapigakano yanayoendelea maeneo ya Kivu na Goma nchini Congo.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon alisema kwamba, Umoja huo umeonyesha wasiwasi kuhusu taarifa ya kutokutendewa haki kwa wafungwa wa M23 na kunajisiwa kwa maiti ya wapiganaji wa M23 baada ya kukamatwa na vikosi vya silaha.
Alisema watuhumiwa wa M23 walifanyiwa vitendo vibaya na askari wa DRC mbele ya raia bila ya kuzingatia Sera ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu na kwamba watuhumiwa waliohusika katika matukio hayo watafanyiwa uchunguzi wa kina.
Wanajeshi wa DRC wakiinajisi maiiti ya muasi wa M23 baada ya kukamatwa na kupigwa hadi kufa mbele ya raia
Wanajeshi wa DRC wakiendeleza mateso makali kwa waasi wa kundi la M23 mpaka kifo kinapowafika wakiwa uraiani
Wanajeshi wa DRC wakiwa wamemfunga mpiganaji wa kundi la M23 nyuma ya gari na kumpitisha mitaani.
Wanajeshi wa Congo wakimfunga askari wa kundi la M23 mbele ya raia baada ya kukamatwa
Wanajeshi wa DRC wakimtembeza muasi wa kundi la M23 mitaani baada ya kukamatwa.

JENGO JIPYA LA BENKI YA CRBD TAWI LA TABORA


Hili ndio Jengo Jipya la CRDB Tabora

MWAKASAKA,WAZAMBI WATEULIWA KUWA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA WILAYA CCM TABORA MJINI


Mlezi wa Chipukizi mkoa wa Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka

NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

Chama  cha mapinduzi  wilaya ya  Tabora  mjini  kimeamua kukata mzizi wa fitna baada  ya  kuwateua  wanachama  wawili  Emmanuel  Mwakasaka  na Nassor Wazambi kuwa  wajumbe wa halmashauri kuu  ya  wilaya  hatua  ambayo  imezua  gumzo  na  kupengezwa  na  wanachama waliowengi kwa uamuzi huo wa busara.

Hatua hiyo  imekuja siku chache baada ya Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Rage kusikika amemshitaki makao makuu ya CCM Taifa mjumbe wa kamati ya fedha na kamanda wa vijana Chipukizi Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka kuwa amekuwa akijipitisha kwa wananchi jimboni humo kwa lengo la kutaka kugombea Ubunge  ifikapo mwaka 2015 jambo ambalo limebainika kuwa ni majungu wanayotengenezewa watu wenye nia ya kukisaidia Chama hicho.

Habari alizozinasa mdodosaji wetu kutoka ndani ya Chama hicho,zinasema kuwa katika kikao cha halmashauri kuu ya wilaya ya CCM Tabora mjini kilichoketi  leo  tarehe  20 Julai 2013 kujadili masuala mbalimbali ya Chama hicho katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini  Bw. Moshi Nkokota kabla ya kukifunga kikao hicho alitangaza rasmi kuwateua wajumbe wawili ambao wataziba nafasi ngazi ya halmashauri kuu ya wilaya hiyo ambapo alimtaja Nassor Wazambi na Emmanuel Mwakasaka kuwa ni wajumbe halali kufuatia katiba ya Chama hicho inayompatia fursa Mwenyekiti ya kuwateua.

Bw.Nkonkota alianza kwa kusema amekuwa anashangazwa na tabia ya baadhi ya watu wanaokuwa wanazorotesha juhudi za wengine wenye nia ya kukisaidia chama hicho ambacho kwa sasa kimeingia kwenye wimbi la kukabiliana na vyama vya upinzani na hivyo kutoa onyo kali  kwa yeyote mwenye tabia ya kuanzisha majungu ya kuvunja nguvu za wengine eti kwa kigezo cha kuwatishia kuwashitaki makao makuu ya CCM ngazi ya Taifa. 

Alisema milango ipo wazi kwa kada yeyote wa CCM kuonesha uwezo wake katika kukisaidia Chama na kwamba hatachukuliwa kama mtu aliyeanza kampeni mapema huku akiweka wazi kuwa CCM itaendelea kuthamini michango ya mwanachama yeyote mwenye nia nzuri kwa Chama hicho.

Akizungumzia juhudi anazozionesha Bw.Mwakasaka ambaye ni kada wa CCM anayeaminika kwa wanachama wa kawaida na viongozi kwa ujumla,Nkonkota alisema Kada huyo amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mambo mbalimbali na kwamba anashiriki mikutano mingi ya hadhara na kuwa na uwezo mzuri wa kujibu hoja za wananchi katika kuitetea serikali iliyoko madarakani kwa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM bila kutafuna maneno.

Alisema  Mwakasaka kwa ushahidi wa waziwazi ameweza kuwarejesha wanachama wa CCM waliokimbilia vyama vya upinzani kama Chadema na Cuf kupitia mikutano ya hadhara  na hivyo kuendelea kukipa nguvu CCM ambayo ilianza kusemwa vibaya  na  wananchi kupitia mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Aden Rage kwa kile kinachodaiwa kuwa kutokuwa karibu na wananchi kwa kutofanya mikutano ya mara kwa mara kama wafanyavyo wabunge kwenye majimbo mengine.  

Kuhusu Nassor Wazambi ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Tabora  naye anatambulika kwa mchango wake katika kuwaunganisha vijana hatua  ambayo imekuwa endelevu na kuenziwa na Mwenyekiti wa UVCCM wa sasa ambaye ni Bw.Lucas Masanja.

Mara baada ya Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya ya Tabora  Bw.Nkonkota  kuwatangaza wajumbe hao wawili Mwakasaka na Wazambi,baadhi wa wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo waliibuka  na kelele za shangwe huku wakiinua viti juu juu wakiashiria kupongeza uamuzi wa busara wa mwenyekiti huyo.

Aidha kwa upande mwingine hata kabla ya uteuzi huo wa wajumbe hao wa halmashauri kuu ya wilaya ya Tabora  Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Aden Rage amekuwa katika wakati mgumu ndani na nje ya CCM wilaya ya Tabora mjini kwa kile kinachodaiwa kuwa kutokuwa karibu na baadhi ya viongozi na wanachama tangu kuchaguliwa kwake kushika wadhifa huo katika uchaguzi wa mwaka 2010,jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa hata na baadhi ya wananchi wa kawaida  ambao kimsingi ndio wapigakura waliomuweka madarakani kupitia Chama hicho.

Hata hivyo  mtihani mkubwa umebaki kwa Rage ambao macho ya wengi yanaangazia kuona kama ataweza kuonesha ushirikiano kwa wajumbe hao wawili wa halmashauri kuu ya wilaya  na hasa kwa mjumbe mmoja ambaye tayari amekwisha fikisha malalamiko dhidi yake CCM ngazi ya Taifa kwamba ameanza kampeni mapema hatua ambayo imejionesha kuwa Rage anahofia nafasi yake ya Ubunge katika uchaguzi ujao bila kujali nafasi hiyo ya Ubunge mara nyingi kwa jimbo la Tabora mjini hutumikiwa kwa awamu moja tu.


WAISLAMU TABORA WAIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA KUWA KARIBU NA WANANCHI





NA LUCAS RAPHAEL,TABORA


Sheikh wa mkoa wa Tabora Shaaban Salum akichukua futari  wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Benk ya CRDB tawi la Tabora ikiwa ni hatua ya kuwa karibu na wananchi wakiwemo wateja wa Benk hiyo.
Hawa ni baadhi ya kinamama wa kiislamu waliojumuika pamoja na wafanyakazi wa CRDB katika hafla hiyo mahususi.
Ilikuwa ni faraja kwa waislamu na wasiowaislamu waliokaribisha na CRDB katika Futari
Baadhi ya waislamu na viongozi wa vyama vya siasa nao walihudhuria.
Viongozi wa dini wakiwa katika meza kuu ya hafla hiyo ya Futari.
Wageni  na wafanyabiashara mjini Tabora nao walihudhuria
Maafisa wa CRDB wakizungumza na msemaji wa waislamu katika hafla hiyo ya Futari.



BENKI ya CRDB imetoa futari kwa waumini wa dini ya kiislamu na wasio waumini wa dini hiyo katika kuwaweka watu wa tofauti pamoja.

Akizungumz akwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo dk charlei kimei,meneja wa mkoa,sydney bakari alisema wameamua kufanya hivyo katika kutimiza wajibu wao kwa jamii

Dk.Kimei aliongeza kuwa Benki yake itaendelea kufanya shughuli za kijamii kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali kusaidia watoto yatima,walemavu,wagonjwa na waliopatwa na majanga mbambali,wakiamini Benki hiyo inatokana na jamii.

Aliongeza kwamba CRDB itaendelea na utaratibu wake wa kutenga sehemu ya faida yake ili kusaidia jamii ambayo ni moja ya sera zake.

katika kujitanua na kuwasogelea wateja wao,itafungua matawi katika wilaya za Urambo na sikonge kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Alisema hata Manispaa ya Tabora pia wameboresha huduma kwa kufungua jengo jipya ambalo ni kubwa na la kisasa na huduma zake ni bora zaidi kuliko awali.

kwa uapande wake Shehe wa mkoa wa Tabora,Shaban salum,aliishukuru benki hiyo kwa tendo lake la kutoa futari kwa waumini wa Imani zote akisema ni utaratibu mzuri unaowaweka pamoja watu wa imani zote na kudumisha mshikamano.

Alieelza ni lazima wananchi wawe pamoja na kuwa na imani tofauti kwa lengo la kudumisha amani na kwamna tofauti za imani zisiwatenganishe wananchi.


mwisho