Nelson Mandela ameendelea kuwekwa hai kwa msaada wa mashine za kumsaidia kupumua na 'anakaribia kifo,' nyaraka za mahakama zimefichua.
Afya ya rais huyo wa zamani ni 'yenye hatari kubwa,' kwa mujibu wa
nyaraka zilizowasilishwa mahakamani kwenye kesi ambayo imepelekea mabaki
ya miili ya watoto wake watatu kuzikwa upya Alhamisi kwenye makaburi
yao ya awali.
Nyaraka za mahakama za Juni 26 zilisema: "Matarajio hayo ya kukaribia kifo chake yanaegemea katika uhalisia na uthabiti,' zilisema nyaraka hizo za mahakama.
Mandela, ambaye alilazwa hospitali Juni 8, ameendelea
kuwa mahututi lakini hali inayoimarika, kwa mujibu wa Ofisi ya Rais
Jacob Zuma, ambaye alimtembelea kiongozi huyo wa mapambano dhidi ya
ubaguzi wa rangi Alhamisi.
Ikulu ya Afrika Kusini imekanusha kwamba Mandela yuko kwenye 'hali ya
kulala tu', na kurejea taarifa zake zilizopita kwamba kiongozi huyo
mpendwa yuko mahututi lakini katika hali inayoimarika.
Ikulu hiyo ilitoa taarifa 'inayofafanua' hali ya Mandela, imeripotiwa.
Walisema: "Tunathibitisha taarifa zetu zilizotolewa awali ... baada ya Rais Jacob Zuma kumtembelea Madiba hospitalini."
Mandela yuko chini ya uangalizi wa karibu wa timu ya wauguzi, ikulu hiyo
ilisema, masaa kadhaa baada ya ripoti hizo za kusisimua za mahakama
kufichuka.
Nyaraka hizo zilisomeka: Wanasema hali ya rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo ni 'yenye hatari kubwa'. "Matarajio ya kukaribia kifo chake yanaegemea katika uhalisia na uthabiti,' ziliongeza.
Nyaraka hizo za kisheria zinahusiana na mapambano makali ya kisheria
yenye chuki kati ya makundi yanayopingana kwenye familia kuhusu wapi
Mandela atakapozikwa.
Baada ya kumchunguza wiki iliyopita, madaktari waliandika:
"Yuko kwenye hali ya kudumu ya kulala tu na anasaidiwa kupumua na mashine ya kuokoa maisha."
Kitabibu, hii inamaanisha hajitambui na yuko kwenye hali katikati ya kuzimia kwa muda mrefu na kifo.
"Kwa kifupi ameshakufa," alisema Charlene Smith, mwandika wasifu wa Mandele aliyethibitishwa.
Taarifa hizo zimekuja huku mabaki ya watoto watatu wa mzee huyo mwenye
miaka 94 yakiwa yamezikwa upya kwenye makaburi yao ya awali kufuatia
amri ya mahamaka kuirejesha miili hiyo baada ya mjukuu wake, Mandla kuwa
ameihamisha.
No comments:
Post a Comment