WACHINA WAKITIKA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI WILAYA YA NZEGA KUJIBU MASHTAKA YA KUPIGA NA KUJERUHI WAFANYAKAZI WAO |
RAIA WA WAKICHINA WAKISHUKA KWEYE MAGARI YAO KATIKA VIWANJWA VYA MAHAKANAI WILAYA YA NZEGA MKOANI TABORA |
NA LUCAS RAPHAEL NZEGA
MAOFISA wa Tatu wa kampuni ya Chanines Communication
and Construction Campany(CCCC) inayohusika na ujenzi wa barabara kutoka nzega
hadi Tabora, wenye athiri ya bara la Asia wamefikishwa katika mahakama ya Hakim
mkazi wilaya ya Nzega kwa tuhuma za kuwapiga walinzi watatu na kuwajeruhi
vibaya.
Mapema jana katika mahakama hiyo waendesha mashitaka wa
Jeshi la polis wilaya wakiongozwa na Inspector Fadhili mpimbwe wameiambia mahakama
hiyo kuwa watuhumiwa watatu wa kampuni ya CCCC wanatuhumiwa kwa makosa ya
kupiga na kujeruhi.
Mpimbwe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Afisa Utawala wa
kampuni hiyo Long Quan(28) mkazi wa Itilo raia wa china, Fundi wa magari Wang
Dong Liang(35)mkazi wa Itilo raia wa china Pamoja na Afisa Usalama Zhang
Han Pang(37) mkazi wa itilo raia wa china.
Mwendesha mashita aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakim
mkazi Slvester Kainda kuwa manamo July 21 mwaka huu majira saa saba usiku
katika kijiji cha Mwanhala watuhumiwa hao waliwapiga na kuwajeruhi vibaya
walinzi watatu wa kampuni hiyo ya ujezni ya CCCC na kuongeza kuwa upelelezi
bado unaendelea.
Mpimbwe aliwataja walinzi hao waliopigwa na maofisa wa
kampuni hiyo kuwa ni Juma sira,Martin Marco pamoja na Samweli Kuli wote wakiwa
wafanya kazi wa kampuni hiyo ya ujenzi katika Idara ya ulinzi,ambapo majeruhi
wawili wamelazwa katika Hosptal ya wilaya ya Nzega huku majeruhi mmoja akiwa
amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya Nkinga wilayani Igunga.
Watuhumiwa hao wamekana kuhusika na tuhuma hizo za kuwa piga
na kujeruhi walinzi wa kampuni hiyo.
Mahakama hiyo imetoa uhuru wa dhamana kwa watuhumiwa hao
huku ikitoa masharti matatu ya kuzingatia katika dhamana hiyo kuwa ni kila
mtuhumiwa kupata mtu mmoja na pesa Tsh,1,000,000, kuwasilisha hati za kusafiria
zote pamoja na kutosafiri nje ya wilaya ya Nzega mpaka kibali maalum cha
mahakama.
Mahakama hiyo imeahilisha shauri hilo hadi mwezi july 30
mwaka huu itakapo anza kusikilizwa.
Aidha Baadhi ya wananchi waliokuwa nje ya mahakama hiyo
wameilalamikia kampuni hiyo ya ujenzi CCCC kutoka China kwa kuwapiga wafanya
kazi wake mara kwa mara pamoja na kutokuwa na mahusiano bora na wananchi.
Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Mwanhala aliyejitambulisha
kwa Juma hamis Selemani ameiomba serikali iingilie kati kuhakikisha mahusiano
bora ya wananchi na wakandarasi hao yanaongezeka.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment