NA LUCAS RAPHAEL,NZEGA
MSIMU wa ununuzi wa
zao la pamba umezinduliwa Rasmi katika kijiji cha Mbogwe kata ya Mbongwe
wilayani Nzega Mkoani Tabora huku bei ya kuanzia kwa kilo moja ya pamba
ikiwa ni shilingi 700 kwa msimu wa mwaka 2013/2014.
Akizindua msimu huo
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatuma Mwasa alisema kuwa bei hiyo ya shilingi 700 ni
bei ya kuanzia na mategemeo yake itazidi kupanda siku hadi siku kutokana na zao
hilo kuwa chache kwa msimu huu wa mavuno.
Alisema kuwa
makampuni ya ununuzi wa zao hilo la pamba yatashindana kuinunua pamba hiyo
ambapo bei hiyo itabadilika kwa manufaa ya mkulima ilikuweza kumpatia faida.
Mkuu huyo alisema
kuwa ilikuweza kudhibiti bei ya pamba kuwa na masirahi kwa wakulima serikali
inatarajia kufufua viwanda vya nyuzi na kuimalisha viwanda vya nguo pamoja na
kuanzisha viwanda vingine ili pamba hiyo iweze kununuliwa hapa nchini kwa bei
itakayo mnufaisha mkulima.
Aliwataka wakulima
kuongeza tija ya kulima zao hilo hapa nchini ambalo halina uhalibifu wa
mazingira kama baadhi ya mazao ya kibiashara na kuongeza kuwa serikali
imejipanga kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za zao hilo kwa muda muafaka
ilikuweza kuendana na kalenda za kilimo hicho.
Aliwataka maofisa
ugani kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma ikiwa na kuandaa mashamba darasa
ya wakulima ambayo yataweza kutoa mwanga kwa wakulima katika kulima pamba kwa
kufuata taratibu za zao hilo.
Kwaupande wake
Mwenyekiti wa Bodi ya pamba Taifa Dkt,Buluma karidushi alisema kuwa bei ya
pamba inatokana na soko la Dunia hata hivyo alisema kuwa jitihada kubwa
zilifanyika hadi kufika bei hiyo.
Alisema kuwa kutokana
na tamko la serikali la kufungua viwanda vya nyuzi litaweza kusaidia kuongeza
bei hiyo ya pamba ambayo itaweza kumfidia mkulima wa zao hilo.
Alisema kuwa
uzalishaji wa pamba mwaka 2012 ulikuwa mkubwa ambapo zaidi ya tani 3.5million
zilizalishwa kitaifa huku mwaka 2013 uzalishaji umeshuka zaidi hadi kufikia
tani zaidi ya 2.5 million.
Mwenyekiti huyo
akizungumzia changamoto za kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo kuwa ni pamoja na
sehemu nyingi kuwa na mafuriko huku sehem nyingine ikiwa na ukame mkubwa.
Alisema sabab u
nyingine ya kushuka ni upatikanaji wa pembejeo ulikuwa hafifu ambao ulitumia
mfumo wa stakabadhi gharani pamoja na kushuka kwa bei ambapo wakulima wengi
walikata tama.
Akitoa tahadhari kwa
wakulima kuwa makini na matapeli dhidi ya pesa bandia ambaopo katika msimu huu
matapeli hayo huingilia biashara hiyo na kujipatia mali kwa njia ya
udanganyifu.
Hata hivyo aliwatoa
hofu wakulima hao kuwa vyombo vya Dora vimejipanga kukabiliana na waharifu hao
kwanyakati mbalimbali ilikuhakikisha wakulima wana uza mazao yao kwa usalama.
Wakizungumza
kwanyakati mbalimbali baadhi ya wakulima wa zao hilo walisema kuwa bei hiyo ya
shilingi 700 bado haijalidhisha kutokana na gharama zauendeshaji wa
kilimo na kuiomba serikali iweke mikakati mikubwa ya kuwaangalia wakulima hao.
Joseph kadoshi
mkulima mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa bei hiyo bado haitoshelezi kulingana
na gharama za uendeshaji wa zao hilo na kuongezxa kuwa serikali iongeze bei
hiyo ifikie 1000 ili mkulima aweze kunufaika na zao hilo la pamba.
‘’Bei hii ya pamba
bado haijaridhisha wakulima nadhani umeona hata walipo tamka ni kias gain
wakulima walikaa kimya jibu hilo hawakulidhika na bei hiyo tunaomba bei ifike
japo 1000 kwani uendeshaji wa kilimo hiki ni mkubwa sana serikali
itusikie’’alisema Joseph kadoshi mkulima wa kijiji hicho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment