NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Sheikh wa mkoa wa Tabora Shaaban Salum akichukua futari wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Benk ya CRDB tawi la Tabora ikiwa ni hatua ya kuwa karibu na wananchi wakiwemo wateja wa Benk hiyo. |
Hawa ni baadhi ya kinamama wa kiislamu waliojumuika pamoja na wafanyakazi wa CRDB katika hafla hiyo mahususi. |
Ilikuwa ni faraja kwa waislamu na wasiowaislamu waliokaribisha na CRDB katika Futari |
Baadhi ya waislamu na viongozi wa vyama vya siasa nao walihudhuria. |
Viongozi wa dini wakiwa katika meza kuu ya hafla hiyo ya Futari. |
Wageni na wafanyabiashara mjini Tabora nao walihudhuria |
Maafisa wa CRDB wakizungumza na msemaji wa waislamu katika hafla hiyo ya Futari. |
BENKI ya CRDB imetoa
futari kwa waumini wa dini ya kiislamu na wasio waumini wa dini hiyo katika
kuwaweka watu wa tofauti pamoja.
Akizungumz akwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo dk charlei kimei,meneja wa mkoa,sydney bakari alisema wameamua kufanya hivyo katika kutimiza wajibu wao kwa jamii
Akizungumz akwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo dk charlei kimei,meneja wa mkoa,sydney bakari alisema wameamua kufanya hivyo katika kutimiza wajibu wao kwa jamii
Dk.Kimei
aliongeza kuwa Benki yake itaendelea kufanya shughuli za kijamii kwa
kushirikiana na Taasisi mbalimbali kusaidia watoto yatima,walemavu,wagonjwa na
waliopatwa na majanga mbambali,wakiamini Benki hiyo inatokana na jamii.
Aliongeza
kwamba CRDB itaendelea na utaratibu wake wa kutenga sehemu ya faida yake ili
kusaidia jamii ambayo ni moja ya sera zake.
katika
kujitanua na kuwasogelea wateja wao,itafungua matawi katika wilaya za Urambo na
sikonge kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Alisema
hata Manispaa ya Tabora pia wameboresha huduma kwa kufungua jengo jipya ambalo
ni kubwa na la kisasa na huduma zake ni bora zaidi kuliko awali.
kwa
uapande wake Shehe wa mkoa wa Tabora,Shaban salum,aliishukuru benki hiyo kwa
tendo lake la kutoa futari kwa waumini wa Imani zote akisema ni utaratibu mzuri
unaowaweka pamoja watu wa imani zote na kudumisha mshikamano.
Alieelza
ni lazima wananchi wawe pamoja na kuwa na imani tofauti kwa lengo la kudumisha
amani na kwamna tofauti za imani zisiwatenganishe wananchi.
mwisho
No comments:
Post a Comment